Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Mar 3, 2023
16,797
51,966
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu. Kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa muda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi. Mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kuwa nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani.

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi.

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae. Hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia.

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi.
 
Mzazi ni mzazi tu hatakama na mchawi changudoa mlevi au kitu chochote.

wewe kama kijana wake inabidi umfuate na umueleze hali halisi inayokukumba ikiwa mmeshasuluhisha mgogoro uliotokea hapo awali.

tumia maarifa ya level ya elimu uliyopo kumaliza changamoto hiyo.
 
Wazazi nao wanazinguaga basi tu ndio vile washakua wakubwa kwetu so tunajitahidi kuishi humo kwenye nidhamu

Kama sababu za ugomvi wenu ni kupishana mitazamo mfano mama anataka uende kanisani wewe hutaki,hataki utembee usiku basi jitahidi kumsikiliza anayotaka yeye...muhimu hayana madhara kwako
 
Jitahidi kufunga mdomo wako, sio vizuri kugombana na mzazi najua umetambua kuwa ni tatizo, we unaweza kwenda nyumbani tu, Kama mzazi wako ni mtu mwenye gubu akiwa sebureni unaingia chumbani kwako, unajiepusha kukaakaa naye karibu.
 
Back
Top Bottom