Kwa hali niliyonayo nahisi hii ni covid 19 3rd wave Delta.
Kwa muda wa wiki nzima hii inayoisha kesho nimekua naumwa ugonjwa usiojulikana. Nimeenda hospitali zaidi ya 2 bado sionyeshi ugonjwa wowote.
Kuanzia jumamosi iliyopita nilikua naumwa kichwa kisicho cha kawaida, nikapewa dawa za kutuliza maumivu lakini wapi, jumatano nikaenda hospitali nyingine nikabadilishiwa dawa kichwa kimeacha kuuma ila mwili hauna nguvu, nimekua mnyonge na dhaifu sana.
Sina ladha ya chakula na wala sitaki kula, nataka muda wote niwe nimelala hadi mbavu zinauma, sihisi harufu yoyote lakini pia nimeanza kuhara mara moja moja na kukohoa kifua kinawasha washa.
Naomba kufahamu hapa Dar ni wapi naweza kwenda kupima covid. Ingawa nimeanza kuona improvement lakini natamani nipime niwe na uhakika.
Ahsante.
Haraka Sana tumia dawa hii.
Nunua bicarbonate of soda nunua na limao ylza kutosha.
Kata limao mbili kama ni ndogo au moja kama ni kubwa kamulia kwenye mug ya kunywea chai. Ondoa mbegu. Chukua nusu kijiko cha chai cha bicarbonate of soda tia kwenye maji ya limao. Itafoka Sana na povu acha itulie halafu chukua maji Moto yanayochemka mimina kwenye kikombe taratibu na itafoka tena na povu. Acha kidogo itulie na chukua kijiko Indoa povu kidogo lililobaki. Kunywa asubuhi, mchana na jioni unapolala.
Ndani ya siku Moja au mbili utarudi kutoa ushuhuda hapa.
Endelea kunywa kwa siku 7 mfulilizo.
Angalizo: Kama Una presha ya kupanda tumia robo kijiko ya bicarbonate of soda.
Wakati huo huo blend matango, limao na ganda lake nusu, tunguu swaumu punje 3, kariti Moja, tangawizi ukubwa wa kidole gumba na majani 5 mchicha kunywa kwa budii.
Kwa ulivyoeleza ni korona na hujapata dawa na unazidi kupoteza muda kirusi kinazidi kuelekea kubaya.
Pambana.
Ila sasa kila siku dalili za korona ziko mitandaoni na matangazo ya serikali hamtaki kusoma maana mnabeza hakuna Korona na wengine wanambeza mheshimiwa Rais. Ni hivi Korona IPO na inaua. Juzi kijijini Moshi huko nilikooa geneza Nne Kanisani kwa mpigo na huko Marangu kwa rafiki yangu marehemu 7 Kanisani kwa ibada.
Tuendekee kuchukua tahadhari.