Nahisi kama nimerogwa

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Jamani yaani mwenzenu mimi nahisi kama nimerogwa hivi.

Tangu nipate ajira nimekuwa mtu wa magonjwa tu yaani kila ikifika Jumamosi na Jumapili kunaibuka ugonjwa wa mpya.

Hali hii inanisumbua kidogo, na kila nikifika hospitali hata kabla sijaonana na daktari nahisi napona au ugonjwa unazidi saana.

Nilianza na ugonjwa wa mgongo, nikacheki wakaniambia ni maumivu tu mikapona.

Nikashikwa na ugonjwa wa shambulio la hofu, nikapona.

Nikashikwa na ugonjwa wa tumbo kujaa gesi na chakula kutokusagwa vizuri tumboni nikapona.

Nikashikwa na ugonjwa tena wa shambulio la hofu nimepona.

Sasa hivi nimeshikwa na ugonjwa wa kichwa nasikia maumivu kisogoni. Na kuna muda nahisi kichwa chepesi au kizitoa na ninasikia kizunguzungu sometime.

Sasa sijui magonjwa haya yananitakia nini mimi!
 
Nenda kwa Mwamposa mkuu ukajipatie uponyaji wako,au la hasha hudhuria kwa madaktari wa physcho kukucounsel urudi sawa
 
Ushirikina kama hujawahi kukukuta utaona kama watu wanatania hivi, Ila mkuu jitahidi ukafanye full body check up na ukapate ushauri wa tiba za kawaida. Ikishindakana hapo at least ndo utoe hitimisho kuwa kuna michezo ya kiswahili unafanyiwa
 
Simama katika maombi, angalia sehemu sahihi, ambapo wanamwabudu Mungu wa kweli, uwe na imani naamini yatakwisha
 
Simama katika maombi,angalia sehemu sahihi,ambapo wanamwabudu Mungu wa kweli
,uwe na imani naamini yatakwisha
wachawi utawajua tu, huwa wanapendekeza kumwomba Mungu, wakati nao wanapenda kujificha huko huko makanisani

Tafuta cure, Mungu aliumba vyote duniani tuvitumie pia akagawa na vipawa kwa wataalam mbali mbali pale tunapishindwa sisi tuwatumie. Amina
 
wachawi utawajua tu, huwa wanapendekeza kumwomba Mungu, wakati nao wanapenda kujificha huko huko makanisani
Tafuta cure, Mungu aliomba vyote duniani tuvitumie pia akagawa na vipawa kwa wataalam mbali mbali pale tunapishindwa sisi tuwatumie . Amina
Hii comment yako ina lenga nn mkuu, kwamba ushauri wangu ni mbaya na kunifananisha na mchawi au sijaelewa naomba nieleweshe.
 
Pole mkuu sasa hujasema ukifikaga hospitali vipimo vinasemaje!? Pia huo ugonjwa wa hofu ya shambulio vipi dalili zake ni zipi na huwa unaandikiwa dozi gani kuutibu? Yawezekana na wengine tukawa nao pasipo kujua!

nashauri kama ukiweza badili makazi, kuna mtu alikuwa mfanyakazi kama wewe wakati akiwa wilaya nyingine alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mgongo kuuma lakini toka alivohamia wilaya nyingine tatizo hili hakuwahi kuliskia tena!
 
Anxiety disorder
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom