Nahisi kuachwa na niliempenda

Nahisi kuachwa na niliempenda

Ngoja akabadilishwe gia angani na Wenye pesa Kama ufipa .

Atarudi tuuu
 
Nilikua na mdada na mdate kwa miaka kadhaa sasa,ila mwaka juzi Mamake akawa hanitaki kwa kuwa Mimi hohehahe sina kitu,lakini baada ya kuambiwa na watoto[jamaa tu] kuwa Mimi ndio natoka na mwanae.

Waliwahi kuwapeleka kwa Mama wanaume wenye mkwanja akawatolea nje,kipindi nasoma na yeye ni teacher mkoa fulani,mwakajana alipewa na bibi yake dawa ili aachane na Mimi ataitupa,mwakajana mwishoni Mamake bint akawa anaumwa,akamwambia mwanae mbona haolewi,wakati huo ndio nimemaliza college

Nikambembeleza yakaisha,siku moja Mamake binti akampigia simu mfanyibiashara mwenzake amkopeshe pesa,akaenda jamaa mpaka home kwa Mama mkwe wangu akatoa pesa akamkopesha Mama,jamaa akamwambia Mama mtoto yupo hapa,nipe mwanao nimuoe nitakupa zaidi ya hizo.

Jamaa alivyoondoka Mama akawa anamlaumu mwanae kwa kukomaa na hohehahe Mimi na kuwaacha watu wenye pesa,amenisaidia sana mdada mpaka nimemaliza college,mtoto aliridhika na Mimi ila Mama na ndugu hawanitaki kabisa,mwakajana Mamake alilia akiwa mgonjwa na akamwambia afe bila kuona wajukuu sio sawa,

TImbwili likawa kwangu bado kiuchumi sijakaa vizuri hata kidogo,from no where baby wangu akawa akirudi mjini haniambii,akawa anataka nguo zake eti ziko kwangu kitambo hazitumiki,nikawa naingia wasiwasi nikawa namuuliza kama nataka kunitema akawa anakataa,siku moja akaibuka home gafla nilikua na homa kidogo akaja kuchukua nguo zake nilikua na msela sebleni.

Nikaenda nae room nikamuuliza kama kunatatizo akasema hakuna amefuata nguo zake,nikalazimika kumpa shingo upande,simu nikipiga hapokei ontime au hapokei kabisa,texts hajibu au anareply late,akaweka status 'burning the past' sikusema kitu baada ya kuona nadharaulika nikaacha kupiga simu na kutuma texts pia,akaenda Instagram akaweka nyimbo ya christian Bella aliempenda kwa dhati eti amemkimbia.

Sejasema kitu mpaka sasa zaidi ya mwezi na ushekh hatuwasiliani kwa ufupi ,ingawa nilimuomba aniambie mapema kama amepata mtu mwingine,aaah ajabu Baba yangu anampenda sana huyu bint ingawa hajawah kumuona,alikua anampigia simu na kumsalimia na mzazi wangu hajawahi hata siku moja kuwa na mawasiliano na wapenzi wa watoto wake ila kwa huyu bint imekua tofauti

......nahisi sina changu tena.....

Wakuu nimekwama nafanyaje hapa au ungekua wewe ungefanya nini?

serious hii case niko nayo nilikua na malengo nae sana sana huyu mtu.
mkuu mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguka ila tatizo letu huwa tunatumia mda mwingi kuconcentrate kwenye mlango uliofungwa
 
Ndio mapenzi hayo mdogo wangu.. Punguza slope, unaweza kufa kwa presha
Sio slope mkuu kuna mambo mengi tu nimemshauri kufanya,kuna niliochangia kufanyanae na kama mtoto wa kiume nimemfanyia bila ya kujali ni kipato kiasi gani

Nili invest kama mke wangu mtarajiwa sio kama alikua ananipa pesa ,maisha yangu hayakua yanamtegemea yeye.
 
Kuachwa kunauma wewe asikwambie mtu, tena uachwe na mtu unaempenda. Kwasababu wewe kwako inakuwa news wakati yeye alishaplan.
Lakini ni lazima ukubaliane na moyo na akili yako ili uruhusu mambo mengine yaweze kusonga mbele maana mwenzako kashaamua kwa milango yake yote ya fahamu kuwa sasa basi.
 
mkuu mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguka ila tatizo letu huwa tunatumia mda mwingi kuconcentrate kwenye mlango uliofungwa
Mkuu mdada alikua ametulia tabia njema kabisa Mamake kwa % kubwa ndie amekua kikwazo hasa kwa imani yangu

Sina mtu ambae nilimuandaa kwa ajili ya kureplace
 
Lakini ni lazima ukubaliane na moyo na akili yako ili uruhusu mambo mengine yaweze kusonga mbele maana mwenzako kashaamua kwa milango yake yote ya fahamu kuwa sasa basi.
Ni mpaka iingie akilini mwako sasa una uikubali ndiyo utamove on. Nilipoachwa mimi ilikuwa wakati Will Smith amemwacha Tyra Banks, basi alikwenda kwenye Oprah Talk Show akawa anasimulia alivyodili na kuachwa kule, alibandika karatasi ukutani kila kona 'he was't good enough for me'. Basi kila akisoma ndiyo anajipa moyo kuwa hajapoteza kitu. Lakini shida alisema kila akitoka nje akikutana bill posters Will anafanya advertisement ilikuwa inarudi kichwani. Hii kitu haina mtoto wa mfalme wala celebrity, mapenzi ni mapenzi na kuachwa ni kuachwa tu.
 
Ukiamua kuutesa mwili wako kwa kufikiria hata jambo ambalo lipo nje kbs ya uwezo wako ni wewe tu na akili yako lakini ukiamua na wewe kuwa sasa basi itakuwa basi. Kuachwa na mtu unaemoenda na kufiwa na mzazi kipi kinauma?
 
Mimi niliumia nilimsubiri kama miaka mitano na mawasiliano mazuri tu, sijui kilibadilika nini, siku moja akaniambia mimi na yeye hatuna future tena nimwache aendelee na maisha yake. Ile siku ndiyo nilijua watu wakisema moyo unauma, physically niliyahisi maumivu ya moyo. Alifunga ndoa lakini baada ya miaka mitatu kwenye ndoa vilibuma huko, akaanza kunitafuta, mimi tena? No thank you.
Afadhali uliyemfumania unaweza kumsamehe lakini sio aliyekutamkia kuwa mimi na wewe basi
 
Pole sana, kwanza nakusifu kwa ujasiri wa kutokuendelea kujiumiza kwa kumpigia magoti na kumkumbusha mlipotoka. Usijutie wala usijilaumu kwa hali iliosababisha wewe kutokuanae, huwezi kujua Mungu amekuepushia nini, mwanaume kamili ni yule anaewaza kuachana na ampendae kwa busara pasi na kinyongo moyoni, yaani kiroho safi kbs hata mkikutana salam km kawaida. Nafasi, muda na kila ulichokuwa umekitenga akilini kwa ajili yake viwekeze ktk kutafuta maisha hakika utafanikiwa.
Asante mkuu
 
Mimi niliumia nilimsubiri kama miaka mitano na mawasiliano mazuri tu, sijui kilibadilika nini, siku moja akaniambia mimi na yeye hatuna future tena nimwache aendelee na maisha yake. Ile siku ndiyo nilijua watu wakisema moyo unauma, physically niliyahisi maumivu ya moyo. Alifunga ndoa lakini baada ya miaka mitatu kwenye ndoa vilibuma huko, akaanza kunitafuta, mimi tena? No thank you.
Pole sana, mimi sasahv ninachoamini ni kuwa kila jambo linatokea kwa kusudi kabisa.

Time is always the teller.
 
Pole sana mkuu hapo piga moyo konde tu jijenge kiuchumi kwaza focus katika Malengo yako maumivu siku zote ukizoea yanakuwa historia na funzo pia Amini utazoea tuu na utakuwa imara zaidi ya Hapo na usichoke kumuomba MUNGU akupe mwnamke atakaye kuja kuwa mkeo wa haja ya moyo wako sikuzote naamini mke bora anaandaliwa kwa uwezo wa MUNGU TU.
Na siyo kila mwanaume ana roho mbaya wengine wana copy tu kutokana na vitendo walivyokwisha fanyiwa na wapenzi wao waliopita au marafiki .
 
Itengeneze akili yako ndugu kuwa umeachwa na ukubali ukweli kwamba umeachwa na usijiwekee matumaini ya kurudi kwake kwako. Kama ni kuteseka we teseka ukiitumainia kesho yako itakuwa njema zaidi.
Niliachwa na mwanamke niliempenda kuliko nilivyokuwa nikijipenda mwenyewe mwaka wa 2012, tar 25 July. Aliponitamkia nilisikia ka nimepigwa shoti ya umeme ghafla nikalowa mwili mzima, binti huyu niliiweka akili yangu na moyo wangu kwake kwa kias kikubwa mno. Tena nakumbuka siku hiyo hom ndo tumemaliza kunywa uji usio na sukari, mara kidogo akanitext akanambia its over between us. Sikuwa na kazi ila nilijishughulisha na kazi ndogo ndogo na mimi ndo nilikuwa tumain lake kubwa chuon kiuchumi, by the tym alikuwa mwaka wa pili. Niliteseka mno na it took me 2 plain years inanitesa hali ile. Nilikubaliana nayo huku nikiamin ipo siku yataisha na nitakaa sawa. Usichoke ndugu, jipe matumain, usiache kumshirikisha Muumba, utatoka humo.
 
Kuna mawili unayoweza kufanya sasa yakakusaidia na ukamaliza tatizo kabisa:
1.Pata pesa ghafla umwoe ukiwa sio hohehahe ili kwa wakwe ukubalike.
2.Au msahau huyo binti na usijishughulishe nae tena wala kusikitika kumkosa.
 
Sawa Wakuu nimewaelewa na nitayafanyia kazi,kiukweli nimeumia sana
Kuna mawili unayoweza kufanya sasa yakakusaidia na ukamaliza tatizo kabisa:
1.Pata pesa ghafla umwoe ukiwa sio hohehahe ili kwa wakwe ukubalike.
2.Au msahau huyo binti na usijishughulishe nae tena wala kusikitika kumkosa.
 
Tafuta pesa wew utakosa vitu vitamu mzee. .. pesa ndo kila kitu
 
Sio siri mimi yupo ambaye nilimpenda sana na kumuwekea malengo kabisa akawa ananiacha acha bila sababu za msingi kumbe alikuwa ananicompare na mwingine especcially kwenye suala la kiuchumi, kwa kumpenda nikamwomba msamaha mimi japo kanikosea yeye.

Tukarudisha closeness kwa muda flani akaniacha tena...ikafikia mahali nikachoka na kugive up na sikuwahi kumcheat before.

From there nikaamua kuachana naye rasmi ingawa sasa anataka turudiane ila nimebaki na msimamo huohuo na itabaki hivyo.

Asilimia kubwa ya wanaowatenda wanaowapenda kwa dhati mwishowake they always wants to come back. Walijisemea wazungu "karma is a bit..ch" it is indeed. Mungu hutoa haki zake hapa hapa duniani no matter how long it takes or not meant to be, coz km humpendi mtu au unajua hutaishi nae, in 3 months tu tayari una jibu moyoni kuwa hapaaa nooo hapa yaasss! huyu jamaa yani nampa mwaka mmoja tu ataona karma ya demu na waliomchochea akakimbia.
 
Pole kwa kuachwa ndigu, jipange upya
 
Back
Top Bottom