Nafikiria kumuacha. Je niko sahihi?

Nafikiria kumuacha. Je niko sahihi?

Kumbe bado uko dilemma! Si ajabu wewe pia una mapungufu yako. Nakuona kama mtu fulani conservative hivi. Jitazame na wewe pia
Hakuna aliyekamilika chini ya jua Ndugu

Ila kuna mambo ya msingi huwa tunatazama tunapotafuta wenza wetu wa Maisha
 
Bado niko 50/50

Kuna muda nawaza kumuacha na nikapata mtu mwenye sifa ninazozipenda

Kuna muda naona yeyote nitakayekutana nae kwa sasa atanipenda kutokana na mali nilizonazo na sio utu na atanifanya nijute kumuacha huyu
Kadhalika sio lazima kuoa
 
Hakuna aliyekamilika chini ya jua Ndugu

Ila kuna mambo ya msingi huwa tunatazama tunapotafuta wenza wetu wa Maisha
Hilo hutakiwi kunifundisha mdogo wangu maana nimekuzidi kila kitu. Ninafahamu hayo yote. Kama unajua hakuna aliyekamilika kwanini unaomba ushauri?
 
Ni kwambie kitu kimoja tu kumbadilisha tabia mtu mzima ni ngumu na ukifanikiwa basi ni baadhi ya vitu kama sio kimoja basi viwili,
Kwa swala lako yaani nyie ni( incompatible)you have different ideologies. siwezi nikamjudge sana kwa sababu wewe unachokiona kibaya yeye ndo kinampa furaha maana yake unapotaka abadilike basi unapoteza furaha yake
Mfano umekuta mtu anakunywa pombe unataka aache,kama kwake ni kiburudisho usimfosi,unataka asokunywa pombe mtafte asokunywa sio umtafte anayekunywa utake kumbadilisha nikuharibiana starehe, anapenda western culture wewe hupend vyema mtafte asopenda
Ushauri
Tafta mtu mwenye misimamo inayokaribiana na yako,mnaeza msiendane kila sekta lakin mkawa mnakaribiana(no one is perfect) kiufupi kesi yako sio kubwa kuamua maana iko wazi sema kinachohitajika ni maamuzi ya kiume
 
Habari zenu wana jukwaa

Poleni na majukumu na pilika pilika za wiki nzima

Nina swala moja linalonisumbua sana kichwa kwa sasa, na nimekuja kwenu kuomba ushauri wa jambo hili.

Mimi ni mwanaume, nina miaka 28 kwa sasa. Nimekuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu kidogo wa takribani miaka nane na mpenzi wangu lakini naona mahusiano yenu yanafikia ukingoni.

Namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata malezi ya wazazi wote wawili, lakini mwenzangu hajabahatika kupata malezi ya baba, namaanisha mpaka leo amebahatika kulelewa na Mama tu ingawa Baba yake yu mzima mpaka leo na kwa sababu ya kulelewa na Mama tu naona amelishwa sumu ya kumchukia mzazi wake wa kiume.

Mpenzi wangu huyu kwa sasa yupo chuo, ila mimi nipo mtaani nna ajira ambayo ukweli ni kwamba ndo chanzo changu cha kipato kinachonifanya niendelee kuishi hapa Dar Es Salaam.

Toka tumeanza mahusiano, nilikua natamani sana nipate wasaa wa kuishi nae kwa muda kidogo kabla sijamuoa ili nipate kumfahamu mwenza wangu kiundani na Alhamdullilah nilipata wasaa wa kuishi nae mwaka jana kwa takribani miezi mitano nyumbani kwangu na nikapata kumfahamu kiundani kidogo.

Ukweli ni kwamba, Wazazi wangu ni watu waliokulia vijijini kabla ya kuja mjini ukubwani kutafuta Maisha na hivyo. Wamenilea katika maadili mazuri ya kiafrika katika nyanja zote za Maisha na namshukuru Mungu kwa malezi yao.

Mwenzangu, Mama yake ni Mcha Mungu sana ila yeye yupo tofauti kidogo na tabia za Mama yake. Akiwa mazingira ya kwao, Mama ndo huwa anamhimiza kwenda Kanisani lakini anapoondoka mazingira ya Nyumbani huwa anaacha kabisa kwenda huko Ibadani na kama akienda ni Mara mojamoja tu. Mwenzangu huyu amekumbatia sana mila za Magharibi kama kuvaa sana suruali za kubana mpaka anakosa nguo za kwenda kanisani, wallpapers zake kwenye simu ni picha za nusu utupu kwa sana, akikaa kwa TV vipindi anavyoangaliaga ni dhahama tupu (Keeping up with Kardashians) mpaka unajiuliza anajifunza nini huku, Hapendi kabisa kusikia mazingira ya vijijini na ukitaka mkosane mwambie unapenda kuishi huko, atakwambia we kaishi huko mm siwezi kama Kuwasiliana WhatsApp ipo. Duuh! Hivi huyu anafaa kuwa mke kweli na anaweza kuishi nadhiri ya kuishi pamoja katika shida na Raha?

Ana hulka ya uvivu, kila kazi atataka mfanye wote akiamini haki sawa ni kazi zote za nyumbani mfanye wote, Ni mtu anayependa sana mikorogo ambayo kimsingi inapoteza rangi yake nzuri nyeusi ya asili, Nimeshajaribu kumkanya sana kuhusu hili na hata kutupa baadhi ya vipodozi vyake bila mafanikio, Marafiki zake wanaomzunguka ni walevi, wadangaji na mabinti wenye tabia chafu nyingi tuu, Na hili pia nimejaribu sana kumkanya ila huishia kusema wale ni marafiki tu na yeye ni mtu mzima anayejua nini anafanya hivyo hawawezi kumbadili tabia kwa namna yoyote ile.

Anapenda sana kula vyakula vya kisasa kama Chipsi na Ice Cream na sio vyakula vya kiafrika. Ugali hapendi kula na akila ugali ni lazima anywe na maziwa mgando la sivyo hataki kusikia ugali. Uvivu wake unanifanyaga nimuulize, " Hivi mama kwa uvivu wako huu, utaweza kuingia Leba, kujifungua kwa njia ya kawaida na kutoka salama kweli", kuamka mapema kwake ni ndoto, kwenye mazingira yake ya chuo huko hata nguo zake binafsi anafuliwa, Sasa huyu ni mke au Slay Queen?


Nimeahidi kumuoa akimaliza chuo, ila kila nikiwaza tabia zake naona hafit kuwa mke na Mama Bora wa familia na kwa maana hiyo nafikiria kumuacha na kuanzisha mahusiano mengine. Je niko sahihi kwenye hilii?
Naombeni ushauri wenu katika hili tafadhali

Achana na hiyo takataka utanishukuru baadae.
 
Bado niko 50/50

Kuna muda nawaza kumuacha na nikapata mtu mwenye sifa ninazozipenda

Kuna muda naona yeyote nitakayekutana nae kwa sasa atanipenda kutokana na mali nilizonazo na sio utu na atanifanya nijute kumuacha huyu
Kuanza mwanzo ni gharama, kama yuko na 25 years she is young mpe muda subiri amalize chuo then ndo uthaminishe vizuri
 
Sijaona tatizo hapo, malalamiko yako hayana msingi
 
Back
Top Bottom