Nahisi marehemu alirudi kuniaga

Nahisi marehemu alirudi kuniaga

vnn

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
3,030
Reaction score
7,498
Wakuu habari za mihangaiko

Leo naomba kama kuna wataalamu wa mambo ya ulimwengu wa roho naomba mnisaidie kunijibu swali langu hili

Nilikua na rafiki yangu wa kike kiukweli nilimpenda vilivyo
Mimi kipindi namaliza yeye alikua mwaka wa pili
Nilikua nataniana nae sana nilipendelea kumuita strong woman
Kwasababu alikua anajihamini sana na alikua mchangamfu sana na alikua mcha Mungu na nilikua naimba nae kwaya moja
Nakumbuka hata siku namaliza chuo Nilienda kumuaga kama mida ya SAA tatu usiku nikimpa taarifa kua kesho yake nasafiri
Lakini alinipigia simu tena kama saa saba usiku akaniambia asubuhi kabla sijasafiri niende anione tena kwa Mara ya mwisho yaani nikamuage tena

Basi me ilipofika asubuhi nikaamka nikaenda kumuaga tena kama alivyonisihi
Tukaagana vizuri tuu nikaondoka kurejea nyumbani
Siku zikapita nikawa naendelea kuwasiliana nae mchana na usiku

Baada kama ya siku kadhaa kupita akaugua ghafla na mauti yakamkuta
Nakumbuka ilikua muda ya SAA sits mchana nikatumiwa ujumbe kwamba amefariki

Kiukweli nilihisi kama utani nikampigia simu marehemu nikiamini hajafa ni utani tu
Simu yake haikupatikana ikabidi nimtumie SMS
Yani kiujumla nilikua kama nimechanganyikiwa kwa muda huo

Nilipata uhakika baada ya kuona picha zake zikianza kusambaa mitandaoni zikiwa na neno R.I.P

Sikua na namna tena nililia kwa sauti kuu nikimlilia
Nilimlaumu sana marehemu kwanini hakuniaga,
Nilitamani aamke ninuulize hats swali moja kisha alale tena

nilifika mpaka hatua nikaanza kumwomba Mungu aniletee huyu Dada kuna kitu nataka nimuulize kisha amchukue tena.

Zilipita kama siku mbili siku ya tatu nikiwa nimelala nikaota ndoto yule msichana akanijia tukapiga story kisha alivitaka kuondoka akaniambia "usilie sana tusipoonana tena duniani tutaonana mbinguni" akaondoka

niliposhtuka usingizini nilihamaki sana nikajiuliza mini maana ya ndoto hii? Je kweli amerudi kumuaga?

Basi asubuhi nikamuandikia rafiki yangu SMS nikamueleza Jana usiku niliota Grace amekuja na akanisihi tutaonana tena,

Rafiki yangu akanijibu kua ninamuwaza sana ndio maana hadi namuota kwaiyo nipunguze mawazo

Basi nikapotezea

Ikapita kama wiki moja nikiwa nimelala nikaota ndoto tena

Grace akaja tulikua chini ya mti tena mazingira tuliyokuwepo ni mazuri sana nikaongea nae mambo kibao kisha akaniambia anawai sana kwani siku hiyo ni siku ambayo mbinguni wako wanajifunza masomo ya biblia kisha akasepa

Nikashtuka tena usingizini kiukweli nilikosa majibu juu ya hii ndoto
Nilibaki nahamaki sana

Mpaka leo Nahisi marehemu alirudi kuniaga

Wadau kwa yoyote anaeweza kuwa anajua ni mini maana ya hizi ndoto?
Je inawezekana ni kweli marehemu alirudi kumuaga au?
 
Ngoja wajuzi waje hila inawezekana alikuja mkuu ata kwa mawazo
 
Nakuliza swali nawewe,je ushawah kufanya nae mapnz?je ukaribu wenu ukikuwaje?na tatu je ulikuwa ukimpnda au ushawah kumtamkia kuwa unampndaa?kama jibu ni ndio,je vip reaction yake juu ya wewe kumwambia hivo?kama hujawah je yeye alishawah kukutamkia?kama hapan je uliona dalili za yeye kukutamkia?anyway Inallillah waina illah rajiun
 
Inasemekana KUWA "siku 30 kabla ya mtu kufa hufanya mambo ya tofauti au mazuri au mabaya".

Mimi zamani nikiwa Teen nilikuwa nikikuota umefariki ndugu yangu wewe andaa wosia maana unakufa kweli kwa sasa naota watu hawafi
 
Nakuliza swali nawewe,je ushawah kufanya nae mapnz?je ukaribu wenu ukikuwaje?na tatu je ulikuwa ukimpnda au ushawah kumtamkia kuwa unampndaa?kama jibu ni ndio,je vip reaction yake juu ya wewe kumwambia hivo?kama hujawah je yeye alishawah kukutamkia?kama hapan je uliona dalili za yeye kukutamkia?anyway Inallillah waina illah rajiun
Hapo kwenye rangi,
Umekosea.
 
Maswali haya hayana tija
 
Yaani wewe mwanakwaya ulikuwa unagegedana na mwanakwaya mwenzio afu mnaimba kusifu na kuabudu!!! Hizo Ni salaamu anakuletea utubu kabisa.
Ndo maaana mm na waimba kwaya huwa hatuivi kabisa! Unafiki wa hali ya juu
 
Mkuu wapi nimeandika nilikua namgegeda?
 
Back
Top Bottom