Nahisi mapenzi yamenipotezea dira ya maisha

Mnisamehe kwa post ndefu ila nimejaribu ku-share nanyi hii issue ili tujue jinsi yakuepuka haya mambo.mkuu @choupa @moting jiepushie zahma mtafute huyo binti kwa gharama yoyote umalize hili tatizo.
 
Habarini za muda huu wadau wa MMU!! Ni story ndefu kidogo ila naomba mmivumilie tu ili mnishauri vzr.

Mimi ni kijana ambaye nina elimu ya shahada ya kwanza ambayo niliipata takribani miaka 6 iliyopita katika chuo kimoja kule visiwani Zanzibar.
Nikiwa mwaka wa 2 nilibahatika kupata mtoto mmoja wa kizanzibar ambaye kwa kipindi hcho alikua anasomea masomo ya computer baada ya matokeo yake ya form six kuwa sio mazur kwa maana hakubahatika kwenda chuo. Penzi lilianza kama masihala lakin mwishoni lilikua much serious mpaka kufikia baadhi ya ndugu zangu wa huku kwetu bara akiwemo na mama yangu mzazi kumfaham msichana huyo. Alikua akiwasiliana na bimkubwa wangu kumjulia hali mara kwa mara. Alikua akimtumia vizawadi vya hapa na pale kama kuimarisha penzi letu.
Ni mwanamke ambaye kwao walikua wako vzr kimaisha tofaut na mimi maana kwa kipindi hcho mzee wake alika ana cheo kikubwa sana uhamiaji kwa upande wa zanzibar. Alifikia kunilipia hata sehem ya ada yangu ambayo kwa kipindi hcho cha maisha ya chuo niliila ili kukidhi mahitaji yangu. Nlikua nachukua mkopo wa 80% kutoka loan board so mwaka wa tatu nlikula 20% ya fee ambao mwishon nlilazimika kutopata transcript mpaka nimalizie ada na nlikua sina ila binti akalipa. Ni mengi sana alinifanyia ila kwa kuifanya story isiwe ndef sana hayo yanafaa kuwa mifano ya jinsi mwanamke alivyojitoa akiamini mimi ntakua mume wake wa maisha. Kwa kipindi hcho mim nlikua nampenda pia ilia nikiri tu kua nlikua na akili ya kitoto au nlikosa mawazo thabiti ya kurudisha upendo kwake.
Miaka ikaenda nkafanikiwa kumaliza masomo yangu nikarud zangu DSM jiji la fujo. Nikiwa nyumban binti aliniambia kuna mchongo wa uhamiaji ambapo ameongea na mzee wake kwamba mimi na yeye tuombe then mkwe atatusimamia. Nikafanya hvyo nkaapply na nikaitwa kwa interview nikafanya nikawa nasubir matokeo. Nakumbuka yalichelewa kidogo matokeo yale kama miez kadhaa.
Sasa wakat nasubir matokeo yale nikapata sehem kufanya kaz temporary kama data collector ktk institution moja ambapo nlipewa mkataba wa miez sita. Huko nlikutana na mtoto mmoja wa kinyaturu nkawa nafanya nae kaz. Naye alikua graduate sasa kama unavyojua tukawa tumeanza kuzoeana na kuwa karibu sana. Huku nako penzi likaanza kumea taratibu na ujuavyo mapenz ni ukaribu. Tulikua tunasafir sana mikoan kwa kipindi hcho kwa ajili ya collecting data tukiwa pamoja na huyo bint. Tulikua tunalala pamoja na kuamka pamoja. Binti alinipenda kiasi kwamba mshahara wake ukiingia nikawa mimi ndio namshikia pesa zake na kumpangia matumiz.
Automatically penz la kisiwani likaanza kupwaya tena, na kumbuka nlikua nasubiria matokeo ya interview yangu ya uhamiaji. Binti wa kisiwan akaanza kuhis mabadiliko maana sometimes nikiwa na yule bint simu sipokei na sijib sms. Nikifanikiwa kupokea simu yake akawa anahoji kulikon mbona kama nimebadilika? Mi namjib hakuna mabadiliko nko kawaida tu. Nikaendelea hvyo na huyu bint wa huku bara akahis kitu ktk mawasiliano yangu. Naye akaanza kunichunguza akagundua nko committed somewhere else. Nakumbuka siku moja tukiwa mwanza yule binti wa huku bara akaniambia anaomba nimwambie ukweli nampenda au simpendi nikamjibu nampenda sana maana kiukwel alikua mzur kuliko yule wa kule kisiwani.
Siku moja usiku wa kama saa sita hiv tukiwa tumelala nakumbuka ilikua wilaya ya Sengerema yule bint wa zanzibar akanipigia simu nkawa naitia mute sipokei, huyu binti nliyelala nae akanilazmisha nipokee simu. Nikapokea nikawa najikanyaga tu kuongea. Yule binti akakata simu akanitumia sms ambayo mpaka leo naikumbuka.
"NIMEKUVUMILIA SANA ILA NAONA UMEAMUA KUNIFANYA MIMI MTOTO MDOGO, NIMEJUA KWAMBA UMEPATA MTU ZAIDI YANGU NA UKO KARIBU NAE SANA, SASA BAS KAA UKIELEWA SITOKUTAFUTA TENA NA ILE KAZ HAUTOPATA NSHAMWAMBIA MZEE ASIHANGAIKE TENA. CHUNGA SANA KUHARIBU MAISHA YA WATOTO WA WATU NA HAUTOFANIKIWA KAMWE NA MAISHANI MALIPO HAPAHAP DUNIANI NA UTANIKUMBUKA"
Nikawaza sana usiku mzima sina raha na nkawa nashindwa kupiga tena maana kumbuka nimelala na mtu ambaye pia naye ana wivu sana. Basi asubuh ilipofika nikawa kila nikipiga simu ya mzanzibar haipokelew, nkamtuma mtu ambaye kwa kule alikua rafk yangu akaenda kuongea nae ila binti alikataa katakata. Nkaona labda anatania siku zkapita kila nkimpigia hapokei duh bas nami nkakata tamaa.
Kazi ile miezi sita ikaisha nikarud nyumban, baada ya hapo ndio pale nlipofikia kusema nahis huyu binti kanitia mkos na penzi lake maana sifanikiwa kamwe. Nmeomba kaz mara zaidi ya 1000 maeneo kibao sifanikiwi. Hata ile kaz za kupewa kindugu nkifika mambo yanakua siyo. Nimejarib biashara japo kwa mtaji mdogo ambao napata znafeli kabisa. Nmejarb kufanya hata kilimo wapi sifanikiwa kabisa.
Mwaka jana nliamua kwenda Zanzibar kumtafuta yule binti baada ya kushauriwa na rafiki yangu mmoja kwenda kumuomba msamaha, maana hata namba yake nilishaipoteza kutokana na harakati za maisha ambayo sifanikiwi. Kufika kule nikakuta yule binti ameolewa na anafanya kaz uhamiaji kwa mujib wa mtu ambaye nliongea naye. Hapa napata majibu kwamba kumbe ile kazi yeye alipata. Nikajitahid nikapata namba yake nikampigia nikajitambulisha akaniambia hawez kuongea nimtumie text. Tukaanza kuchat lengo langu likiwa nkutane nae nimweleze kama kuna baya alilifanya katka maisha yangu aniondolee nisonge na maisha yangu. Sasa katika kuchat kumbe mumewe alikua around akaziona zle sms. Dah asee ilikua balaa yule jamaa akanipigia kwa namba nyingne mimi bila kuelewa nikapokea akaanza kunipa mikwara ya kufa mtu ukizingatia kule niko ugenini. Mikwara yake ilikua ni ya kunitishia maisha sana,ilibidi niwe mdogo tu usiku ule na safar yangu nkaona kama haikufanikiwa ikabidi siku iliyofuata nirud zangu DSM. Yule binti hakunipigia wala kunitafuta.
Mpaka leo hii nnapoandika habari hii maisha yangu sion dira kabisa maana nishahangaika kama kijana mpaka nimechoka . Mpaka rafik zangu washalazimisha sana kunitoa rafiki yao ila nao wamechoka. Huwa nakumbana na wakati mgumu sana ninapokua nko na rafiki zangu ambao wana familia zao na wana maisha yao mazur tu. Kuna wakat najikuta mpaka nadondosha chozi nikiwa alone. Naomba sana mungu kwa imani yangu lakin bado sifanikiwi. Najipa moyo kwamba its matter of time lakin naona mambo yanapamba moto na maisha yanakua magumu sana. Sasa wadau naomba ushaur nifanyeje.
Poleni kwa story ndefu kidogo japo nmefupisha sana maana sijaelezea tena upande wa yule binti wa DSM ambaye tulishaachana baada ya kama miez mitatu hiz kumaliza kazi nliyofanya nae.
Wadau Naombeni ushauri wenu tafadhali.
Na Mnyaturu yupo wapi aisee,, au na yeye alishakukimbia umekosa wote.?
 
pole jamaa, ila mnyaturu hapana. ulipata zali ukalitemea mate kwa dharau. komaa tu utafanikiwa
 
Ingekuwa kweli hizo "Laana" wengine tungekuwa tunabeba makopo mtaani
 
Naamini laana ya Zanzibar itakutesa. Kumbuka hayo maneno ya binti wa Zanzibar naamini Mungu kayasikiliza believe or not. Malipo yapo duniani note that huyo binti alitumia a lot of money kukusaidia na bado still looking u for job ukijiona mjanja kumbe ur going to be cursed.
Ushauri wangu uko hivi tubu makosa yako na naamini umejutia pia kama mkristo nenda jieleze kwa viongozi wa imani yako uombewe. My friend hakika hutapata kazi na ukipata hutafrahia milele.
Issue iko hivi rafiki. Binti wa Zanzibar huenda amekuwa mwaminifu kwako sana na alimwambia Mungu juu ya lenu penzi na mungu akaweka tick na kama yule binti kwenye ndoa atapata shida huko alikoolewa remember laana inakuja kwako.
Lack enough hata aliesababisha kumwacha mzanzibar nae umemwacha au umeachwa.

USITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA.
Mrudie muumba wako mapema na ujutie makosa yako bila kufanya hivyo utaingia kwenye ulevi au kuwa teja.
Chukua ushauri wangu then uone kama hutakuja na majibu ya kufanikiwa.

Usidharau chukua hatua from now na baraka za mungu zitakuwa juu yako. AMEN
Ivi we jamaa unamshauri au unamuongezea machungu?
 
Pole sana mkuu, don't lose hope. Two things:
  • Yes ni vizuri kuishi na watu vyema ila achana na kuhusisha imani kwenye matukio ya maisha, especially when it comes to life struggles.Hebu fikiria kuna watu wangapi wame watenda wanawake even worse (kuwazalisha, kuwakatisha masomo na kuwatelekeza )lakini bado wanapeta? Don't take the easy way out! The reality is, it is simpler to blame your situation on her words rather than facing the truth ie may be you lack something or are a simply a failure.
  • Pia despite the progress you see in your friends kumbuka hali ya ajira nchini si nzuri. There are probably million others (i totally made up the number) in a similar situation. i.e graduates with no jobs and zero income. So hang in there inshallah mungu atakujalia in due time
Yani mwanamke kama wewe ni wakuoa kabisa nimependa ujumbe wako asante sana.
 
pole Sana.
katika maisha yenu msipende kuwafanya watu wawasononekee , Kama huna malengo na MTU usimuaminishe!
sononeko la akupendae ni laana kubwa!!
Dada hajakuroga, Ila alisononeka mno!

jifunze sasa...huyo Dada lazima umuombe msamaha!
umemtenda machafu!
Umesema sawa kbsa hakuna jambo baya kusababisho machungu ya moyo kwa mwenzio
 
pole Sana.
katika maisha yenu msipende kuwafanya watu wawasononekee , Kama huna malengo na MTU usimuaminishe!
sononeko la akupendae ni laana kubwa!!
Dada hajakuroga, Ila alisononeka mno!

jifunze sasa...huyo Dada lazima umuombe msamaha!
umemtenda machafu!

Mtoa mada angekuwa mwanamke ungeona wanaume wa jf ambavyo wangeanza kutoka povu, lol princess ariana
 
Pole sana mtaka yote kwa pupa hukosa yote mwombe sana Mungu akusamehe na kukupatia kazi
 
Pole sana mkuu,
Hayo mambo yapo ata usidanganyike na hao wanaosema kama laana wangeipata kulingana na walichowatenda watu wao!

Wewe binafsi ndio unajua mwenzio alijitoa kiasi gani kwako ni vizuri ukatafuta mbinu ya kukutana naye umuombe msamaha!
Huenda binti wa watu alijitunza akiamini wewe ndio mumewe, wewe unakuja kumchezea kirahisi namna hiyo!

Kuna wimbo flani ameimba Alikiba
"unatema big jii kwa karanga za kuonjeshwa,najua mwanamke akipenda huwa kapenda kweli"

Komaaa na maisha huku ukiendelea kutafuta suluhu na huyo mwanamke........
 
Ingependeza kama ungetumalizia mnyaturu yuko wapi na mliacha nae vipi?
 
Pole sana mkuu, don't lose hope. Two things:
  • Yes ni vizuri kuishi na watu vyema ila achana na kuhusisha imani kwenye matukio ya maisha, especially when it comes to life struggles.Hebu fikiria kuna watu wangapi wame watenda wanawake even worse (kuwazalisha, kuwakatisha masomo na kuwatelekeza )lakini bado wanapeta? Don't take the easy way out! The reality is, it is simpler to blame your situation on her words rather than facing the truth ie may be you lack something or are a simply a failure.
  • Pia despite the progress you see in your friends kumbuka hali ya ajira nchini si nzuri. There are probably million others (i totally made up the number) in a similar situation. i.e graduates with no jobs and zero income. So hang in there inshallah mungu atakujalia in due time
U are right.. I always try not to take things personal.. Kama mambo hayaendi sawa kuna people are in worse condition than u are.. Mi mwenyewe nilitafuta kazi mpaka nilihisi nna mkosi, naanza kuwahisi watu nliogombana nao maybe wameshafanya yao (even my own parents!!) Lakini out of no where a call came in.. Kazi hiyo apo [emoji4]

Ilibidi nitubu kwa mawazo mabaya niliyokua nayo juu ya watu ambao maybe hawakua hata na time na mimi..

that's life.. Najua haya nnayoyasema ningeambiwa mimi kipindi nna suffer nisingekuelewa kabisaa [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom