PAPAKINYI - SJUT 2013
JF-Expert Member
- Jun 5, 2017
- 367
- 251
Jana Halila Yusuf Tongolanga (1965-2017) amezikwa kijijini kwao Tandahimba.
Hakuna asiyemfahamu huyu mtu kwa kazi zake za kisanii zilizobamba sana sana.. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa hadi kutumika katika matamasha mbalimbali na wakubwa...
Wamakonde walipata umaarufu na kimakonde chao sababu ya huyu jamaa. mi binafsi nilikuwa na bado ni mpenzi sana wa nyimbo zake... Naipenda sana ile 'chilambo cha vene!
Wadau, nilichokiona na kusikia katika mazishi yake. Nimelia, ninalia na nitaendelea kulia hadi mwisho wa maisha yangu, bila shaka.
Kusema inasikitisha naona haitoshi..
1. Alianza kuumwa akiwa Dar, mama yake (75) alimtumia nauli ili arudi... Baada ya mwanae huyo kumpigia simu kila siku kuwa 'mama mi naumwa'. ilimlazimu kutuma nauli sababu mwanae huyo hakuwa na chochote.
2. Balozi wa Msumbiji ndiye mwanaserikali pekee aliyeenda kumjulia hali wakati wa ugonjwa wake.
3. Zaidi ya redio Pride Fm ya Mtwara, sijui kama kuna chombo chochote kingine kimejali kuhusu kifo chake.
4. Mama yake alipoulizwa alichoweza kufanya, alijibu ameacha banda la vyumba viwili kijijini.
5. Wabunge wa Mtwara wote, ukitoa Katani wa Tandahimba. Hawakuhudhuria msiba huo na badala yake wamechanga tshs. 700,000/=. Pia hakukuwa na uwakilishi wowote toka serikalini.
6. Wasanii km Harmonize ambaye Mtwara ni kwao, hata pole hajatoa!
Hey great thinkers, nikiangalia na kile kilimchomkuta yule mzee mchora nembo ya taifa na wengine, wallah nayaona maisha hayana maana kabisa.
Hata sijui nimlaumu nani na kivipi, najihisi kuchanganyikiwa tu na hii dunia 'the saddest world' kama alivyosema Celine Dion.
Naomba mchango wenu pengine nitaelewa jambo!