belie
JF-Expert Member
- Sep 19, 2014
- 387
- 261
Habari zenu jamani, mimi ni mgeni kidogo humu, sina muda sana. Nilikuwa napitia tu maongezi na comment za watu na nikavutiwa kujiunga, anyway turudi kwenye point ilionileta hapa.
Nlikua nina mpenzi wangu ambaye alikua workmate wa kaka yangu, akatokea kunipenda na mimi nikampenda tukaanza mahusiano hapo.
Kiukweli nilimpenda sana na nikahisi ndie atakaekuja kuwa mume wangu coz alikua na sifa zote nilizozihitaji. Tulianza mapenzi vizuri sana mpaka nikawa nahisi duniani tumebaki wawili tu mimi na yeye.
Lakini kuna siku alinipa mashaka kidogo. Ikumbukwe kuwa mimi bado nakaa kwetu na nilikua ndo nimemaliza chuo nasubiri majibu nianze na utaratibu wa kutafuta kazi. Kwa jinsi nilivyokuwa nampenda nililazimika kusema uongo nyumbani na kwenda kulala kwake, na hata siku nyingine kutoroka kabisa ili tu niwe na yeye.
Basi bwana, siku hiyo nilienda kwake nikalala huko, sasa asubuhi mapenzi yakazidi akasema haendi kazini anataka tushinde wote ilkuwa siku ya jumatatu. Baadae kama saa tatu akapigiwa simu aende ofisini, ikabidi aende, kufika akapewa barua ya kusimamishwa kazi akarudi akawa upset sana.
Basi nikajaribu kumpoza pale akatulia kidogo sasa baadae akawa ameweka simu kwenye chaji, na mimi nimeweka ya kwangu huku naitumia pale pale, ikawa simu yake ikiita ananiambia nimpe anapokea.
Ikapigwa simu ya mdada ikiwa imeseviwa na picha yake nikampa hakupokea, akaimute, akapiga tena kama mara 5 hivi nikwamwambia mbona hutaki kupokea akanijibu 'aah! msumbufu huyu' akapiga tena akapokea akamwambia nitakupigia badae.
Basi bwana, mimi nikaendelea na zangu, kwakuwa huwa sipendi kugusa simu ya mpenzi wangu nikamuacha na sikumuuliza.
Siku nyingine tukiwa tunaangalia TV mchana nikapitiwa usingizi kwenye kochi, nikalala, simu yangu niliiacha pembeni kidogo na yeye alikua karibu yangu, basi akachukua simu yangu na kuanza kusearch. Sasa kwa sababu simu yangu kila ukiitouch inatoa mlio fulani hivi, nikastuka lakini hakujua kama nipo macho coz nilikua nimegeukia upande mwingine, akaikagua sana siku hiyo na mimi nikamuacha coz nlikua najiamini.
Basi alivyomaliza baadae nikajifanya nimeamka, kushika simu yangu nakuta vitu viko shagalabagala, si unajua mtu chako bana, akitumia mwingine unajua tuu, nikamuuliza umeshika simu yangu akataa huku akiwa amebadilika usoni.
Baadae akaniuliza kuna watu nilikuwa nachat nao kama friends akajua ni mabwana zangu, nikamtoa wasi wasi na kuwapigia kabisa akaamini.
Sasa baada ya hapo nikahisi kuna kitu kinaendelea, kuna siku usiku tunataka kulala namba ile ile ilipopigwa siku ile mara nyingi ikapigwa tena, hakupokea. Nikaona anamtumia message asubuhi yake wakati yupo bafuni nikachukua simu yake na kuangalia nikakuta message zaa ajabu, nikaja kumuuliza akaniambia yule ni rafiki yake tu wamezoeana sana.
Niliumia sana coz huwa sipendi kudanganywa, yakapita hayo akaomba msamaha yakaisha.
Sasa visa vikawa haviishi mara nimpigie asipokee, mara aanze kunambia kama simtaki nimwambie kisa sijampigia wala kumtext wakat na yeye kakaa kimya, kuna kipindi tukaa siku 3 bila mawasiliano yoyote yale, nkaanza kuchoka sasa.
Lakini siku hyo ndo nilichoka zaidi, alikua amesafiri kwenda kwao kwa ajili ya arobaini ya babu yake, akarudi, akataka niende siku ambayo anarudi nikamwambia haiwezekani nitakuja kesho.
Basi kesho nikaenda nikakuta mafuta ya mwanamke hizi lotion za kujichubua na yametumika limebaki kama nusu kopo, nikamuuliza akaniambia ni ya mdogo wake wakati wanarudi akayasahau kwenye begi lake wakati huyo begi lipo sebuleni amelitupa na kuniambia hajalifungua amefika na kuliweka hapo na kulala, na mimi nilienda asubuhi mida ya saa 3 na wakati nafika ndo aliamka kunifungulia geti (shangaeni maajabu hayo) basi nikakaa kimya tu. Nikawa nafanya usafi wa kupanga nguo kabatini nikakuta nguo zimefichwa kwenye mfuko za kike, nikamuuliza za nani akasema za dada ake mmoja hivi aliziacha wakati anahama, nikamwambia mbona siku zote napanga nguo humu sijawahi kuziona na mimi huwa nikipanga nguo natoa kabati zima linakua tupu kabisaa naanza kuwekaa upyaaa.
Akakosa cha kunijibu ndipo nikachukua simu yake baadae kuangalia kwenye picha nakuta picha za utupu za mwanamke na zimetumwa jana yake, na mwanamke mwenyewe ndo yule wa awali aliyekua hapokei simu zake.
Kumuuliza ananiambia kuna rafiki yake alimtumia kitamboo akasema aangalie watoto wa chuo wanavyofanya uchafu wa kupiga picha za uchi, nikamuuliza una uhakika unachokisema ni kweli akajibu ndiooo, nikamuonyesha tarehe siku mwezi na saa iliyotumwa akawa anajing'ata hana cha kujibu mara akawa mkali anataka tugombane, mimi niIichukua vitu vyangu nikaondoka nyumbani nikamwambia 'its over' akajibu 'poaa maisha mema' tukaachana.
Ikumbukwe penzi hili halina hata miezi miwili, lakini imepita mwezi sasa hatuna mawasiliano, na nahisi bado nampenda, kuna siku nimemtumia message hakunijibu, lakini bado nampendaa nawishi arudi na kuadmit mistake zake.
Sijui nyie wenzangu mnaonaje.
Naombeni ushauri.
Nifanyaje