gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
Licha ya mazuri mengi yanayofanywa na Serikali yetu ya awamu ya tano lakini yapo mambo lazima Raisi wetu mpendwa anahitaji apate taarifa vizuri kupitia vyanzo vyake vinginevyo hawa wanaoitwa wanyonge watakuwa wananyongwa.
Hivi wananchi wakaidi kusajili namba za simu ili iweje? Nani yuko tayari simu yake ifungwe kwa sababu yakutosajili line ya simu? Kwanini wananchi hawahawa ambao leo wanaonekana wakaidi hapo awali waliitikia vizuri usajili wa line zao wakati wakutumia kitambulisho cha mpiga kura?
Wapeni wananchi namba za NIDA ndipo muwafungie waliokaidi kujisajili.Namba za NIDA hamtoi ili watu wajisajili halafu mnawapa muda wananchi mliowanyima namba za NIDA wasipojisajili mnawafungia line zao,hivi mnasubiri mpaka muambiwe kwamba mnachowafanyia wananchi mnawaonea?
NIDA wamesababisha usumbufu mkubwa sana kwenye utoaji wa vitambulisho.
Ni vema serikali ikatambua kwamba wananchi waliitikia wito kwenye uandikishaji wa vitambulisho vya uraia mwanzoni kabisa wakati zoezi hili lilipoasisiwa lakini vitambulisho vya waliowengi NIDA hawajawaletea,wapo wananchi waliorudia zoezi hili zaidi ya mara mbili pasipo mafanikio yoyote.
Hivi kwa haya nani ni mzembe?
Zoezi hili limesababisha watanzania wanadamka alfajiri saa nane kuwahi foleni za namba za NIDA na baada ya zoezi wanafuatilia hizi namba kwenye ofisi za vijiji wengine wanafanikiwa na wengine wanafeli.Hivi bado huyu raia aliyehangaika alfajiri anafungiwa line yake?
Wapo wananchi wengi ambao wamefuatilia namba za NIDA lakini wamepewa namba ambazo sio zao.
Serikali itambue kwamba kutokana na uzembe wa NIDA wananchi wengi wanasajiliwa namba zao za simu kwa msaada wa ndugu na jamaa zao jambo ambalo linapoteza maana halisi ya zoezi hili kwani kinachofuata ni watu kutumia line ambazo si zao.
Tunamuomba Mh Raisi afuatilie tena mwenendo wa zoezi hili kwani limegeuka adhabu kwa watanzania kwa uzembe wa NIDA.
Watanzania waadhibiwe kwa uzembe wao lakini kuadhibiwa kwa uzembe wa NIDA sio sawa.