Bwana Godfrey concern yako kama mdogo wako ni ya kweli ila kiukweli kumwita binti wa miaka 29 bibi haumtendei haki. Je wewe una miaka mingapi na je tukuite babu? Umri wa ujana ukomo wake ni miaka 45 na pia unalikuza mno hilo suala kwasababu labda umemchukia tu huyo binti. 29 na 19 ni tofauti ya miaka 10 kwa mahusiano ya kawaida ya kimapenzi ya kusogeza time siyo vibaya waache waendelee. Mshauri tu dogo azingatie kinga asije kusingiziwa mimba. Kuhusu maradhi hatujui maana tayari wanaendelea labda wamepima wanajijua wenye kama wanakula bila ganda au wanatumia kinga. Kama dogo anataka kufunga naye ndoa unaweza kumshauri kwa busara kwamba aangalie suala la umri. Ila akikataa usilazimisha maana si vizuri kuingilia mahusiano ya ndugu yako mtakuja kugombana bila sababu ya msingi. Kama wazazi wapo basi nashauri waachie wenyewe wamshauri kama anaelekea kutaka kufunga naye ndoa. Maana ni lazima watafuata taratibu. Note: 29 ni umri mdogo sana acha tafsiri hasi kudharau watu. Umri huo unaweza kukuta mwingine bikira hasa aliyejitunza na kujiheshimu katika maadili na malezi ya imani na wazazi wake. Kama msomi pia tumia busara na elimu yako kuchambua mambo. Ukitaka kuomba ushauri usiweke maamuzi yako au kuwa na msimamo maana itakuwa vigumu kupokea ushauri wa watu. Mwisho kama kijana msomi kama ulivyojitambulisha umemaliza chuo, punguza tafsiri hasi kuhusu kazi wanazofanya watu kujipatia chakula. Kazi ya bar ni sawa na kazi nyingine yoyote. Wanaokwenda kunywa wametoka kwenye kazi zao wanaenda kupata huduma na anayewahudumia anafanya kazi naye apate kipato siku ziende. Na siyo kila anayeuza bar ni malaya au alikosa kazi ya kufanya. Natumai ushauri huu pamoja na rai za wengine zitakusaidia wewe binafsi na pia utaendelea kuwa mshauri wa mdogo wako.