Nahisi kuchanganyikiwa, ina maana Tongolanga hakuwa muhimu?

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
367
251
Jana Halila Yusuf Tongolanga (1965-2017) amezikwa kijijini kwao Tandahimba.

Hakuna asiyemfahamu huyu mtu kwa kazi zake za kisanii zilizobamba sana sana.. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa hadi kutumika katika matamasha mbalimbali na wakubwa...

Wamakonde walipata umaarufu na kimakonde chao sababu ya huyu jamaa. mi binafsi nilikuwa na bado ni mpenzi sana wa nyimbo zake... Naipenda sana ile 'chilambo cha vene!

Wadau, nilichokiona na kusikia katika mazishi yake. Nimelia, ninalia na nitaendelea kulia hadi mwisho wa maisha yangu, bila shaka.

Kusema inasikitisha naona haitoshi..

1. Alianza kuumwa akiwa Dar, mama yake (75) alimtumia nauli ili arudi... Baada ya mwanae huyo kumpigia simu kila siku kuwa 'mama mi naumwa'. ilimlazimu kutuma nauli sababu mwanae huyo hakuwa na chochote.

2. Balozi wa Msumbiji ndiye mwanaserikali pekee aliyeenda kumjulia hali wakati wa ugonjwa wake.

3. Zaidi ya redio Pride Fm ya Mtwara, sijui kama kuna chombo chochote kingine kimejali kuhusu kifo chake.

4. Mama yake alipoulizwa alichoweza kufanya, alijibu ameacha banda la vyumba viwili kijijini.

5. Wabunge wa Mtwara wote, ukitoa Katani wa Tandahimba. Hawakuhudhuria msiba huo na badala yake wamechanga tshs. 700,000/=. Pia hakukuwa na uwakilishi wowote toka serikalini.

6. Wasanii km Harmonize ambaye Mtwara ni kwao, hata pole hajatoa!

Hey great thinkers, nikiangalia na kile kilimchomkuta yule mzee mchora nembo ya taifa na wengine, wallah nayaona maisha hayana maana kabisa.

Hata sijui nimlaumu nani na kivipi, najihisi kuchanganyikiwa tu na hii dunia 'the saddest world' kama alivyosema Celine Dion.

Naomba mchango wenu pengine nitaelewa jambo!
 
mimi binafsi simjui,na kama alikuwa maarufu hivyo ni kwamba alikuwa anafanya show/muziki bure au?isije kuwa tunaanza kumimina sympathy kumbe alikuwa mhongaji mzuri
 
Binafsi simjui na sijui alikuwa anahusika na nini. Lakini ni vyema tukaweka akilini kuwa pale tutakapoifanyia serikali kazi maalum ni vyema tukadai chetu palepale, baadae hakuna atakae jali. Tujenge mazingira mazuri ya watoto wetu na sisi wenyewe ili kuepuka fedheha baadae.
 
Huyu jamaa alikuwa msanii sawa. sasa ndugu yangu ulitaka jamii na serikali vifanye nini. maisha yako yatajengwa na wewe mwenyewe. kama huwezi kujihurumia, hakuna wa kukuhurumia. Dunia hii ni katili. huyo jamaa kama alikubali kufanya matamasha ya kisiasa bure utamlaumu nani?
 
sawa, lkn sina uhakika km nitakuwa hai muda wote maandalizi ya maisha yake....jamii inahusika pia!

Hiyo jamaa unayoililia itakuwa busy kulea watoto wake. Future ya wanao ipo mikononi mwako peke yako, siyo hata ya ndugu zako achilia mbali jamii.
Andalia wanao vyema, ikitokea jamaa wakashow sympathy itakuwa ni bonus
 
Mleta mada nadhani huyo aliyefariki ni baba ako au ndugu wa karibu yako, na sasa unataka tukuchagie chochote kitu.

Haiwzekani mtu hafaamiki miaka yote afu leo unaitupia serikali lawama. Japo mimi binafsi naichukia hii serikali ya JPM lakini not to that extent aise.

Ila kwakuwa ni mmakonde tafadhali kwa mwenye Namba ya Nape ampm mleta mada
 
Ungeweka na picha ya huyo marehemu tumuone.

jana Halila Yusuf Tongolanga (1965-2017) amezikwa kijijini kwao tandahimba.

hakuna asiyemfahamu huyu mtu kwa kazi zake za kisanii zilizobamba sana sana...umaarufu wake ulikuwa mkubwa hadi kutumika katika matamasha mbalimbali na wakubwa...wamakonde walipata umaarufu na kimakonde chao sababu ya huyu jamaa. mi binafsi nilikuwa, na bado ni mpenzi sana wa nyimbo zake...naipenda sana ile 'chilambo cha vene!!

wadau, nilichokiona na kusikia katika mazishi yake...nimelia, ninalia na nitaendelea kulia hadi mwisho wa maisha yangu, bila shaka. kusema inasikitisha naona haitoshi.....
1. alianza kuumwa akiwa dar, mama yake (75) alimtumia nauli ili arudi...baada ya mwanae huyo kumpigia simu kila siku kuwa 'mama mi naumwa'. ilimlazimu kutuma nauli sababu mwanae huyo hakuwa na chochote.
2. balozi wa msumbiji ndiye mwanaserikali pekee aliyeenda kumjulia hali wakati wa ugonjwa wake
3. zaidi ya redio pride fm ya mtwara, sijui kama kuna chombo chochote kingine kimejali kuhusu kifo chake.
4. mama yake alipoulizwa alichoweza kufanya, alijibu ameacha banda la vyumba viwili kijijini.
5. wabunge wa mtwara wote, ukitoa katani wa tandahimba, hawakuhudhuria msiba huo na badala yake wamechanga tshs. 700,000/=. pia hakukuwa na uwakilishi wowote toka serikalini.
6. wasanii km harmonize ambaye mtwara ni kwao, hata pole hajatoa!

hey great thinkers, nikiangalia na kile kilimchomkuta yule mzee mchora nembo ya taifa na wengine, wallah nayaona maisha hayana maana kabisa...hata sijui nimlaumu nani na kivipi, najihisi kuchanganyikiwa tu na hii dunia 'the saddest world' km alivyosema celine dione....naomba mchango wenu pengine nitaelewa jambo!!!!!
 
Back
Top Bottom