Nahisi alikuwa ni Malaika

MBITIYAZA

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
14,950
26,050
Wiki lilopita narud kutoka kwenye majukumu kama saa 11 jion hivi nakaribia nyumbani kwangu kabisa nikamuona mtu mmoja anaongea na dada wa kazi !basi nikashuka nikamsalimia ,alikua ni bibi wa kama miaka 60 ! alikua akitetemeka kama anaonyesha ana njaa au anaumwa sana !

Ukweli niliogopa kumkaribisha ndani maana ndo kwanza tumehamia hapa sijajua vzr majiran !nikaongea naye hapo nje !Bibi akaniambia anaumwa ametoka hosptali lakini amekosa nauli na anaumwa njaa sana !hili la njaa akawa analirudia kila mara ! dah na mie nilikua nimechoka sana akili na uchovu tu wa siku plus joto ! nikaongea naye walau nijue anaishi wapi lakini chakushangaza anaishi upande mwingine kabisa !ni kama bibi aje tegeta lakini aseme ametoka mwenge hospitali anaishi kiwalani huko !nikamuuliza mbn huku umekuja kwingine !akasema nilipewa lift nikasema wanishushe huku niombe msaada ! nikasema kama unahitaj msaada pia nenda na kwa majirani zangu kawaeleze akawa anasitasita akaenda wakat huo nami nampikia mchakula ale !alirud mikono mitupu akaniambia mwanangu KUTOA NI MOYO !Hapo ndo akili ikaja kwanini nisimsaidie anachotaka !

nilimpa chakula cha haraka haraka tu maana nilianza kuogopa anavyotetemeka ,baada ya muda nikamuuliza unaumwa nini akaniambia yeye ni HIV+ !niliumia kiukweli! akasema ameambukizwa na mwanaye alikua mgonjwa kwahyo yeye ndo alikua akimuuguza !na akasema ana watoto wengine ,mmoja ni trafiki lakini hawana msaada kwake! aliyekuwa msaada amejinyonga wiki 3 zilizopita ! na nikamuuliza mume je ? akanijibu HUYO NILISHAMSAHAU ! sikuelewa anamaanisha nini na nikaogopa kuendelea kumhoji ! bibi aliniambia amekuwa mgonjwa zaid baada ya huyu mwanaye kufariki hana msaada na mtu !lakini na mie nilijiongeza anioneshe vithibitisho kama yeye mwathirika na kweli alinionesha dawa alizoenda kufata na ile kadi yao !
nikampa pesa za siku mbili tatu na aliomba mayai ya kuku wa kienyej nikampa !

baada ya siku 1 kupita nikaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa mtoto mmoja wa ndugu yangu ! nikamchukua na dada wa kazi nikaenda naye hyo ilikua saa8 mchana !nikadrop mjini kufanya mahitaj hasa zawad za huyu mtoto (maana ni wajina wangu) nyuma ya kiti niliacha mkoba ndani una laptop na mazagazaga mengine ! basi kumbe nilipoenda dukan kununua zawad alikuja kijana akamwambia dada wa kazi kuwa nimemtuma ampe mkoba nimesahau pesa mle aupeleke dukan ! dada akampa !imefika jion turud zetu hom naangalia mkoba siuon later dada akaniambia si ulimtuma mtu auchukue akuletee? NILIKAA CHINI !

Tukarud usk hom nikiwa nimechanganyikiwa mnoo nalaani vibaya had najihis mkosi tupu !machoz hayakuwa yanatoka lakini moyoni nilikua nalia mbaya ! nikamweleza mume naye akashtuka akaniambia bas tena !
nilishindwa kula wala kulala ! saa 5 nilikua macho nataman nifanye nn sina la kufanya kitanda nakiona kichungu , 30min later mama mzaz akanipigia simu sikuipokea maana nilikua na jazba sana jins dada alivyokubali kirahis kudangnyika !akapiga kwa mume naye nikamwambia usipokee(maana lazima ningepewa niongee naye ) alipiga sana sana kwangu na kwa mume ! baadaye sana nikaamua kupokea maana alinisms kuna shida !

Aliniambia leo umepoteza nini ? nikamwambia laptop tena ina mambo muhimu mama !akasema nimepigiwa simu na mtu anasema ameokota laptop !
kufupisha stry mama alidhan wale ni majambaz !kwa hyo latop kulikua na modem yangu hivyo waliitoa line wakaanza kupigia watu kuniulizia maana kwa mkoba kulikua na pasport zangu !wote wakawa hawanifaham ! wakaja ona jina la MAMA!ndo mamangu kukiri ni mwanaye !jaman niliipata laptop yangu kesho yake ikiwa na kila kitu !(jinsi walipoipata hao watu napo ni kizungumkuti)
jaman leo nimewaza sana nadhan yule BIBI ALIKUA MALAIKA NA ALITUMWA NA MUNGU SIJUI? nimejifunza kutenda wema hata km ni kiduchu !jaman tutende mema kila iitwapo leo !
 
Inawezekana akawa ni malaika lakini pia inawezekana asiwe ni malaika ila umeunganisha tu matukio kwa kuvipata vifaa vyako vilivyopotea, katika hadithi nyingi za watu waliotokewa na malaika, inasemekana malaika hawakuwabembeleza kuwapa vitu kama we we wala hawakupata kuwa na maongezi marefu ya kumhoj malaika, ila tu ulitenda jambo jema kwa msaada na mungu akaamua kukutendea miujiza ya kuupata mzigo kwako kwani pia ulitolewa na beki tatu wako katika mazingira ya kutatanisha
 
Inawezekana akawa ni malaika lakini pia inawezekana asiwe ni malaika ila umeunganisha tu matukio kwa kuvipata vifaa vyako vilivyopotea, katika hadithi nyingi za watu waliotokewa na malaika, inasemekana malaika hawakuwabembeleza kuwapa vitu kama we we wala hawakupata kuwa na maongezi marefu ya kumhoj malaika, ila tu ulitenda jambo jema kwa msaada na mungu akaamua kukutendea miujiza ya kuupata mzigo kwako kwani pia ulitolewa na beki tatu wako katika mazingira ya kutatanisha


Huenda aisee !
 
Sijaona connection ya kupatikana kwa vitu vyako na wewe kumtendea wema bibi mpaka ukahisi ni malaika.Though it z a very interesting story.

Sina uhakika kama nimemuwahi Joseverest.
 
Aaisehh barikiwa mpendwa katika jina la bwana

japo stor mbili sijaona muunganiko wake mi nilifikiri huyo bibi ndio kakuokotea mahali laptop yako
 
sio kwa awamu hii!!umerudishiwa laptop???


thts why naunganisha dots na yule bibi unajua hatukuamini kbs ! maana ni ngumu sana !imagine maofisin watu wanaiba laptop sembuse kitaan mtu akurudishie jaman
 
Aaisehh barikiwa mpendwa katika jina la bwana

japo stor mbili sijaona muunganiko wake mi nilifikiri huyo bibi ndio kakuokotea mahali laptop yako


mie nauona aisee ! nauona mno tu maana bibi alivyokuwa katika ile hali dah !sijui !hajaniokotea ni tukio limefululiza siku hii na inayofuata! na majiran hawakumskiliza kbsaaa
 
thts why naunganisha dots na yule bibi unajua hatukuamini kbs ! maana ni ngumu sana !imagine maofisin watu wanaiba laptop sembuse kitaan mtu akurudishie jaman
anyways,ulichukua namba za simu za bibi?nirushie kama vip nmeibiwa godoro
 
True, kutenda wema kwa Binadamu mwezio hasa usiyemjua kabisa na anauhitaji wa kitu ulichonacho ni kuwekeza kwa MOLA, ndo maana hata maandiko yanasema siku ya mwisho wengine wataambiwa hawafahamiki na MUUMBA kwa kuwa hawakuwasaidia wagonjwa, masikini, wahitaji kwa kupenda ubinafsi#[LOVE-IS-MY-RELIGION]#
 
kwa hali ilivyo sasaivi ngumu sana kutokea kilichokutokea, wakati mwingine ni mungu tu mwenyewe amefanya yake hasa baada ya kusikia kilio chako.
 
Hongera kwa moyo wa kusaidia wahitaji, ni mtihani ulikua unapewa ijulikane ungefanyaje, na hiyo ina uhusiano kabisa na kupatikana kwa vitu vyako baada ya kumsaidia mama.
 
Back
Top Bottom