Nahisi mdogo wangu amerogwa

Nahisi mdogo wangu amerogwa

Bibi anauza bar? Dogo analelewa. Mahitaji muhimu akiwa shuleni anapata toka kwenu au ndio bibi ana-provide?

sio kwamba kwa sasa anauza baa ila alishawahi kuuza baa hapo alipokuwa msichana!!
 
Bibi ana miaka 29, na dogo ana miaka mingapi? Kuna madogo wana miaka 24 wako a-level. Labda dogo anapenda mapenzi ya kudekezwa/kulelewa. Si ajabu yeye ndo alienda kumuimbisha dada wa watu.

dogo mwezi wa kumi anatimiza miaka 19 ona hilo gap.....
 
hahahaha dunia ina mambo,huyo dogo anafungulia mbwa muache ajifunze kidogo atoe kiwi cha utoto bhana.
 
hahahaha dunia ina mambo,huyo dogo anafungulia mbwa muache ajifunze kidogo atoe kiwi cha utoto bhana.

kamejifanya kwenda kwa huyo bibi kujitambulisha kenyewe, daah huyu dogo karogwa sio bure hapa!!!
 
Mimi niko na dogo kaoa kabisa mwanamke anayemzidi miaka 15. Na wala sikuona ubaya wowote. Halafu upate jua katika maisha tunatafuta furaha na amami.

Waache wafurahie maisha huwezi jua huyo unayemwita bibi kesho akakusaidia.
 
Bwana Godfrey concern yako kama mdogo wako ni ya kweli ila kiukweli kumwita binti wa miaka 29 bibi haumtendei haki. Je wewe una miaka mingapi na je tukuite babu? Umri wa ujana ukomo wake ni miaka 45 na pia unalikuza mno hilo suala kwasababu labda umemchukia tu huyo binti. 29 na 19 ni tofauti ya miaka 10 kwa mahusiano ya kawaida ya kimapenzi ya kusogeza time siyo vibaya waache waendelee. Mshauri tu dogo azingatie kinga asije kusingiziwa mimba. Kuhusu maradhi hatujui maana tayari wanaendelea labda wamepima wanajijua wenye kama wanakula bila ganda au wanatumia kinga. Kama dogo anataka kufunga naye ndoa unaweza kumshauri kwa busara kwamba aangalie suala la umri. Ila akikataa usilazimisha maana si vizuri kuingilia mahusiano ya ndugu yako mtakuja kugombana bila sababu ya msingi. Kama wazazi wapo basi nashauri waachie wenyewe wamshauri kama anaelekea kutaka kufunga naye ndoa. Maana ni lazima watafuata taratibu. Note: 29 ni umri mdogo sana acha tafsiri hasi kudharau watu. Umri huo unaweza kukuta mwingine bikira hasa aliyejitunza na kujiheshimu katika maadili na malezi ya imani na wazazi wake. Kama msomi pia tumia busara na elimu yako kuchambua mambo. Ukitaka kuomba ushauri usiweke maamuzi yako au kuwa na msimamo maana itakuwa vigumu kupokea ushauri wa watu. Mwisho kama kijana msomi kama ulivyojitambulisha umemaliza chuo, punguza tafsiri hasi kuhusu kazi wanazofanya watu kujipatia chakula. Kazi ya bar ni sawa na kazi nyingine yoyote. Wanaokwenda kunywa wametoka kwenye kazi zao wanaenda kupata huduma na anayewahudumia anafanya kazi naye apate kipato siku ziende. Na siyo kila anayeuza bar ni malaya au alikosa kazi ya kufanya. Natumai ushauri huu pamoja na rai za wengine zitakusaidia wewe binafsi na pia utaendelea kuwa mshauri wa mdogo wako.
 
Usipomuacha alternative ni kumkata chululuu yake?
it ain't your call to decide anamdate nani. Mshauri na umuache hapo. Weeh endelea kumuita shemejio bibi, utashaaa siku unaenda kwa ndugu yako na yeye ndio maza hausi.
kwahy mkuu ndugu yako mfano akiwa anatembea na mtu mwenye HIV na wewe unajua utamwacha!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom