Nahisi simpendi mke wangu

Pole sana mkuu, kuna swali najiuliza ambalo sijaona jibu lake humu, huyo mwanamke mlifunga ndoa?

Maisha ni yako kaka, hela unatafuta mwenyewe kaka, kama mtu haeleweki ndani ya miaka 10 ataeleweka lini tena? watoto wote watatu bado wadogo ila wa kwanza na wa pili nahisi wanaweza kujihudumia vizur sana

Cha msingi angalia Moyo wako unataka nini, watu wengine wanakuaga wametumwa na shetan kuwaharibia watu, au kukuondolea aman tu, Mwanamke rudisha kwao, tafuta dada wa kazi akusaidie kulea wanao mpaka watakapo kua ndio ufikirie kuoa mwingine, kwa sisi wa kristo dini hairuhusu kuachana ila kuna baadhi ya mazingira inabidi talaka ihusike, na mali za kugawana n mali mlizoshirikiana kutafuta kama kwenye uchumi wa familia hana mchango wowote anataka mali gani?

Utampa kiinua mgongo tu
 
vitabu vina sehemu yake ila sehemu uliyofikia wewe unahitaji maombi, jiombee mwenyewe na familia yako, omba Mungu akuonyeshe njia na nini cha kufanya, anasema njooni wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha, kama una mtumishi wa Mungu unayemwamini mshirikishe kama hauna jua Mungu anasikia maombi yako, na mimi nitakuombea.
 

Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.
 

Pole sana...kwani ni lazima uishi nae au kashakuloga ninii...oa mke mwingine na atakaloamua na aamue kwani atakufanya nini na ukishaoa anza kumpotezea taratibu,matumizi unayapunguza mpaka unaacha kumpa kabisaa akienda usttawi wa jamii utaitwa uwe unatoa matumizi ya watoto unasema uwezo wako ni elfu 30 mwisho wa siku watoto watakufuata wenyewew...mwanamke anaheshimiwa lakini hajieshim wawapi uyoo mxfyuuu sana...hakuna kugawana mali mali andikia watoto nukta.anamwanaume ndo anayemtia bichwa tafuta kipotable uzae nae faster ndo atajibeba vizur
 
Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.
miaka kumi bila ndoa????
 
miaka kumi bila ndoa????

Ndiyo, hakuna mazingira ya kunishawishi kujifunga nira na mtu mwenye moyo kama huo. Mi natafuta namna ya kufanya kwa ajili ya kunusuru afya yangu na amani ya moyo wangu
 
Kuwa makini inawezekana ana ajenda ya siri ya kutaka kukupumzisha kwa amani.
 

Pole !!!!!!!!!!! Huwezi kupata suluhu kwa kumwacha huyo mke na kutafuta mwingine kwani huyo mpya anaweza kuwa mbaya kuliko uliyemwacha na ukimwacha na huyo atakayekuja atakuwa mbaya kuliko waliotangulia na mwisho kabisa utageuziwa kibao kuwa wewe ndio mbaya kwa kuwa kila unayekutana naye ni mbaya kwako. Na mbaya nyingine wale watoto bwana naona mateso kwao hao ulionao kulelewa na mke wa pili na wa mke wa pili na wa kwanza kulelewa na wa tatu na nk

Ninavyojua mimi wanadamu wote ni wazuri kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa MUNGU, ila aliye kinyume na MUNGU amewaharibu ili wafanane na yeye. kwa hiyo kila mtu ni mzuri tu ila aliye ndani yake ndiyo matokeo yake hayo unayoyaona. Na ili aondokane na hayo na wewe uipate amani unayoitamani ni muhimu ukutane na YESU na siyo yesu (usidhani kuwa nakubeza mkuu ila ni kutokana na maelezo yako yamenipelekea kuwa huna YESU bali una yesu)
 
Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.

Very easy, huhitaji akili ya PHD kuamua hili, hamjafunga ndoa, ujue sisi wa kristo vile viapo mbele za Mungu, na mbele za waumini ndio hua vinatufunga kama hamjafunga ndoa mbona issue nyepes tu

simama kama mwanaume, kuanzia sasa tengeneza mazingira kwa wanao, hata mbuzi akili hana lakini ukimfundisha anaelewa, kama saa tano n mda wa kunywa maji kila ukifika huo mda utawaona wanaelekea mtoni wenyewe,

Miaka 10 sio midogo, huyo sio sahihi

Fanya mpango urudi kundini hata kimya kimya, mchungaji anaweza kukurudisha ofisini kwake
 
Ndiyo, hakuna mazingira ya kunishawishi kujifunga nira na mtu mwenye moyo kama huo. Mi natafuta namna ya kufanya kwa ajili ya kunusuru afya yangu na amani ya moyo wangu
saa miaka kumi yote unasubiri nini jamani? huoni kama ungekuwa umeshafanya maamuzi mapema na kuepusha yote hayo, mtu humwamini yet unadiriki kukaa naye miaka kumi na kuzaa watoto watatu naye, mmoja tunaweza sema ok hukujua but three? kama mtu unashindwa kuamini kumuoa, na hakushawishi why ten years with her? it doesn't make sense, nakushauri ufanye maamuzi na uanze maisha, hao watoto unawatesa tu kama wazazi ndio kugombana na kuogopana na nani mbaya hamleti mazingira mazuri kulea watoto, wewe ni mwanaume fanya maamuzi ya kiume. Maisha yako yanatilisha huruma but haileti maana. something is not clear.
 
Amuache ili iweje, hujui kama MUNGU hapendi kuachana? hakuna cha kanisani hapo hiyo tayari ni ndoa (10 yrs wanakaa pamoja na watoto 3 halafu uje na ushauri wa kuwaachanisha wewe. Mungu atakuhukumu wewe huyu jamaa akitoroaa majukumu yake hayo na hatimaye watoto kutaabika kwa ushauri wako huo
 
Acha kulalamika na kufeel sorry for yourself, kama unataka kuwa na furaha amua sasa hakuna kikwazo chochote. Kama hauna furaha sasa ni kutokana na uamuzi wako na wala si wa mtu mwingine, huyo Mwanamke ni none factor as far as i'm concern unless umeamua kuwa Jesus kuifia dunia then hauna sababu ya kulialia.
You have 2 options
1. Kaa na huyo Mama mvumilie huku wewe ukiumia na accept your fate quietly
2. Kick her out, tell her to go as far away as possible from you. Claim your life do the things that makes u happy, (usisahau wanao lakini) You do not owe anybody anything! Go on and live! DO IT NOW
 

Acha kumtisha mwenzio. Amuache kabisa huyo mwanamke na asijichanganye zaidi kwa kuokoka au kuingia kwenye dini kupata suluhisho
 
Kwani kuchat na ex girlfriend wa kaka yao ni kosa...
Unajua wamemjualia wapi...?
Unajua kuna makaka wana date marafiki wa dada zao?

Jamani tujitahidi kuolewa kwetu kusiwe chanzo cha kusambaratisha familia za watu...
Kwani ukifanikiwa kumtenga mumeo na familia yake huwezi kuwa na amani kwenye ndoa yako kama huyu na mkewe...
Kwani mume akiwa hana amani wewe utaitoa wapi...?
kumbuka hao ni nduguze wewe ni mke ...kila mtu ana nafasi yake ...huwezi kuziba nafasi yao....moyoni anasononeka mwisho anakuchoka...


 

Acha kupotosha au hauijui biblia, talaka ipo kwa Wakristo.
 
Umeona eehh

Life's too short, you only live once!

 
pole ndugu jaribu kukaa na mwenzako muongee ai hata utafute mshauri wa mambo ya ndoa anaweza wapa msaada zaidi maana inaonekana kuna mambo mengi sana hapo ili kuyamaliza na kukaa kwa amani lazima kuwe na mazungumzo ya kina.
 
Nilitaka kukazia na miye kwenye elimu...nikaona huruma...

Haya wale wa std 7 ndio mke material njoeni pande hizi mtoe ushauri...


 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…