Nahisi mapenzi yamenipotezea dira ya maisha

choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,508
2,560
Habarini za muda huu wadau wa MMU,

Ni story ndefu kidogo ila naomba mmivumilie tu ili mnishauri vizuri.

Mimi ni kijana ambaye nina elimu ya shahada ya kwanza ambayo niliipata takribani miaka 6 iliyopita katika chuo kimoja kule visiwani Zanzibar.
Nikiwa mwaka wa 2 nilibahatika kupata mtoto mmoja wa kizanzibar ambaye kwa kipindi hcho alikua anasomea masomo ya computer baada ya matokeo yake ya form six kuwa sio mazuri kwa maana hakubahatika kwenda chuo.

Penzi lilianza kama masihara lakini mwishoni lilikua much serious mpaka kufikia baadhi ya ndugu zangu wa huku kwetu bara akiwemo na mama yangu mzazi kumfahamu msichana huyo. Alikua akiwasiliana na bimkubwa wangu kumjulia hali mara kwa mara. Alikua akimtumia vizawadi vya hapa na pale kama kuimarisha penzi letu.

Ni mwanamke ambaye kwao walikua wako vizuri kimaisha tofauti na mimi maana kwa kipindi hcho mzee wake alikua ana cheo kikubwa sana Uhamiaji kwa upande wa Zanzibar. Alifikia kunilipia hata sehemu ya ada yangu ambayo kwa kipindi hicho cha maisha ya chuo niliila ili kukidhi mahitaji yangu.

Nlikua nachukua mkopo wa 80% kutoka loan board so mwaka wa tatu nlikula 20% ya fee ambao mwishoni nlilazimika kutopata transcript mpaka nimalizie ada na nilikua sina ila binti akalipa. Ni mengi sana alinifanyia ila kwa kuifanya story isiwe ndefu sana hayo yanafaa kuwa mifano ya jinsi mwanamke alivyojitoa akiamini mimi nitakua mume wake wa maisha.

Kwa kipindi hicho mimi nilikua nampenda pia ilia nikiri tu kuwa nilikua na akili ya kitoto au nilikosa mawazo thabiti ya kurudisha upendo kwake.
Miaka ikaenda nikafanikiwa kumaliza masomo yangu nikarudi zangu DSM jiji la fujo. Nikiwa nyumbani binti aliniambia kuna mchongo wa Uhamiaji ambapo ameongea na mzee wake kwamba mimi na yeye tuombe then mkwe atatusimamia.

Nikafanya hivyo nikaapply na nikaitwa kwa interview nikafanya nikawa nasubiri matokeo. Nakumbuka yalichelewa kidogo matokeo yale kama miezi kadhaa. Sasa wakati nasubiri matokeo yale nikapata sehemi kufanya kazi temporary kama data collector katika institution moja ambapo nilipewa mkataba wa miezi sita.

Huko nlikutana na mtoto mmoja wa Kinyaturu nikawa nafanya nae kazi. Naye alikua graduate sasa kama unavyojua tukawa tumeanza kuzoeana na kuwa karibu sana. Huku nako penzi likaanza kumea taratibu na ujuavyo mapenz ini ukaribu. Tulikua tunasafiri sana mikoani kwa kipindi hicho kwa ajili ya collecting data tukiwa pamoja na huyo binti.

Tulikua tunalala pamoja na kuamka pamoja. Binti alinipenda kiasi kwamba mshahara wake ukiingia nikawa mimi ndio namshikia pesa zake na kumpangia matumizi. Automatically penzi la kisiwani likaanza kupwaya tena, na kumbuka nilikua nasubiria matokeo ya interview yangu ya Uhamiaji.

Binti wa kisiwani akaanza kuhisi mabadiliko maana sometimes nikiwa na yule binti simu sipokei na sijibu sms. Nikifanikiwa kupokea simu yake akawa anahoji kulikoni mbona kama nimebadilika? Mi namjibu hakuna mabadiliko niko kawaida tu. Nikaendelea hivyo na huyu binti wa huku bara akahisi kitu katika mawasiliano yangu. Naye akaanza kunichunguza akagundua niko committed somewhere else.

Nakumbuka siku moja tukiwa Mwanza yule binti wa huku Bara akaniambia anaomba nimwambie ukweli nampenda au simpendi nikamjibu nampenda sana maana kiukweli alikua mzuri kuliko yule wa kule kisiwani.

Siku moja usiku wa kama saa sita hivi tukiwa tumelala nakumbuka ilikua wilaya ya Sengerema yule binti wa Zanzibar akanipigia simu nikawa naitia mute sipokei, huyu binti niliyelala nae akanilazmisha nipokee simu. Nikapokea nikawa najikanyaga tu kuongea. Yule binti akakata simu akanitumia sms ambayo mpaka leo naikumbuka.

"NIMEKUVUMILIA SANA ILA NAONA UMEAMUA KUNIFANYA MIMI MTOTO MDOGO, NIMEJUA KWAMBA UMEPATA MTU ZAIDI YANGU NA UKO KARIBU NAE SANA, SASA BASI KAA UKIELEWA SITOKUTAFUTA TENA NA ILE KAZI HAUTOPATA NISHAMWAMBIA MZEE ASIHANGAIKE TENA. CHUNGA SANA KUHARIBU MAISHA YA WATOTO WA WATU NA HAUTOFANIKIWA KAMWE NA MAISHANI, MALIPO HAPAHAPA DUNIANI NA UTANIKUMBUKA"

Nikawaza sana usiku mzima sina raha na nikawa nashindwa kupiga tena maana kumbuka nimelala na mtu ambaye pia naye ana wivu sana. Basi asubuhi ilipofika nikawa kila nikipiga simu ya mzanzibar haipokelewi, nikamtuma mtu ambaye kwa kule alikua rafiki yangu akaenda kuongea nae ila binti alikataa katakata. Nikaona labda anatania siku zikapita kila nikimpigia hapokei duh basi nami nikakata tamaa.

Kazi ile miezi sita ikaisha nikarudi nyumbani, baada ya hapo ndio pale nilipofikia kusema nahisi huyu binti kanitia mkosi na penzi lake maana sifanikiwa kamwe. Nimeomba kazi mara zaidi ya 1000 maeneo kibao sifanikiwi. Hata ile kazi za kupewa kindugu nikifika mambo yanakua siyo.

Nimejaribu biashara japo kwa mtaji mdogo ambao napata zinafeli kabisa. Nimejarubu kufanya hata kilimo wapi sifanikiwa kabisa. Mwaka jana niliamua kwenda Zanzibar kumtafuta yule binti baada ya kushauriwa na rafiki yangu mmoja kwenda kumuomba msamaha, maana hata namba yake nilishaipoteza kutokana na harakati za maisha ambayo sifanikiwi.

Kufika kule nikakuta yule binti ameolewa na anafanya kazi Uhamiaji kwa mujibu wa mtu ambaye niliongea naye. Hapa napata majibu kwamba kumbe ile kazi yeye alipata. Nikajitahidi nikapata namba yake nikampigia nikajitambulisha akaniambia hawezi kuongea nimtumie text.

Tukaanza kuchat lengo langu likiwa nikutane nae nimweleze kama kuna baya alilifanya katika maisha yangu aniondolee nisonge na maisha yangu. Sasa katika kuchat kumbe mumewe alikua around akaziona zle sms. Dah asee ilikua balaa yule jamaa akanipigia kwa namba nyingine mimi bila kuelewa nikapokea akaanza kunipa mikwara ya kufa mtu ukizingatia kule niko ugenini. Mikwara yake ilikua ni ya kunitishia maisha sana, ilibidi niwe mdogo tu usiku ule na safari yangu nikaona kama haikufanikiwa ikabidi siku iliyofuata nirudi zangu DSM. Yule binti hakunipigia wala kunitafuta.

Mpaka leo hii ninapoandika habari hii maisha yangu sioni dira kabisa maana nishahangaika kama kijana mpaka nimechoka. Mpaka rafiki zangu washalazimisha sana kunitoa rafiki yao ila nao wamechoka. Huwa nakumbana na wakati mgumu sana ninapokua niko na rafiki zangu ambao wana familia zao na wana maisha yao mazuri tu. Kuna wakati najikuta mpaka nadondosha chozi nikiwa alone.

Naomba sana Mungu kwa imani yangu lakini bado sifanikiwi. Najipa moyo kwamba its matter of time lakini naona mambo yanapamba moto na maisha yanakua magumu sana. Sasa wadau naomba ushauri nifanyeje.

Poleni kwa story ndefu kidogo japo nimefupisha sana maana sijaelezea tena upande wa yule binti wa DSM ambaye tulishaachana baada ya kama miezi mitatu hizi kumaliza kazi niliyofanya nae.

Wadau naombeni ushauri wenu tafadhali.
 
Pole sana mkuu, don't lose hope. Two things:
  • Yes ni vizuri kuishi na watu vyema ila achana na kuhusisha imani kwenye matukio ya maisha, especially when it comes to life struggles.Hebu fikiria kuna watu wangapi wame watenda wanawake even worse (kuwazalisha, kuwakatisha masomo na kuwatelekeza )lakini bado wanapeta? Don't take the easy way out! The reality is, it is simpler to blame your situation on her words rather than facing the truth ie may be you lack something or are a simply a failure.
  • Pia despite the progress you see in your friends kumbuka hali ya ajira nchini si nzuri. There are probably million others (i totally made up the number) in a similar situation. i.e graduates with no jobs and zero income. So hang in there inshallah mungu atakujalia in due time
 
Kaka huyo Mzanzibari hahusiki kwa namna yoyte na maisha yako. Pambana mkuu.
Mimi laana za aina hiyo nishazipata kwa wanawake zaidi ya watano. Kuna niliyemzalisha, na mwingine nlipiga mimba afu nkalazmisha atoe. Na nlifikia hadi kuongea na wazee wake.. Na maisha yangu yanasonga vizuri tu. Kaka pambana pambana pambana. Halafu ukishakua na mentality hiyo basi jua hutafanikiwa kweli. Achana naye, yeye siye anayetoa riziki bana. Yeye mwenyewe anamtegemea Mungu tu, atawezaje kuzuia riziki zake kwa laana za kijinga? Kwanz hukuoa. Kwahyo mlikua mnafanya makosa wote, sasa iweje mfanye makosa wote afu uadhibiwe wewe peke yako??!

Achana nae, songa mbele mkuu, yeye hahusiki kabisa hapo acha kupoteza muda
 
Pole sana mkuu, don't lose hope. Two things:
  • Yes ni vizuri kuishi na watu vyema ila achana na kuhusisha imani kwenye matukio ya maisha, especially when it comes to life struggles.Hebu fikiria kuna watu wangapi wame watenda wanawake even worse (kuwazalisha, kuwakatisha masomo na kuwatelekeza )lakini bado wanapeta? Don't take the easy way out! The reality is, it is simpler to blame your situation on her words rather than facing the truth ie may be you lack something or are a simply a failure.
  • Pia despite the progress you see in your friends kumbuka hali ya ajira nchini si nzuri. There are probably million others (i totally made up the number) in a similar situation. i.e graduates with no jobs and zero income. So hang in there inshallah mungu atakujalia in due time
Ushauri mzuri utanifaa sana huu
 
Kaka huyo Mzanzibari hahusiki kwa namna yoyte na maisha yako. Pambana mkuu.
Mimi laana za aina hiyo nishazipata kwa wanawake zaidi ya watano. Kuna niliyemzalisha, na mwingine nlipiga mimba afu nkalazmisha atoe. Na nlifikia hadi kuongea na wazee wake.. Na maisha yangu yanasonga vizuri tu. Kaka pambana pambana pambana. Halafu ukishakua na mentality hiyo basi jua hutafanikiwa kweli. Achana naye, yeye siye anayetoa riziki bana. Yeye mwenyewe anamtegemea Mungu tu, atawezaje kuzuia riziki zake kwa laana za kijinga? Kwanz hukuoa. Kwahyo mlikua mnafanya makosa wote, sasa iweje mfanye makosa wote afu uadhibiwe wewe peke yako??!

Achana nae, songa mbele mkuu, yeye hahusiki kabisa hapo acha kupoteza muda
Ushauri mzuri Mkuu
Namimi Nina mentally hiyo nina story ya kufanana na jamaa
Nitatumia ambacho wew umemshauri
 
Back
Top Bottom