Nahisi mapenzi yamenipotezea dira ya maisha

Nahisi mapenzi yamenipotezea dira ya maisha

Kaka huyo Mzanzibari hahusiki kwa namna yoyte na maisha yako. Pambana mkuu.
Mimi laana za aina hiyo nishazipata kwa wanawake zaidi ya watano. Kuna niliyemzalisha, na mwingine nlipiga mimba afu nkalazmisha atoe. Na nlifikia hadi kuongea na wazee wake.. Na maisha yangu yanasonga vizuri tu. Kaka pambana pambana pambana. Halafu ukishakua na mentality hiyo basi jua hutafanikiwa kweli. Achana naye, yeye siye anayetoa riziki bana. Yeye mwenyewe anamtegemea Mungu tu, atawezaje kuzuia riziki zake kwa laana za kijinga? Kwanz hukuoa. Kwahyo mlikua mnafanya makosa wote, sasa iweje mfanye makosa wote afu uadhibiwe wewe peke yako??!

Achana nae, songa mbele mkuu, yeye hahusiki kabisa hapo acha kupoteza muda
Hahahah huyu jamaa bhn binadamu hana uwezo wa kumlaani binadamu mwenzake hiyo sio laana ni ugumu tuu wa maisha we ondoa hiyo fikra ya kulaaniwa af kaza moyo konde piga kazi kwa malengo utafanikiwa

Achana na imani potofu hizo
 
Habarini za muda huu wadau wa MMU!! Ni story ndefu kidogo ila naomba mmivumilie tu ili mnishauri vzr.

Mimi ni kijana ambaye nina elimu ya shahada ya kwanza ambayo niliipata takribani miaka 6 iliyopita katika chuo kimoja kule visiwani Zanzibar.
Nikiwa mwaka wa 2 nilibahatika kupata mtoto mmoja wa kizanzibar ambaye kwa kipindi hcho alikua anasomea masomo ya computer baada ya matokeo yake ya form six kuwa sio mazur kwa maana hakubahatika kwenda chuo. Penzi lilianza kama masihala lakin mwishoni lilikua much serious mpaka kufikia baadhi ya ndugu zangu wa huku kwetu bara akiwemo na mama yangu mzazi kumfaham msichana huyo. Alikua akiwasiliana na bimkubwa wangu kumjulia hali mara kwa mara. Alikua akimtumia vizawadi vya hapa na pale kama kuimarisha penzi letu.
Ni mwanamke ambaye kwao walikua wako vzr kimaisha tofaut na mimi maana kwa kipindi hcho mzee wake alika ana cheo kikubwa sana uhamiaji kwa upande wa zanzibar. Alifikia kunilipia hata sehem ya ada yangu ambayo kwa kipindi hcho cha maisha ya chuo niliila ili kukidhi mahitaji yangu. Nlikua nachukua mkopo wa 80% kutoka loan board so mwaka wa tatu nlikula 20% ya fee ambao mwishon nlilazimika kutopata transcript mpaka nimalizie ada na nlikua sina ila binti akalipa. Ni mengi sana alinifanyia ila kwa kuifanya story isiwe ndef sana hayo yanafaa kuwa mifano ya jinsi mwanamke alivyojitoa akiamini mimi ntakua mume wake wa maisha. Kwa kipindi hcho mim nlikua nampenda pia ilia nikiri tu kua nlikua na akili ya kitoto au nlikosa mawazo thabiti ya kurudisha upendo kwake.
Miaka ikaenda nkafanikiwa kumaliza masomo yangu nikarud zangu DSM jiji la fujo. Nikiwa nyumban binti aliniambia kuna mchongo wa uhamiaji ambapo ameongea na mzee wake kwamba mimi na yeye tuombe then mkwe atatusimamia. Nikafanya hvyo nkaapply na nikaitwa kwa interview nikafanya nikawa nasubir matokeo. Nakumbuka yalichelewa kidogo matokeo yale kama miez kadhaa.
Sasa wakat nasubir matokeo yale nikapata sehem kufanya kaz temporary kama data collector ktk institution moja ambapo nlipewa mkataba wa miez sita. Huko nlikutana na mtoto mmoja wa kinyaturu nkawa nafanya nae kaz. Naye alikua graduate sasa kama unavyojua tukawa tumeanza kuzoeana na kuwa karibu sana. Huku nako penzi likaanza kumea taratibu na ujuavyo mapenz ni ukaribu. Tulikua tunasafir sana mikoan kwa kipindi hcho kwa ajili ya collecting data tukiwa pamoja na huyo bint. Tulikua tunalala pamoja na kuamka pamoja. Binti alinipenda kiasi kwamba mshahara wake ukiingia nikawa mimi ndio namshikia pesa zake na kumpangia matumiz.
Automatically penz la kisiwani likaanza kupwaya tena, na kumbuka nlikua nasubiria matokeo ya interview yangu ya uhamiaji. Binti wa kisiwan akaanza kuhis mabadiliko maana sometimes nikiwa na yule bint simu sipokei na sijib sms. Nikifanikiwa kupokea simu yake akawa anahoji kulikon mbona kama nimebadilika? Mi namjib hakuna mabadiliko nko kawaida tu. Nikaendelea hvyo na huyu bint wa huku bara akahis kitu ktk mawasiliano yangu. Naye akaanza kunichunguza akagundua nko committed somewhere else. Nakumbuka siku moja tukiwa mwanza yule binti wa huku bara akaniambia anaomba nimwambie ukweli nampenda au simpendi nikamjibu nampenda sana maana kiukwel alikua mzur kuliko yule wa kule kisiwani.
Siku moja usiku wa kama saa sita hiv tukiwa tumelala nakumbuka ilikua wilaya ya Sengerema yule bint wa zanzibar akanipigia simu nkawa naitia mute sipokei, huyu binti nliyelala nae akanilazmisha nipokee simu. Nikapokea nikawa najikanyaga tu kuongea. Yule binti akakata simu akanitumia sms ambayo mpaka leo naikumbuka.
"NIMEKUVUMILIA SANA ILA NAONA UMEAMUA KUNIFANYA MIMI MTOTO MDOGO, NIMEJUA KWAMBA UMEPATA MTU ZAIDI YANGU NA UKO KARIBU NAE SANA, SASA BAS KAA UKIELEWA SITOKUTAFUTA TENA NA ILE KAZ HAUTOPATA NSHAMWAMBIA MZEE ASIHANGAIKE TENA. CHUNGA SANA KUHARIBU MAISHA YA WATOTO WA WATU NA HAUTOFANIKIWA KAMWE NA MAISHANI MALIPO HAPAHAP DUNIANI NA UTANIKUMBUKA"
Nikawaza sana usiku mzima sina raha na nkawa nashindwa kupiga tena maana kumbuka nimelala na mtu ambaye pia naye ana wivu sana. Basi asubuh ilipofika nikawa kila nikipiga simu ya mzanzibar haipokelew, nkamtuma mtu ambaye kwa kule alikua rafk yangu akaenda kuongea nae ila binti alikataa katakata. Nkaona labda anatania siku zkapita kila nkimpigia hapokei duh bas nami nkakata tamaa.
Kazi ile miezi sita ikaisha nikarud nyumban, baada ya hapo ndio pale nlipofikia kusema nahis huyu binti kanitia mkos na penzi lake maana sifanikiwa kamwe. Nmeomba kaz mara zaidi ya 1000 maeneo kibao sifanikiwi. Hata ile kaz za kupewa kindugu nkifika mambo yanakua siyo. Nimejarib biashara japo kwa mtaji mdogo ambao napata znafeli kabisa. Nmejarb kufanya hata kilimo wapi sifanikiwa kabisa.
Mwaka jana nliamua kwenda Zanzibar kumtafuta yule binti baada ya kushauriwa na rafiki yangu mmoja kwenda kumuomba msamaha, maana hata namba yake nilishaipoteza kutokana na harakati za maisha ambayo sifanikiwi. Kufika kule nikakuta yule binti ameolewa na anafanya kaz uhamiaji kwa mujib wa mtu ambaye nliongea naye. Hapa napata majibu kwamba kumbe ile kazi yeye alipata. Nikajitahid nikapata namba yake nikampigia nikajitambulisha akaniambia hawez kuongea nimtumie text. Tukaanza kuchat lengo langu likiwa nkutane nae nimweleze kama kuna baya alilifanya katka maisha yangu aniondolee nisonge na maisha yangu. Sasa katika kuchat kumbe mumewe alikua around akaziona zle sms. Dah asee ilikua balaa yule jamaa akanipigia kwa namba nyingne mimi bila kuelewa nikapokea akaanza kunipa mikwara ya kufa mtu ukizingatia kule niko ugenini. Mikwara yake ilikua ni ya kunitishia maisha sana,ilibidi niwe mdogo tu usiku ule na safar yangu nkaona kama haikufanikiwa ikabidi siku iliyofuata nirud zangu DSM. Yule binti hakunipigia wala kunitafuta.
Mpaka leo hii nnapoandika habari hii maisha yangu sion dira kabisa maana nishahangaika kama kijana mpaka nimechoka . Mpaka rafik zangu washalazimisha sana kunitoa rafiki yao ila nao wamechoka. Huwa nakumbana na wakati mgumu sana ninapokua nko na rafiki zangu ambao wana familia zao na wana maisha yao mazur tu. Kuna wakat najikuta mpaka nadondosha chozi nikiwa alone. Naomba sana mungu kwa imani yangu lakin bado sifanikiwi. Najipa moyo kwamba its matter of time lakin naona mambo yanapamba moto na maisha yanakua magumu sana. Sasa wadau naomba ushaur nifanyeje.
Poleni kwa story ndefu kidogo japo nmefupisha sana maana sijaelezea tena upande wa yule binti wa DSM ambaye tulishaachana baada ya kama miez mitatu hiz kumaliza kazi nliyofanya nae.
Wadau Naombeni ushauri wenu tafadhali.
Sikiliza haya kijana; epuka kufikiria umerogwa, na achana kabisa na kasumba hio. Jua kwamba sio kila mwanamke utae kutana naye atakua mkeo. Utakuja shangaa utakaye muowa.
Pigana na maisha, na nasema Mara zote aliwazalo mjinga ndilo humtokea. Jiwazie mazuri mengi yaliyopo mbele yako. Niwengutu wanapitia changamoto zaidi ya hili lako. Jua mungu hamtupi muja wake. Think positive about yourself utawanikiwa. Ukianza kujiwazia negatively, hutokae ufanikiwe. Ji keep bize, tafuta vi simple job, na kama nikabiashara kako, dedicate yourself kwa hip biashara.
Tafadhali, potezea mbali kabisa huo ujinga wa Zanzibar, na tena kaolewa, ndo mpotezee kabisa. Tumia nguvu zako zote kutafuata ajira.
La mwisho, soma nyakati. Kwasasa, sio mfanya kazi, wala mfanya biashara, wala mkulima, hali ningumu tena sana. Keep the fight, and don't give up, utatoboa kimaisha. Kuna watu wametuma maombi ya kazi Mara 10,000 na bado hajapata, sembuse wewe Mara 1000 tuu. Utapata na utafanikiwa, tens shukuru mungu baba yake hakupa hiyo kazi. Ungenyanyaswa mpaka basi, sababu kingekua kigezo cha wewe kumuoa. Shukuru mungu kwa hill, Leo upon huru kuja kuoa utakae kuja mpenda. God bless and keep the fire of success burning in you and don't let anyone make you loose hope. Enjoy your life and your day!
 
Tujifunze kuishi na watu vizuri, huwezi jua ya kesho
 
Tatizo lako ni la kisaikolojia zaidi na wala sio laana ya mwanamke wa Ki - Zanzibari.
 
Naamini laana ya Zanzibar itakutesa. Kumbuka hayo maneno ya binti wa Zanzibar naamini Mungu kayasikiliza believe or not. Malipo yapo duniani note that huyo binti alitumia a lot of money kukusaidia na bado still looking u for job ukijiona mjanja kumbe ur going to be cursed.
Ushauri wangu uko hivi tubu makosa yako na naamini umejutia pia kama mkristo nenda jieleze kwa viongozi wa imani yako uombewe. My friend hakika hutapata kazi na ukipata hutafrahia milele.
Issue iko hivi rafiki. Binti wa Zanzibar huenda amekuwa mwaminifu kwako sana na alimwambia Mungu juu ya lenu penzi na mungu akaweka tick na kama yule binti kwenye ndoa atapata shida huko alikoolewa remember laana inakuja kwako.
Lack enough hata aliesababisha kumwacha mzanzibar nae umemwacha au umeachwa.

USITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA.
Mrudie muumba wako mapema na ujutie makosa yako bila kufanya hivyo utaingia kwenye ulevi au kuwa teja.
Chukua ushauri wangu then uone kama hutakuja na majibu ya kufanikiwa.

Usidharau chukua hatua from now na baraka za mungu zitakuwa juu yako. AMEN
 
Kaka huyo Mzanzibari hahusiki kwa namna yoyte na maisha yako. Pambana mkuu.
Mimi laana za aina hiyo nishazipata kwa wanawake zaidi ya watano. Kuna niliyemzalisha, na mwingine nlipiga mimba afu nkalazmisha atoe. Na nlifikia hadi kuongea na wazee wake.. Na maisha yangu yanasonga vizuri tu. Kaka pambana pambana pambana. Halafu ukishakua na mentality hiyo basi jua hutafanikiwa kweli. Achana naye, yeye siye anayetoa riziki bana. Yeye mwenyewe anamtegemea Mungu tu, atawezaje kuzuia riziki zake kwa laana za kijinga? Kwanz hukuoa. Kwahyo mlikua mnafanya makosa wote, sasa iweje mfanye makosa wote afu uadhibiwe wewe peke yako??!

Achana nae, songa mbele mkuu, yeye hahusiki kabisa hapo acha kupoteza muda
Laana haijalishi mkuu kumbuka amemgharamikia akiwa chuoni na bado walikubaliana kuoana. So yampasa kumrudia mungu wake. Ahadi pekee na uongo aliosema kwa binti ni laana tosha.
Amrudie mungu wake kwa toba
 
Aiseee hakuna kitu kizur kama kupata mwanamke anaekupenda na Baba yake anakupenda pia aisee hata Ku cheat sio mpaka astuke daaah
 
Laana haijalishi mkuu kumbuka amemgharamikia akiwa chuoni na bado walikubaliana kuoana. So yampasa kumrudia mungu wake. Ahadi pekee na uongo aliosema kwa binti ni laana tosha.
Amrudie mungu wake kwa toba
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kutoa laana kwa binadamu mwenzake.. Hata Mungu anatupa vingi sana na bado tunamkosea sana. Na wala hatoi laaana..
Hebu imagine wewe uliyepewa pumzi ya bure kabisa, halafu unafikia hatua hali unafanya mapenzi kinyume na maumbile!! Ni jinsi gani Mungu anakasirika? Ni vipi Mungu tunamuudhi? Kwanini bado wanaofanya matendo hayo bado wanabarikiwa daily na wala hawana shida katika maisha ya dunia?
Hapo cha kufanya ni kumuomba Mungu tu, atafungua mambo, lakni nasisitiza kuwa MZANZIBARI HAHUSIKI HAPO KATIKA RIZIKI YA JAMAA.
 
Pole sana, Mkuu.
Mshirikishe Mungu, ktk hali unayoipitia. Ukifanya hivi naamini utafanikiwa pia achana na imani hizo kuwa inawezekana mtu amekuzuilia riziki yako hayo ni mawazo tu! Usikate tamaa songa mbele, bahati yako ipo tena umeikaribia sana kuifikia.
 
pole Sana.
katika maisha yenu msipende kuwafanya watu wawasononekee , Kama huna malengo na MTU usimuaminishe!
sononeko la akupendae ni laana kubwa!!
Dada hajakuroga, Ila alisononeka mno!

jifunze sasa...huyo Dada lazima umuombe msamaha!
umemtenda machafu!
 
Mkuu cyo kila hisia ni zakuchezea chezea tu hisia zingine kaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hakuna msaada hapo.. umechezea shilingi kwenye tundu la choo...
 
Amini usiamini yale maneno aliyokutumia ktk sms ndo yalokuvurugia maisha yako na hujui huko alikokuwa alikufanyia kitendo gani,solution ni kumtafuta uso kwa macho na kumuomba msamaha otherwise utazidi kupotea ktk line ya maisha yako...alinuia na ili kuiondoa hii laana yakubidi uwe mdogo kushinda sisimizi ili akusamehe kwa moyo wake wote,nakotokea kuna familia moja naijua vizuri mabinti ktk nyumba yao hawaolewi,wapo kama nane/saba hivi siku moja sina cha kuuliza nipo na marehemu babu yangu nikamletea uzushi kutaka kujua..kwanza alinipa onyo niuheshimu sana ujana wangu ktk njia zangu nikitaka kupata mke,niepuke kuahidi ahadi zisizotekelezeka,akaniambia ile nyumba tatizo lilianza pale baba wa familia alipomuahidi dada mmoja pale kijijini kwamba atamuoa,ila amsubiri kwanza akatafute maisha ataporudi waanze maisha,alikaa almost miaka 9 binti anamsubiri kurudi akarudi ana mke na watoto tayari,binti alipopata taarifa akenda kumuhoji kwa amani tu imekuwaje yeye amewakataa wanaume chungu nzima akimsubiri yeye ila amerudi na mke so nini hatma yake jamaa akamtukana na kumfukuza,dada kwa hasira alipofika mwisho wa shamba la jamaa akainua gauni lake akabaki na nguo ya ndani tu nakuinama huku makalio kayaelekeza nyumbani kwa jamaa huku akitamka “ktk nyumba hii ya(akimtaja jina)watoto wa kike wasiolewe wawe na mkosi kama alivyonipa yeye mkosi na uzazi wao wamzalie wajukuu hapa hapa nyumbani kwake",believe me haya yalitokea...mabinti walikuwa wanapata wachumba,kuwatambulisha nyumbani but mara ujauzito mchumba haonekani wanazaa maisha yanasonga mpaka wote nane hakuna aliyesalimika mmoja wa mwisho ndo alitegemewa angesoma but akiwa form four nae akapitiwa.mwanamke akinuia jambo kwa mabaya impact yake kwa muhusika ni gharika nzito.
 
Sikiliza haya kijana; epuka kufikiria umerogwa, na achana kabisa na kasumba hio. Jua kwamba sio kila mwanamke utae kutana naye atakua mkeo. Utakuja shangaa utakaye muowa.
Pigana na maisha, na nasema Mara zote aliwazalo mjinga ndilo humtokea. Jiwazie mazuri mengi yaliyopo mbele yako. Niwengutu wanapitia changamoto zaidi ya hili lako. Jua mungu hamtupi muja wake. Think positive about yourself utawanikiwa. Ukianza kujiwazia negatively, hutokae ufanikiwe. Ji keep bize, tafuta vi simple job, na kama nikabiashara kako, dedicate yourself kwa hip biashara.
Tafadhali, potezea mbali kabisa huo ujinga wa Zanzibar, na tena kaolewa, ndo mpotezee kabisa. Tumia nguvu zako zote kutafuata ajira.
La mwisho, soma nyakati. Kwasasa, sio mfanya kazi, wala mfanya biashara, wala mkulima, hali ningumu tena sana. Keep the fight, and don't give up, utatoboa kimaisha. Kuna watu wametuma maombi ya kazi Mara 10,000 na bado hajapata, sembuse wewe Mara 1000 tuu. Utapata na utafanikiwa, tens shukuru mungu baba yake hakupa hiyo kazi. Ungenyanyaswa mpaka basi, sababu kingekua kigezo cha wewe kumuoa. Shukuru mungu kwa hill, Leo upon huru kuja kuoa utakae kuja mpenda. God bless and keep the fire of success burning in you and don't let anyone make you loose hope. Enjoy your life and your day!

Japo ushauri wako ni wa ki-hip hop ila well sid bro. Thanx very much and god bless u forever.
 
Naamini laana ya Zanzibar itakutesa. Kumbuka hayo maneno ya binti wa Zanzibar naamini Mungu kayasikiliza believe or not. Malipo yapo duniani note that huyo binti alitumia a lot of money kukusaidia na bado still looking u for job ukijiona mjanja kumbe ur going to be cursed.
Ushauri wangu uko hivi tubu makosa yako na naamini umejutia pia kama mkristo nenda jieleze kwa viongozi wa imani yako uombewe. My friend hakika hutapata kazi na ukipata hutafrahia milele.
Issue iko hivi rafiki. Binti wa Zanzibar huenda amekuwa mwaminifu kwako sana na alimwambia Mungu juu ya lenu penzi na mungu akaweka tick na kama yule binti kwenye ndoa atapata shida huko alikoolewa remember laana inakuja kwako.
Lack enough hata aliesababisha kumwacha mzanzibar nae umemwacha au umeachwa.

USITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA.
Mrudie muumba wako mapema na ujutie makosa yako bila kufanya hivyo utaingia kwenye ulevi au kuwa teja.
Chukua ushauri wangu then uone kama hutakuja na majibu ya kufanikiwa.

Usidharau chukua hatua from now na baraka za mungu zitakuwa juu yako. AMEN

Nashukur bro tuko pamoja sana
 
hapo ni hisia zako tu kuwa mzanzibar kakupa mikosi but nothing acha kuamini hicho kit maisha ni fumbo wakat mwingine mtu hujaribiwa ili kuon kma utahimili hyo mikikimikiki jiamini na amini ipo siku utafanikiwa
 
Salama yako kwanza ni Mungu, muombe sana na ufanye toba hasa, na pili ni huyo dada siwezi kusema amekuroga ama la maana yote yanawezekana, ila mtafute nenda z'bar ofisini kwao omba kuonana nae muombe radhi
 
Back
Top Bottom