Nahisi kuchezewa mchezo mchafu na mtu niliemuajiri dukani kwangu

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
176
Ni miezi sita sasa tangu nilipofungua biashara ya kuuza duka la jumla na rejareja.

Kutokana na u-busy wa majukumu nikaamua kumpa ajira msichana pale dukani ili tusaidiane maisha cha ajabu yule mdada baada ya miezi minne ananiambia majirani zake pale dukani wanamchezea michezo ya kishirikina anakuta damu ndani ya duka akifungua asubuhi.

Wakati mwingine anazikuta nje ya mlango na tangu alivyoanza kuniambia mambo hayo nimekuwa sina sauti tena kwake. Vitu vinaisha na hela siion na nikienda nikimuangalia tu usoni nguvu ya kumuuliza nakuwa sina, amekuwa kama yeye ndio boss anapanga kila kitu cha kufanya.

Mara ananiambia hapendi ninavyoenda pale dukani kwasababu kuna wateja wake wakiniona hawaji kununua vitu.

Inafika wakati napanga kwenda kumfukuza kazi lakini nikifika naishiwa nguvu siwezi kumfanya chochote.

Sasa nimeongea na baadhi ya watu wakaribu wameniambia kuwa yule binti sio mtu mzuri niwe nae makini.

Sasa nahisi amenichezea mchezo mbaya na kwenda kwa waganga ili nisiwe na mamlaka kwenye biashara yangu. Wadau this is serious kabisa yani.

IMG_20200702_015718.jpeg
 
Muondoe kisiasa tu mwambie mambo hayaendi vyema unataka kufunga duka mpe chake ajikatae nunua vitu weka mtu mwengine utakaemmudu na atakaemudu hiyo kazi kwa uaminifu.

We utamuelewaje mtu kwa visingizio vya uchawi.. komalia hesabu zako tu mpk akome atachoka ataacha akizungumzia ati kuna wachawi mwambie Hilo anajua yeye wewe unachojua ni hela tu.
 
Weka CCTV Camera dukani kwanza wakati unafanya mpango wa kumtimua. Na mpaka unaandika hivi ushajitambua aka dawa imeisha.

Ila jamani haya mambo yapo mie nimesoma haswa na nilikuwa siamini mambo ya kiswahili kwenye biashara sasa kuna kipindi nilinunua Coaster mbili nikawa nazikodisha kwenye shughuli kama misiba, harusi na si daladala.

Kila gari ilikuwa na dereva wake. Sasa kuna dereva mmoja alinichezea yaani nilikuwa sina sauti kwake kabisa wakati mwingine nilikuwa ninammudu haswa.

Baadae yule mwingine ndio akanieleza kuwa yule dereva ananiendea kwa waganga ili nisiwe na sauti kwake. na kweli sikuwa na sauti nilikuwa napanga nimtimue ila nikikutana nae najishangaa kila akiongea nakubaliana nae. Uchawi upo kwenye biashara
 
Kaka mshukuru Mungu kitendo cha kujua tu hayo basi unaufaham chukua hatua Kali sana piga nae hesabu kisha mtimue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom