Nafsi ni kitu gani?

kichekoh

JF-Expert Member
Sep 19, 2015
1,376
1,479
Heshima kwenu wadau, nijuavyo mi ni kwamba binadamu ana mihimili mikuu mitatu. Kwanza ni roho, pili ni mwili na tatu ni nafsi.

ROHO nafahamu ni ile pumzi ya uzima kutoka kwa mungu mwenyezi, ambayo ipo connected na Mungu mwenyewe.

MWILI ni Physical appearance ya mtu ambayo inajumuisha milango yote ya fahamu. Kwa suala la NAFSI bado sijalipatia ufumbuzi.

Naomba mwenye elimu zaidi atujuze.
 
Huwa nina jiuliza maswali mengi sana juu ya hivi vitu sijui ndio vitu, au ndio nini "roho, akili, nafsi".

Hivi vitu tunaambiwa kinadharia kwamba kila mtu anavyo lakini ukimuuliza anaekwambia kwamba una hivyo vitu viko wapi kama kweli ninavyo, Atakuletea misamiati mingi kweli na inayochanganya lakini kukuthibitishia kiko wapi hawezi.

Ninaamini kila mmoja wetu anaamini kwamba makao ya Akili ni kichwani lakini ukimfanyia mtu upasuaji wa kichwa huwezi kuzi kuta akili bali utakuta ubongo!

Sasa ninaomba kwa mwenye jibu nini huwa kinatokea mpaka akili ziwe kichwani lakini zisiwe zinaonekana atusaidie jibu.

Msamiati waki nadharia kama huo tuna ukuta kwenye ... hiki kitu kiitwacho ,Roho, nachenyewe hiki kitu kiitwacho .Roho,tuna ambiwa kina ishi ndani , ya moyo, wa mtu lakini ajabu. Na chenyewe hakithibitishiki , hakuna mtu anae weza kuni letea ,roho yamtu kama amba vyo hakuna mtu , mwenye uwezo wa kuniletea Akili , zamtu. Kama , pia kuna mtu mwenye uwezo wakuni saidia jibu nita shukuru sana , nini huwa kina fanya hivyo vitu visi onekane ?? Nani nani alie vigundua .. kwamaana havionekani........nani kwanini kama hatu wezi ku ziona Akili ni kwanini tusi amini , huwa tuna tumia ubongo kufikiri na wala sio akili zisizo onekana.

Misamiati kama hiyo hapo juu tuna kutana nayo tena kwenye kitu kiitwacho , nafsi hiki ndicho sijui hata kinadhaniwa kuishi wapi.

Ninawakaribisha wote ili tujiulize kwa pamoja kama vipo au havipo , tusije tukawa tunaamini vitu ambavyo ni nadharia tu na wala havipo.
 
Akili ni ule ufahamu wa kuweza kupembua zuri na baya, jema na ovu. na kuna milango mikuu 5 ya fahamu, ambayo akili inaweza kutumia katika utendaji wake. kwa mfano kwa kutumia mlango wa fahamu wa ulimi, akili inaweza kutofautisha maelfu ya ladha. ulimi ni kama kiwakilishi tu, coz kama ukiwa umezimia kwa mfano, hata ukipewa kitu uonje hutoweza kupata ladha, why?? kwa sababu ufahamu wako(akili) haifanyi kaz kwa wakati huo. kwa akili ndo fahamu yenyewe inayokuongoza kufanya shughuli. na ulimi, sikio, ngozi, macho na pua hi ni milango ambayo akili inatumia katika utendaji wake. ntaendelea upande wa roho.
 
Roho ni ile pumzi tunayopuliziwa na mungu mwenyewe. na hii roho ndo kiunganish pekee kati yetu na mungu. siku hizo pumzi zitakapokata na ndo mwisho wa uhai wako hapa duniani.
 
Asante sana nime kuelewa vizuri sana.
 
Roho ni ile pumzi tunayopuliziwa na mungu mwenyewe. na hii roho ndo kiunganish pekee kati yetu na mungu. siku hizo pumzi zitakapokata na ndo mwisho wa uhai wako hapa duniani.
Asante sana ila katika hili ninaomba ku uliza , ina kuwaje katika vitabu vyadini tuna ambiwa kwamba roho ndio zitakazo hukumiwa au muda mwingine tuna ambiwa shetani niroho...kama huto jali kuni jibu kama ulivyo nijibu nita endelea kushukurusana.
 
kwa faida yako, kuna aina mbili za ufahamu. 'conscious mind' na 'sub conscious mind'. conscious mind ni aina ya ufaham ambao nimeuzungumzia hapo juu. ni ule unatumia milango ya fahamu. ufahamu unadili na mambo ya hiari tu, kama vile kusikiliza, kula na mambo yote unayojiongoza katika kuyafanya. conscious mind ipo kwa ajili ya kuchambua kila tendo ulifanyalo. tukija kwenye sub conscious huu ni aina ya ufahamu hujiongoza wenyewe. hu deal na matendo yasiyo hiari, mfano unapolala conscious mind inakua haifanyi kaz. lakin kinachofanya mapigo ya moyo yaendelee kupiga, msukumo wa damu na kupumua ni sub conscious. i hope nimechangia.
 
Back
Top Bottom