Nahisi marehemu alirudi kuniaga

Nahisi marehemu alirudi kuniaga

Pepo hilo mkuu akija mkemee kwa jina la Yesu halitarudi tena
Yeah mkuu...hapo ni hao roho wa nguvu za giza wakiwa kazini kwa njia ya ndoto...marehemu hayupo hai tena. Na hata huko mbinguni hayupo...

Sasa anakuelezaje kuwa eti mbinguni siku hiyo wanajifunza masomo ya biblia..? Kweli kabisa? Nani anawafundisha hayo masomo? Kuna kifungu kwenye biblia kinathibitisha hayo aliyokueleza ndotoni?
 
Huo mtego jamaa wangu.
Akirudi tena na wewe ukaona makaburi ujue na wewe ni RIP
 
Wakuu habari za mihangaiko

Leo naomba kama kuna wataalamu wa mambo ya ulimwengu wa roho naomba mnisaidie kunijibu swali langu hili

Nilikua na rafiki yangu wa kike kiukweli nilimpenda vilivyo
Mimi kipindi namaliza yeye alikua mwaka wa pili
Nilikua nataniana nae sana nilipendelea kumuita strong woman
Kwasababu alikua anajihamini sana na alikua mchangamfu sana na alikua mcha Mungu na nilikua naimba nae kwaya moja
Nakumbuka hata siku namaliza chuo Nilienda kumuaga kama mida ya SAA tatu usiku nikimpa taarifa kua kesho yake nasafiri
Lakini alinipigia simu tena kama saa saba usiku akaniambia asubuhi kabla sijasafiri niende anione tena kwa Mara ya mwisho yaani nikamuage tena

Basi me ilipofika asubuhi nikaamka nikaenda kumuaga tena kama alivyonisihi
Tukaagana vizuri tuu nikaondoka kurejea nyumbani
Siku zikapita nikawa naendelea kuwasiliana nae mchana na usiku

Baada kama ya siku kadhaa kupita akaugua ghafla na mauti yakamkuta
Nakumbuka ilikua muda ya SAA sits mchana nikatumiwa ujumbe kwamba amefariki

Kiukweli nilihisi kama utani nikampigia simu marehemu nikiamini hajafa ni utani tu
Simu yake haikupatikana ikabidi nimtumie SMS
Yani kiujumla nilikua kama nimechanganyikiwa kwa muda huo

Nilipata uhakika baada ya kuona picha zake zikianza kusambaa mitandaoni zikiwa na neno R.I.P

Sikua na namna tena nililia kwa sauti kuu nikimlilia
Nilimlaumu sana marehemu kwanini hakuniaga,
Nilitamani aamke ninuulize hats swali moja kisha alale tena

nilifika mpaka hatua nikaanza kumwomba Mungu aniletee huyu Dada kuna kitu nataka nimuulize kisha amchukue tena.

Zilipita kama siku mbili siku ya tatu nikiwa nimelala nikaota ndoto yule msichana akanijia tukapiga story kisha alivitaka kuondoka akaniambia "usilie sana tusipoonana tena duniani tutaonana mbinguni" akaondoka

niliposhtuka usingizini nilihamaki sana nikajiuliza mini maana ya ndoto hii? Je kweli amerudi kumuaga?

Basi asubuhi nikamuandikia rafiki yangu SMS nikamueleza Jana usiku niliota Grace amekuja na akanisihi tutaonana tena,

Rafiki yangu akanijibu kua ninamuwaza sana ndio maana hadi namuota kwaiyo nipunguze mawazo

Basi nikapotezea

Ikapita kama wiki moja nikiwa nimelala nikaota ndoto tena

Grace akaja tulikua chini ya mti tena mazingira tuliyokuwepo ni mazuri sana nikaongea nae mambo kibao kisha akaniambia anawai sana kwani siku hiyo ni siku ambayo mbinguni wako wanajifunza masomo ya biblia kisha akasepa

Nikashtuka tena usingizini kiukweli nilikosa majibu juu ya hii ndoto
Nilibaki nahamaki sana

Mpaka leo Nahisi marehemu alirudi kuniaga

Wadau kwa yoyote anaeweza kuwa anajua ni mini maana ya hizi ndoto?
Je inawezekana ni kweli marehemu alirudi kumuaga au?
Mkuuhiyo ni dalili mbaya si muda mrefu Israel anakuja kukuchukua saiz anakamilisha visa yako ya kuzimu
 
Yeah mkuu...hapo ni hao roho wa nguvu za giza wakiwa kazini kwa njia ya ndoto...marehemu hayupo hai tena. Na hata huko mbinguni hayupo...

Sasa anakuelezaje kuwa eti mbinguni siku hiyo wanajifunza masomo ya biblia..? Kweli kabisa? Nani anawafundisha hayo masomo? Kuna kifungu kwenye biblia kinathibitisha hayo aliyokueleza ndotoni?
Na wengi hudanganyika wakiamini ni kweli wapendwa wao wamerudi ila ni uongo maana wafu hawajui neno lolote wamelala kwenye kimya mpka ya ufufuo

Hicho kinachowajia ni pepo wachafu wanaochukua miili ya marehemu na kuigiza kila kitu chao ili waaminike na hutoa maelezo kama ya mtoa mada ila sio huwa sio wao

Ni sawa na tukio la mfalme sauli kwenda kwa mwanamke mchawi kumuomba ampandishe Samweli na alifanya hivyo na tunaona wakiwasiliana lkn hakuwa Samweli ila pepo wa mwovu aliyeassume mwili wa Samweli
 
Inasemekana KUWA "siku 30 kabla ya mtu kufa hufanya mambo ya tofauti au mazuri au mabaya".

Mimi zamani nikiwa Teen nilikuwa nikikuota umefariki ndugu yangu wewe andaa wosia maana unakufa kweli kwa sasa naota watu hawafi
Acha kututisha tutakutoa kwenye ukoo
hahahahaha
 
Mkuu, kwanza huyo mdada alikuwa mcha Mungu na mcha Mungu yoyote aliyezama ndani ya Yesu kabla hajaondoka hapa duniani huwa anaaga. Tazama akina Paulo, Yesu n.k
.
.
Mawazo pia yanachangia ila pengine malaika amekuja kupitia sura ya marehemu ili kukwambia ni wapi marehemu alipo baada ya safari yake ya maisha hapa duniani ili kukutia moyo na wewe kukazana ktk imani ili ufikr alipo mtumishi wake aliyetangulia.
.
.
Kumbuka walio ndani ya Kristo hawafi bali wanalala na siku ya mwisho ajapo Kristo wanainuka na Kristo Yesu kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Heri wafu wafao sasa ktk Kristo Yesu.
.
.
Tubu mbele za Mungu na uishi ktk uchaji wake, siku ya hukumu imekaribia, tutubu dhambi zetu tuondolewe ktk habari ya dhambi.
 
Mhubiri 9:5 Wafu hawajui lolote
Zaburi 115:17 Wafu hawawezi kumsifu Bwana
Kumb. 18: 11 Msiombe wafu
2Wakor. 11: 13-15 Shetani na malaika wake (Majini/mapepo) hujigeuza wawe mfano wa waliokufa ili kupotosha neno la Mungu . Kwa kifupi huyo uliyeota sio Grace bali unaongea na pepo kwenye ndoto ambalo huvaa umbo na sura ileile ya mpendwa wako ili uzidi kuamini kuwa kuna maisha yanaendelea baada ya kifo.
Wafu wote watakuwa hai Kristo atakaporudi kuwafufua (Yohana 5:28-29)
 
Mkuu, kwanza huyo mdada alikuwa mcha Mungu na mcha Mungu yoyote aliyezama ndani ya Yesu kabla hajaondoka hapa duniani huwa anaaga. Tazama akina Paulo, Yesu n.
.
.
Mawazo pia yanachangia ila pengine malaika amekuja kupitia sura ya marehemu ili kukwambia ni wapi marehemu alipo baada ya safari yake ya maisha hapa duniani ili kukutia moyo na wewe kukazana ktk imani ili ufikr alipo mtumishi wake aliyetangulia.
.
.
Kumbuka walio ndani ya Kristo hawafi bali wanalala na siku ya mwisho ajapo Kristo wanainuka na Kristo Yesu kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Heri wafu wafao sasa ktk Kristo Yesu.
.
.
Tubu mbele za Mungu na uishi ktk uchaji wake, siku ya hukumu imekaribia, tutubu dhambi zetu tuondolewe ktk habari ya dhambi.

Sawa mkuu
 
Mhubiri 9:5 Wafu hawajui lolote
Zaburi 115:17 Wafu hawawezi kumsifu Bwana
Kumb. 18: 11 Msiombe wafu
2Wakor. 11: 13-15 Shetani na malaika wake (Majini/mapepo) hujigeuza wawe mfano wa waliokufa ili kupotosha neno la Mungu . Kwa kifupi huyo uliyeota sio Grace bali unaongea na pepo kwenye ndoto ambalo huvaa umbo na sura ileile ya mpendwa wako ili uzidi kuamini kuwa kuna maisha yanaendelea baada ya kifo.
Wafu wote watakuwa hai Kristo atakaporudi kuwafufua (Yohana 5:28-29)

Asante mkuu
 
Ndoto hazina jibu moja na wala mtu asije akakuaminisha haraka kuwa ulichoota kimetokana na kitu fulani. Kuna vitu unatazama historia yako unapata majibu. Mie nishaota ndoto za matukio na kesho yake yanatokea kama ilivyo. Nishaonta ndoto hazina maana yoyote. Nishawaota watu ambao hata sijawahi wafikiria akilini mwangu. Nishaota mtu ananiaga na asubuhi nagundua kweli kafa. Nishaota mtu kafa miaka karibu 30 sasa anaishi. Nishaota tukio lilikwisha tokea. Nishaota kama wewe ulivyoota na sio mala moja bali mala nyingi tu. Kuna wanaosema utukane, nakumbuka nilitukana. Wengine watasema tafuta mbinu usiote. Wapo wanaoshauri usiwaze kabisa japo sidhani kama ni tiba. Ndoto ni kama neno lenyewe maana yake nayo ni ndoto kuipata. Tafsiri sahihi na chanzo cha ndoto anacho muotaji mwenyewe. Kama unawaza acha, kama zinakuja tu sawa. Ndoto zingine zinatokea kama kumbusho la unfulfilled promise. Tafakari.
 
Roho zinapotoka hazina haraka kwenda zinakotakiwa. Huwa zinawarudia marafiki/ndugu kumalizana nao kwenye mambo flani flani haswa ahadi. Awezakuja kukuomba umtunzie mtoto au umrudishie mali yake. Haya mambo yapo, huyo ni kweli marehemu alikuja kukuaga
 
Huyo ni shetani mkuu.Uwe unapiga maombi kabla ya kulala.
 
Huyo ni shetani mkuu.Uwe unapiga maombi kabla ya kulala.
 
Back
Top Bottom