Nagombea Remote na Watoto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nagombea Remote na Watoto!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Oct 6, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Jamani hii kitu imekuwa inanisumbua kwa muda sasa ndani ya nyumba! Hivi karibuni nimefunga cable service kutoka kwenye kampuni moja hapa nnapoishi. Binafsi hawa jamaa wana channel nyingi za mpira, wanyama, cartoon, movies, yaani ni kama dstv kwa asilimia 100. Kwa bahati mbaya-kwangu- na nzuri kwa watoto, ni kwamba kuna channel moja ya movie za akina kanumba-namaanisha za kiswahili.

  Kivumbi ni kwamba karibu watoto wote wanapenda kuangalia kama sio movie za kiswahili basi ni katuni. Yaani muda mwingi wamekuwa wakifanya hivyo, na wanaponiona mimi nakuja, utaona kabisa ni kama wanakosa raha maana wanajua, hapa Baba anakuja kubadili channel na kuweka kama sio channel ya mpira, basi ni discovery world au geographic channe, au animal planet au geographic wild, cnn, sky news au bbc. Hali hii nimeiona kwa muda mrefu sasa mpaka nimefika mahali nimeona kama naingilia uhuru wa members wengine wa familia, kwa maana nahisi wanaanza kuniona mimi kama mbinafsi vile. Imefika mahali sasa nimeamua kutokaa sebuleni, najifungia chumbani na kufanya kazi nyingine huku nikijua kuwa kuna mambo ya maana nayakosa lakini ntafayaje sasa watoto wenyewe wana mind wakiona nahamisha program wanazozipenda.

  Kwa kuwa nimehisi huenda wanashindwa tu kusema, nami sijui nifanyeje maana kama kuna mpira au kuna issue ambayo ni 'educative' huwa najikuta nahamisha channel ili kuangalia hiyo progam bila kujali hiyo mipicha yao ya kina kanumba.

  Hebu wakuu naombeni ushauri wenu, nifanyeje au nyie mnatumia njia gani, ili watoto waone kuwa na wewe kama mzazi unajali interest zao? Nakwazika, sasa kukosa mpira, kisa katoto ka chekechea kamekomalia remote kuangalia katuni/movie za kina kanumba wakati mie nataka nione Arsenal inavyochabangwa na kina Drogba. Nishaurini wakuu njia nzuri ipi nitumie ili watoto wasione kuwa Dingi Mnoko!

  Nawasubiria!
   
 2. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,468
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  nunua TV weka chumbani angalia kwa raha zako na wao wanajinafasi sebuleni
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,437
  Likes Received: 22,352
  Trophy Points: 280
  ma great thinka wengine bwana? Yaana solution ipo, nayo ni kununua tv na kuweka chumbani kwako, lakini bado unakuja JF na kuomba ushauri, je utakasirika iwapo watu wakikushauri ununue simu ya mchina yenye tv ndani?
   
 4. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kWAKWELI UNAWABOA WATOTO WEWE UNADHANI BAR WAMEJENGEWA NANI? hUJUI UNDER 18 HAWARUHUSIWI BAR MEANING KWAMBA ABOVE 18 HATAKIWI KUGOMBANIA REMOTE. AF WEWE UNAANGALIAJE MPIRA PEKE YAKO? UNASHANGILIA NANANI? kUNA MUDA WA BABA KURUDI NYUMBANI FANYA MAREKEBISHO. vINGINEVYO UTAMBOA HATA MKEO MANAKE ATAKUMISS VIPI.
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Asante dada, nashukuru kwa hilo!
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hahahahaaaaa! Mtu aliyekulia mjini muda mwingi utamjua tu kwa matendo na kauli zake. Aisee ungejua nnavyopenda kukaa na watoto na familia usingesema hiyo ya bar mkuu. Hayo mambo anayaweza bujibuji, mdomo unakunywa na macho yanakula pia. Huwa najifunza mengi sana kutoka kwa watoto nnavyokaa nao muda mwingi
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hivi suluhu ya ugomvi ndani ya nyumba ni 'kuachana' tu? Don't be too mechanical. Gari ikipata pancha, kuna njia zaidi ya moja ili kuendelea na safari. Aidha unaziba pancha au unaweka tairi la akiba. Suluhu ya umasikini sio kuiba pekee.
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  mikela, kununua tv nyingine na kuhamia chumbani haina tofauti na kuhama nyumba kwa sababu tu ya kutofautiana kitu na mwenzio/wanao. kama baba kuna umuhimu wa kujua wanao wanaangalia nini, na wanafanya nini wawapo nyumbani. hii ina maana na baba pia ata-sacrifice kutoangalia mpira na boxing, na mama nae na movies zake pia ziwe rehani. pia ni muhimu kufundisha watoto kushare resources na watu waliopo nyumbani kwao. kuna watu ofisini ukisafiri nao humo garini atataka msikilize kwaya yake tu (anakuja na cd kabisaa), mle hoteli aliyoizoea na kulala anapotaka yeye! nadhani kunaanzia huku. wafundishe wanao kuwa tunaweza kuangalia cartoon, na national geographic wajifunze kitu pia. na ccn ili wajue world news. humo kwenye movie za kiswahili na ki-nijeria nisitie neno manake sioni watakachojifunza zaidi ya miondoko feki na english mbobu, ila inahitaji kuwashawishi pia!
  hata kama unanunua tv ya chumbani ni kwa ajili ya kuangalia news za alfajiri wakati unamuwinda mama nanilii kwa morning glory. sio kwa ajili ya kukimbia wanao na cartoon. ni mtizamo tu lakini...

   
 9. M

  Mundu JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Pole sana..kaka, naona watu wanakuzodoa bro! Ni tatizo kwa familia nyingi...solution sio kununua ma TV kumi kumi ili kila mmoja aridhike. Mana kuna house girl anataka kumuona kanumba, Kuna Mama mwenyewe nyumba anataka kuona Nigerian movie, kuna watoto wanataka kuona katuni, na baba nyumba anataka kuona Arsenal...sasa hapo si mtakuwa ma anti sosho hapo nyumbani kwenu?

  Nadhani kila kitu kina wakati wake...na kuwe na kuvumiliana katika familia!! Mwaweza kuwa na TV moja na kila mmoja akawa yupo accomodated na kujiona ni mwanafamilia anayejaliwa.

  Kila mmoja athamini anachopenda mwengine...Katoni ni programs zinazoendelea kwa masaa ishirini na nne, na vivyo hivyo movie n.k. mechi ya Arseno ni dakika Tisini tu!!

  Ni sula la mawasiliano tu katika nyumba ndipo kila mmoja anaweza kuridhika kuangalia channel ya mwenzake na kusaidiana katika kujenga interest ya kitu ambacho labda haukuwa na mapenzi nacho zamani.

  Na ushauri mwingine ni kuwa, watoto waongozwe zaidi na waelimishwe ili waelewe ni muda gani wanapaswa kuwa katika TV, muda gani kucheza na muda gani kufanya homework n.k. Vinginevyo watakaa kwenye screen 24/7 tusipokuwa makini. Jamaa wale huwa hawachoki bana...
   
 10. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  so baba tulia uangalie katuni. "toto party kitoto"
   
 11. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mkuu pole! Ila nimeshawahi kusikia kuwa unaweza kuunga TV nyingine chumbani kwa dikoda moja. Kama ni kweli fanya uwaone wataalam na ununue TV nyingine uwe unakula uhondo wa huduma zaidi ya moja ukiwa chumbani kwako. Sebuleni utakuwa unawapita kama nguzo ya daraja na hizo katuni zao na mitamthilia ya kina kanumba.
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Mimi ni miongoni mwa waadhiriwa wa tatizo hilo. Lakini tumepanga ratiba ya kuangalia vipindi kila mmoja kwa wakati wake kulingana na mapenzi yake. Watoto sio kila wakati wanakuwa kwenye TV, home work au kujisomea watafanya muda gani au wanapaswa kulala mapema ili kesho wasisinngie shule. Kuwachia wototo kukesha kwenye TV sio jambo zuri maana bado wanatakiwa kuandaa maisha yao ili nao waje wawe na uwezo wa kununua TV kama hiyo au zaidi mara watakupokuwa na maisha yao.

  Aidha, kitendo cha kutumia TV moja kwa utaratibu mzuri kukidhi matakwa ya familia nzima kinawajengea watoto tabia ya kuwajali watu wengine katika matumizi ya rasilimali kuliko kujifikiria wenyewe. Watakapokuwa wakubwa hawataeza kuwa Mafisadi wa kujilimbikizia mali kwa manufaa yao wenyewe bali watawafikiria watu wengine.
   
 13. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180

  Nashukuru mzee, maana majibu ya Nsabhi na mikela yalinifanya nijione kama kweli ni kilaza katika hili. Nawashukuru sana kwa majibu ya kujenga familia wakuu!
   
 14. s

  sawabho JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Mimi ni miongoni mwa waadhiriwa wa tatizo hilo. Lakini tumepanga ratiba ya kuangalia vipindi kila mmoja kwa wakati wake kulingana na mapenzi yake. Watoto sio kila wakati wanakuwa kwenye TV, home work au kujisomea watafanya muda gani au wanapaswa kulala mapema ili kesho wasisinngie shule. Kuwachia wototo kukesha kwenye TV sio jambo zuri maana bado wanatakiwa kuandaa maisha yao ili nao waje wawe na uwezo wa kununua TV kama hiyo au zaidi mara watakupokuwa na maisha yao.

  Aidha, kitendo cha kutumia TV moja kwa utaratibu mzuri kukidhi matakwa ya familia nzima kinawajengea watoto tabia ya kuwajali watu wengine katika matumizi ya rasilimali kuliko kujifikiria wenyewe. Watakapokuwa wakubwa hawataeza kuwa Mafisadi wa kujilimbikizia mali kwa manufaa yao wenyewe bali watawafikiria watu wengine.
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hahahahahaaaaaaaaa! thnx mkuu, yaani napata faraja kweli, maana mwanzoni kuna watu walini steam out kweli!
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Thanx wajemeni, nawashukru sana ktk hili
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hili wala siyo tatizo mbona...

  Wewe nunua tivii yenye feature ya Picture in picture. Ukiwa nayo ya hivyo wewe unaweza ukaangalia vipindi vyako huku na wao wakijinafasi na akina Pink Panther au Popeye the sailor man na wote mkawa mko kwenye sofa mkiangalia.
   
 18. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nakuunga mkono
  lakini kuna umuhimu wa kuwa na tv zaidi ya moja pia
  nakubaliana na wewe kuwa umuhimu wa kuangalia tv pamoja ni mkubwa sana

   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  a
  Hii itawafundisha watoto tabia ya ubinafsi na ufisadi. Watakapokuwa wakubwa watakuwa na tabia ya kujimbilikizia mali. Baba, Mama na watoto wanatoka kwenda kumsalimia shangazi lakini kila mmoja anatoka na gari lake.
   
 20. c

  charndams JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  vp, mtu wangu! unaiharibu nyumba yako mwenyewe. weka ratiba ya kuangali TV kwa wanao. sio kila saaa. wazingatie kwanza masomo. kwani ni muda gani huo mnagombania remote na watoto? nikidhani wanaporudi shuleni jioni homework kwanza, kufanya matayarisho yao binafsi kwa ajili ya kesho na mengine madogo madogo. utakuta ule muda wa TV ni wakati wa kula tu. tena marufuku mtoto kuangalia TV baada ya saa nne, awe ni wa sekondari au msingi, wote kitandani na kwa wale wakubwa Study room. na wewe ni muda gani huo unao nyumbani wa TV? mipira sio kila siku na wala hizo program unazo sema sio kila siku. ili kuwatia displine weka ratiba kama baba. unachekesha kweli
   
Loading...