Nafsi yangu moja imefungwa

Nafsi yangu moja imefungwa

Mkondo wa Nungwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2019
Posts
332
Reaction score
389
Wakuu heshima kwenu,

Sababu ya kusema nafsi yangu moja imefungwa ninatokana na historia ya mitihani na majaribio mengi ya maisha 44yrs ndani ya majaribio na mitihani.
Siku ya leo nimeamka nikajiuliza kwann nafsi zinatitesa hivi na maradhi,vifungo, majanga, na dhulma iliyonipata tangu nilipoletwa katika hii dunia. Nikasikia sauti inaniambia nimefungwa. Je wataalamu binadamu ana nafsi ngapi na ikifungwa inakuaje.?

Historia yangu fupi niliwahi kufanya biashara nikawa na wateja wengi lakin sikuwahi kuziona pesa kabisa na sikujua hata kuzihesabu wala kuweka akiba miaka 15 nilikua siruhusiki hata kwenda na pesa nyumbani kwangu wala kununua kitu kizuri.

Nilikwenda kwa mtu mtaalam akanipa dawa nikapata nafuuakayafungua nikapata nafuu kubwa nikajua kuhesabu pesa na kuweka akiba maisha hayo yalidumu kwa miaka 2 tu pesa ikaanza kusambaratika tena biashara zikasambaratika nyumba na gari mpaka familia ikasambaratika mke tuliachana na mimi na watoto tunaishi mbali mbali bila ya kuwaona miaka 3 saivi

Ndani ya miaka 6 na nusu nimehama nyumba 9. Nilipigana navita vya kiroho kwa kusikia sauti zinazonituma nifanye mambo wanayotaka wao mpaka nikapelekwa mental.

Chanzo cha kusikia sauti ilianza kuniambia "kwann unamfanyia dawa mke wako basi utakoma".sauti zimenitesa na kuniweka katika mateso ya uchizi navua nguo na kukimbia ovyo na kuchezea vitu ovyo nikitulia naweza kumuandikia mtu mesej bila ya kutegemea au kumwambia maneno bila ya kutaka. Sauti zilikua zinaniambia wao ni maadui wakubwa na wapo kwangu kwa mikataba. Napata hisia kama nashikishwa anga au kuifungua na kuifunga anga. Na mambo mengi sana

Nimepata nafuu saivi lakin maisha yangu bado hayaeleweki na nimekuwa kama bado niko kwenye kifungo siruhusiki kupata pesa wala safari yoyote ndugu kama wamenitenga sina ushauri na mtu yoyote siwezi kufanya tiba yoyote hata nikijaribu nawacha pesa sirudii tena kwenye tiba.

Nisaidieni kujielewa na hatma ya maisha yangu na zaidi lililonitisha hata mtoto wangu wa kiume ilimuingia iyo sauti kwenye roho akawa anaambiwa maneno. Na wa kike akaniambia baba ninavoona hatutegemei tena kuishi na sisi tena watoto wako. Mimi ni baba mwebye watoto 5 lakin katika sauti nilizowahi kuzisikia kila nikifanya mapenzi na alokua mke wangu ilikua naskia sauti inaniambia "mtoto" yaanni kuashiria kama mke atashika mimba.

Nakaribisha maswali ili kufafanua zaidi sina elimu wala kipaji cha kujieleza vizuri ahsanteni ila kujibu nitajitahidi.
 
kuna brother alinambia muda mwingine usimuelezee kila mtu shida zako maana kuna wengine wakikuangalia unavyoweweseka nazo wakilinganisha na za kwao, wanaona unaigiza tu na nimeamini

Pole sana mkuu lakini hiyo shida yako si ya kisaikolojia hadi iwakute wanao ni ya kiroho. Fuata njia za kiroho naamini utasaidika
 
Safi.
Sala za Usiku nzuri sana.. ukiachana na Hizi Sunna za baada au kabala ya Sala zile za siku..

Piga sala zako 5
Jiweke safi kutoka ktk Maasi ya kidunia.
Toa Sadaka sana.

Usiku ndio muda mzuri wa Kuongea na Allah.. mlilie shida yako bila kuchoka ukiambatanisha na Sala za Usiku.

Pia Usisahau kufunga sunna J3 na Alhamis kwa mfululizo..

Then ulete mrejesh
 
Mkuu,sijui nikuulize kama ukoo/familia kuna mtu mwenye magonjwa ya akili???sijuikwa nini nalazimika kuamini una mental health problem(schizophrenia),huu ugonjwa unakua unasikia na kuona vitu ambavyo havipo...watu wanapewa dawa na sauti zinaisha,,,,,,,,,,,,,,,,,,

mimi naomba kama kuna Psychologist ama behaviour therapist humu amsaidie ndugu yetu huyu, he is feeling guilty kaenda kwa waganga ni jambo analo feel guilty..lina play na kumla taratibu in his sub -conscious mind,sitashangaa kama anakunywa heavily to escape/distract himself
 
Mkuu,sijui nikuulize kama ukoo/familia kuna mtu mwenye magonjwa ya akili???sijuikwa nini nalazimika kuamini una mental health problem(schizophrenia),huu ugonjwa unakua unasikia na kuona vitu ambavyo havipo...watu wanapewa dawa na sauti zinaisha,,,,,,,,,,,,,,,,,,

mimi naomba kama kuna Psychologist ama behaviour therapist humu amsaidie ndugu yetu huyu, he is feeling guilty kaenda kwa waganga ni jambo analo feel guilty..lina play na kumla taratibu in his sub -conscious mind,sitashangaa kama anakunywa heavily to escape/distract himself

Hatuna historia ya ugonjwa wa akili na nilipofika mental niliulizwa unasikia sauti lakin majibu yangu nikajibu hapana. Kwakua nilipelekwa niko kwenye utilivu kidogo nikachomwa shindano inaonekana inapoteza kumbukumbu masaa24. Nilitumia dawa zao mara moja tu ubongo nilihisi unataka kutoka na nikatoa mate kwa sana. Mental nililazwa wiki mbili nilikua nikichanganyikiwa najitambua kabisa lakin nafanya mambo bila ya kuweza kujizuia. Niliwakuta wagonjwa wengine wengi lakini nimegundua pia kumbe wengi sio kama wanamatizo ya akili ni mitihani ambayo iko nje ya uwezo wao. Wale wagonjwa wote wanajitambua kabisa wanaoga wengine mgonjwa wa akili hutaweza kuoga wala kula wala kuvuuka barabara wala kuomba pesa. Akili ni ugonjwa mbaya sana ukikufika mental hakuna mgonjwa wa akili kwa niliwakuta mimi vijana kama 20.
 
Hatuna historia ya ugonjwa wa akili na nilipofika mental niliulizwa unasikia sauti lakin majibu yangu nikajibu hapana. Kwakua nilipelekwa niko kwenye utilivu kidogo nikachomwa shindano inaonekana inapoteza kumbukumbu masaa24. Nilitumia dawa zao mara moja tu ubongo nilihisi unataka kutoka na nikatoa mate kwa sana. Mental nililazwa wiki mbili nilikua nikichanganyikiwa najitambua kabisa lakin nafanya mambo bila ya kuweza kujizuia. Niliwakuta wagonjwa wengine wengi lakini nimegundua pia kumbe wengi sio kama wanamatizo ya akili ni mitihani ambayo iko nje ya uwezo wao. Wale wagonjwa wote wanajitambua kabisa wanaoga wengine mgonjwa wa akili hutaweza kuoga wala kula wala kuvuuka barabara wala kuomba pesa. Akili ni ugonjwa mbaya sana ukikufika mental hakuna mgonjwa wa akili kwa niliwakuta mimi vijana kama 20.

Mkuu mm si mtaalamu sana,ila unahitaji to forgive yourself and not be hard on yourself....

mambo machache nayoweza kukushauri ni kubadilisha life style yako...

moja, hakikisha unapata usingizi wa kutosha. ukilala vizuri hautaipa mind yako to wander/kusumbuliwa na mawazo sijui waganga wamefanya nini. Ukilala vizuri, utaamka fresh and energetic ready to face the day,namaanisha utakua na nguvu ya kufuatilia biashara zako. Kutolala vizuri vinakufanya unachoka asubuhi, not motivated kufanya lolote, which makes your condition worse. Kama una struggle kupata usingizi kuna vidonge vya kulala lakini vina side effects,ila inaweza kusaidia siku za mwanzo. Si uliona ulivyokua mental hospital ulivyochomwa sindano ya usingizi ulivyoamka ulisikia unafuu?? ndio ujue usingizi vinaweza kusaidia tatiz lako.

Mbili, acha pombe, pombe i understand you might want to escape/distract yourself ila hii ni kama unamkubatia adui, pombe inakufanya usiwe na clear mind,huipi akili yako kufikiri nini ufanye, biashara gani uifatilie plus pombe ni gharama,mifuko inatoboka, hata kile kidogo ulichonacho utakimalizia kwenye pombe,manake hutakunywa bia moja,unahitaji bia nyingi kukimbia unpleasant feelings. Mwishowe unasema una biashara ila hujui pesa inakoenda,ni huyu mdudu POMBE amekua kope,anakunyonya tu, break free kutoka kwa huyu shetani na utaona matokeo/pesa ya biashara yako.

Third,kama waliotangulia kukushauri, fanya sala na kutoa sadaka. Sasa hivi unaona Mungu anakuadhibu sababu haukua karibu nae na ulifanya maagano na shetani, cha kukushauri ni ufanye opposite , ask for forgiveness,sali na utoe zaka, ukiamini Mungu wetu ni wa forgiveness. Kisaikolojia ukifanya haya ya kumfurahisha Mungu, ukafanya iwe part ya routine,namaanisha ukifanya REINFORCEMENT of this postive behaviour,slowly you will start to forgive yourself...

All the best rafiki.....
 
Kama hili tatizo limetoka kwako na sasa lipo kwa mtoto wako means na wewe kuna sehemu umelirithi,chakufanya tafuta watumishi wa Mungu mtafute chimbuko la tatizo,pole sana


Kingsmann
 
Fika kanisa linaitwa UAMSHO WA WAKRISTO TANZANIA (UWATA). kuna makanisa hayashindwi mambo haya UWATA ni suluhisho lako. UWATA Sio kama pentecoste, fullgospel, au ufufuo na uzima, sijui maji ya upako no! Watafute mahali ulipo naamini wapo ukiwakosa nenda fb tafuta magroup yao omba msaada wa kuwapata kutokana na ulipo au karibu yako. Baada ya week chache utawaambia ndugu zako wote waje UWATA.
 
i think hapo kwenye biashara nashauri usome vitu kuhusu biashara na vitabu vya biashara na jinsi ya kutumia pesa.
pia soma vitabu kuhusu saikolojia.

kingine soma vitabu kila unapopata muda hayo matatizo yataisha.

soma vitabu as much as you can.
pia jaribu kutafuta hobby yako.
pia tafuta purpose ya maisha yako.

nenda kwa daktari wa wa maswala ya saikolojia.
 
Unaishi na maagano..na Ni mbaya Sana Kama mtoto wako nae anaelekea uko..muombe Mungu hayo maagano yakuachie na utoe sadaka itakayovunja hayo maagano kushambulia kizazi chako..sali kwa imani yako pasipo kuchoka hasa Sala za usiku ni nzuri Sana.
 
Back
Top Bottom