Nahisi huyu mtoto ni wangu

Nahisi huyu mtoto ni wangu

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
12,534
Reaction score
27,800
Naomba mnisaidie katika hili.
Miaka 4 nyuma nilichaguliwa kujiunga na mafunzo fulani, moja ya masharti hayo yalikuwa kupima kundi la damu na magonjwa mengine.

Basi nikaamua kukamilisha mapema, nkaenda hospital kwa ajili ya kuchukua vipimo, muhudumu niliemkuta alikuwa mdada japo kwangu alikuwa mkubwa ila alikuwa kama na miaka 30 ivi.

Kanichukua vipimo vyote na akanambia nisubili majibu, nusu saa baadae kanipatia majibu huku ana furaha na kunipongeza sana mi sikufahamu kwa nini anafurahi ila katika kunipa majibu akaniomba namba yangu. nkampatia maana alinambia anataka nimfahamishe juu ya upatikanaji wa fomu nilizoenda kujaza.

Baada ya kama siku 3 tukawasilina, tukapanga sehemu ya kuonana na ikawa ivo. alicho nambia sasa kwamba siku ile alinipima HIV na kunikuta salama( ikumbukwe HIV haikuwa moja ya masharti ya medical examination) basi nami nkafurahi ila sikujua lengo lake baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya karibu, basi nikamjulisha juu ya safari yangu, akanambia ataomba ruhusa tuongozane. ila siku ya safari akapanga tar. yake tofauti na yangu sikujua sababu nami nkamkubalia nikajivuta vuta hadi tarehe iyo.

Tulikutana nje ya mkoa tukashinda na kulala pamoja siku 3 ila alisisitiza mchezo wa nyama kwa nyama kwa madai wote ni wazima (alisha wahi kupima na kunionesha) basi nami sikuwa na shaka.

Baada ya hapo tuliendelea kuwa na mawasiliano kama miezi 2 (ndani ya miezi hii alikuwa akinishukuru sana na kuntumia pesa akinambia nimemwokoa ila sikuwahi kujua ni nini ana maanisha ) mara yakakatika ghafla sikujua tatizo ni nini mi nkaendelea na mafunzo yangu.

Baada ya mafunzo yangu (miaka 3) nkarudi nyumbani nka bahatika kuonana tukawa na mawasiliano ila haikuwa ya karibu sana maana alikuwa akinambia mmewe ana wivu nami sikuwa na tatizo. ila mwezi jana kani SMS kama kuna uwezekeno wa kufanya safari kama ya siku ile sijamjibu,

Hili lina nipa mawazo maana niliwahi kaa kijiweni wakawa wanasema hazai (hapa alikuwa kwenye ndoa kwa miaka 3), sasa wanassema ana kizazi cha mbali ( miaka 4 tangu azae).

Nikimwomba nimwone mwanae hataki, ila kaniambia kama ntakubali kuwa na safari nae atanipa zawadi kubwa ila mimi nahisi huyu mwanae ni damu yangu, na hapa anataka mtoto wa pili. sina uhakika ila nahisi tu naomba mnisaidie niko sahihi au mawazo tu.
 
kubali io safari kwanza (safari moja huanzisha nyingine)....la sivyo hapa itakua tunabahatisha tu...
 
Heeh kumbe unazalisha mbegu Kali hivyo?? Siku hizi hata kumpata wa kukupa mimba ni kazi kubwa so wanawake wenye maisha yao ndo hutumia hyo trick
 
Mkuu unasema siku moja ulikaa ''kijiweni'' ukasikia wambea wanamteta huyo dada kwamba hazai? Sijui ana kizazi cha mbali? Sijui sijakuelewa vizuri pale juu? Ulisema umesikia kijiweni au kijijini kwao? Ha ha ha ha
 
Mkuu unasema siku moja ulikaa ''kijiweni'' ukasikia wambea wanamteta huyo dada kwamba hazai? Sijui ana kizazi cha mbali? Sijui sijakuelewa vizuri pale juu? Ulisema umesikia kijiweni au kijijini kwao? Ha ha ha ha

ilikuwa kijiweni before kupata mtoto alikuwa kaolewa 3 yrs ila hakuwa na mtoto wakadai ni tasa but after kupata mtoto (ukumbuke hapa nilikuwa mafunzoni ) hadi leo nimerudi mwaka wa 4 hana mtoto mwingine ndo wanadai ana kizazi cha mbali nae anakuja na program yake ya safari yetu kama mwanzo kwa ahadi nono, hili linanifanya niwaze anataka mimba japo sina uhakika mkuu
 
Mtafute mkae chini Muongee vizuri mtaelewana tu.
 
Back
Top Bottom