Nafunga ndoa natawakali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafunga ndoa natawakali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sokomoko, Jul 15, 2011.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Salaamu zangu natuma, zifike kila mahali,
  Tunaziomba rehema, za Mungu zituwasili,
  Hapo siku ya Qiyaama, tuwe chini ya kivuli,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Naoa mke Muumini, nafunga ndoa natawakali,
  Mke aloshika dini, na kila siku kuswali,
  Hijaab ipo kichwani, afunikae wote mwili,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.


  Sijatafuta uzuri, au yule mwenye mali,
  Nimechagua tabia nzuri, alotulia akili,
  Aloleleka vizuri, kidini na kiasili,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Sikumtafuta kwa haraka, nijionyeshe kamili,
  Zinifikie baraka, za Mola wangu Jalali,
  Nitulie kwa hakika, tabia mbaya nibadili,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Fadhila zake ni nyingi, uliza kila pahali,
  Huo ndio ni msingi, wa maisha ya halali,
  Ni kinga kwa mambo mengi, kwa madhambi mbalimbali,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Kuoa ni utulivu, tumeshaona dalili,
  Huyaondoa maovu, na mambo huwa sahali,
  Hukufanya mtulivu, shida ikikukabili,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Wajibu wangu tatimiza, tutakapokuwa wawili,
  Tukikaa kuzungumza, na mambo kuyajadili,
  Tutajaribu kueleza, tuelezane ukweli,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Niwe msimamizi, kwa mali na kila hali,
  Ayaonyeshe mapenzi, maneno kama asali,
  Katika masimulizi, sitosema kwa ukali,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Mungu atupe watoto, hao ni rasilmali,
  Mke ni mama watoto, awe mwema na mkali,
  Awatazame watoto, wasikuwe kijahili,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Mke ni nguzo nyumbani, kama vile matofali,
  Na mume ndio rubani, huona yaliyo mbali,
  Kamba ya Mungu tuishike, ibada iwe awali,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.

  Mungu Watunze vigoli, pamoja na wanawali,
  Wawe kama wa awali, kama zama za Rasuli,
  Nimemaliza kauli, hapa nafunga kufuli,
  Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  We ni mkali mazee!
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,658
  Likes Received: 8,211
  Trophy Points: 280
  sokomoko we pongezi, uamuzi wa busara
  umeepuka uzinzi, kigori ukampura
  wa dini na siyo mwizi, mzuri tabia sura
  Tualike hata wali, nasi tuje sherekea!
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Du!Leo kazi ipo!
   
 5. s

  shalis JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe na wewe umeiona eeeh
   
 6. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Kila la kheri.
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pongezi nazipokea ewe wangu mshirika
  Uzinzi hauna maana na wengi wameathirika
  Harusini wakaribishwa muda utakapofika
  Wewe ndugu jamaa na marafiki kadhalika


  Mimi najaribu wapo malenga walofuzu
  Siwezi jifananisha najifananisha na kauzu
  Hao beti huzichezea huziona kama mzuzu
  Ipo siku nitafuweza umalenga kuufuzu


  Hana ukali ni dini kutimiza
  Ama weye hujui HIV yaumiza?
  Bora uoe utulie usijejiviza


  Amin nakuitikia ewe wangu sahib
  Dua yako iwe nisipate masahib
  Ndoa iwe tamu kushinda zabubu
  Tuwe wema na wenye kuabudu
   
 8. S

  Senior Bachelor Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza nikupe pongezi, bibi huyo kumpata
  Kwa wako huu utenzi, yaonyesha umekita
  Upunguze matembezi, kwani chema ushapata
  Ukishaifunga ndoa, zipuyo siache wazi!

  Sokomoko uziache, 'kishaingia ndoani
  Na ukware uuache, hata 'kiwa mkoani
  Bibie usimuache, hasa kama muumini
  Ukishaifunga ndoa, bibiye umuheshimu

  Watoto mkijaliwa, muwalee kwa imani
  Ununue na maziwa, shibe ilete amani
  Elimu kizawadiwa, wawe ka' Kofi Anani
  Ukishaifunga ndoa, majukumu sikimbie.

  Tena ninakuhusia, talaka usiipende
  Hata kama ni wosia, haichanui mtende
  Kwa zake hizo ghasia, wanao usiwatende
  Ukishaifunga ndoa, wa pembeni siwaone.

  Mwenzio bado mseja, sijafanya uamuzi
  Sasa naiona haja, nisomapo hu' utenzi
  Nitalipa na mkaja, kishafanya uamuzi
  Nami najipanga pia, kutafuta muamini.

   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shukrani zipokee ewe wangu sahib
  Nasiha zako nzuri tena za kishababi
  Insha'Allah tazingatia namuomba Yarabi
  Mungu atuhitimishe kama babu na bibi

  Sokomoko taziacha mapenzi kuongeza
  Mungu atujalie pacha familia kuongeza
  Nitainamisha macho wala sitakonyeza
  Nimeamua kuoa uhuni kuutokomeza

  Majukumu tayashika bila shaka na wasi
  Watoto nitawalisha hata kama si mkwasi
  Na elimu tawapatia iliyo bora kuliko sisi
  Namomba Rahman anipe pumzi na nafasi

  Nakuombea yalo mema usiku na mchana
  Zikuepuke fitina kwa watu wenye khiyana
  Akujaalie mke mwema kwa nia yako njema
  Akuepushe lawama binaadamu si wema

  Tafuta mke haraka ukijiona kamili
  Utulie kwa haraka tabia mbaya ubadili
  Ikufike baraka ya Mola wako Jalali
  Funga ndoa tawakali oa mke muumini.

  Usitafute uzuri, au yule mwenye mali,
  Chagua tabia nzuri, alotulia akili,
  Aloleleka vizuri, kidini na kiasili,
  Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
   
Loading...