Nahisi nimenyewa, Mambo yangu yote hayaendi

Tuo Tuo

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
504
874
Wakuu,

Nahisi kabisa toka moyoni kuna mtu kaniwekea kimavi.Yaan vitu vyangu vyote haviendi madili yote yanabuma…

Huwezi amini nikikusimulia aisee,

Kila nachojaribu kinagoma safari hii…Nishapitia msoto lakini huu si msoto n kimavi kabisa.

Naombeni ushauri kama naweza nikatoa hali hii.

Kama huna msaada positive pita ivi! Mi mwenyewe ninna stress! Tusameheane

Jf wadau
 
kuna dawa ukiifanya bila kuidharau ndani ya siku 7...hiyo hali itakutoka na inaanza kuleta matikeo kuanzi siku hiyo hiyo utakayo anza...

kesho panapo majaaliwa asubuhi ukienda kuoga hakikisha maji unayooga unayachanganya na mkojo wako wa asubuhi ule wa kwanza kabisa...maji yanayo hitajika ni ya room temperature ambayo hayajachemshwa mnaita yabaridi. hivyo kama upo kwenye mkoa wenye baridi kazi utakuwa nayo.

hakikisha ndoo inajaa ya rita kumi {sio uijaze mikojo🤣🤣🤣 mkojo ni uo kidogo utakao toka asubuhi ukiwa unakojoa utauchanganya kwenye ndoo yenye maji rita 10 Oga hadi maji yaishe...!

ila kama ukifanya mapenzi na mwanamke ule mkojo ambao umechanganyika na manii haufai.

mkojo unao takiwa ni ule ambao haujachanganyika na manii...!

fanya dawa hiyo kwa kuirudia kila ASUBUHI ndani ya siku 7. baada ya hapo ikikupendeza rudi utoe mrejesho.​
 
Acha na hayo mambo, weka malengo yako fanya tathmini ulifeli wapi, chunguza kwenye tatizo njoo na suluhu na mbinu mpya.
Wabongo wengi wakifeli kidogo tu, hayo mambo ya malengo, tathmini, kufeli wapi, kuchunguza kwenye tatizo, kuja na suluhu, hawataki.

Wanataka uwaambie habari za balaa, laana, kimavi, kuombewa, kutambika, kutafuta mchawi, kwenda kwa waganga wa kienyeji, kusafisha nyota, na ujinga mwingine kama huo.
 
Back
Top Bottom