Nafasi za masomo katika chuo cha maji

Chuo cha Maji

Member
May 4, 2017
54
34
Habari wana jukwaa.
Chuo cha Maji kinapenda kutangaza nafasi za masomo katika ngazi ya certificate na diploma kwa mwaka wa masomo 2017/18.

Courses zitolewazo katika chuo hiki ni:
  1. Water Supply and Sanitation Engineering
  2. Irrigation Engineering
  3. Water Quality and Laboratory Technology
  4. Hydrogeology and Water Wells Drilling na
  5. Hydrology and Meteorology.
Course zote tajwa hapo juu ni za Miaka Mitatu kwa ngazi ya Diploma.

Jinsi ya ku-apply:
Kutokana na tamko la NACTE la tarehe 10 May 2017, maombi yote yanatakiwa yafanyike moja kwa moja katika chuo husika. Hivyo, form za kujiunga zinapatikana katika website ya chuo: http://www.waterinstitute.ac.tz/upl...ation Form for Ordinary Diploma 2017-2018.pdf

Masomo yataanza Tarehe 30 October 2017.

Mkopo kutoka Chuo cha Maji

Chuo cha Maji pia kwa kushirikiana na The Registered Trustees of Water Technician Fund na wadau wengine mbalimbali, kinatoa Mikopo pia kwa wanafunzi wapya na wanaoanza masomo katika ngazi ya Diploma na Certificate. Mikopo inaweza kua moja kati ya Ada ya mwaka, Pesa ya kujikimu (Chakula) au Maradhi.
Form za kuapply mikopo zilianza kutolewa kuanzia tarehe 24 Aprili 2017 na mwisho wa kupokea fomu ni tarehe 30 Agosti 2017 saa 10:00 Jioni (kumi kamili).
Wanawake/wasichana wanahimizwa sana ku-apply.

Form ya Mkopo unaweza download hapa: http://www.waterinstitute.ac.tz/uploads/documents/en/1493032205-WTF FOMU YA MIKOPO 2017.pdf

Huduma za Hostel

Chuo kinatoa huduma za malazi kwa baadhi ya wanafunzi kwa kufuata vigezo vya umbali kutoka nyumbani, jinsia, na disabilities. Wanafunzi ambao wana ndugu Dar es Salaam au wanaweza kupanga nyumba jirani na chuo wanahimizwa kukaa nyumbani au kupanga nje ya maeneo ya Chuo.

Form unaweza kuzituma kwa njia ya Posta au ukazileta moja kwa moja chuoni.
Chuo kipo Dar es Salaam, Ubungo, barabara ya kwenda Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Pia unaweza ku-download form zote Tatu hapa katika hii post.

Asanteni na karibuni Sana.
 
Attachments

  • fomu_ya_mikopo2017 (1).docx
    101.8 KB · Views: 738
  • WATER INSTITUTE APPLICATION FORM 2017-18.pdf
    106 KB · Views: 1,048
  • INVITATION OF APPLICATIONS DIPLOMA PROGRAMS 2017-2018.pdf
    48.9 KB · Views: 587
Watu wa arts wanaweza soma course gani apo chuo

Kujiunga na Chuo, tunatumia matokeo ya kidato cha 4, sio ya Advance.
Mwanafunzi awe amesoma masomo ya Science, Physics, Biology, Chemistry, Mathematics na Geography. Pia, uwe na ufahuru wa C moja na D mbili katika hayo masomo, bila kua na F ya Mathematics.

Kwa kanuni za NACTE, mwanafunzi ili uwe na D nne katika matokeo yako ya kidato cha nne ili uingie Chuo chochote kwa ngazi ya Certificate na Diploma.
 
kijana wangu ana hizo sifa je , ada ni kiasi gani kwa mwaka.....????

Kwa Mwaka, Ada ni Tsh 1,070,000 pamoja na Michango yote kasoro Accommodation fees. Unaweza kulipa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza Tsh 610,000 na ya pili Tsh 460,000.
Mwanafunzi asie na Bima ya Afya, atachangia Tsh 50400 kwaajili ya kukatiwa BIMA kama vyuo vingine vyote vinavyofanya Tanzania.
 
Kuna dogo wangu kasoma it certificate je anaweza endelea na diploma hapo chuon kwenu
 
Kuna dogo wangu kasoma it certificate je anaweza endelea na diploma hapo chuon kwenu

Alisomea course gani? Mbali na C D D za kidato cha Nne, pia tunampokea mwanafunzi mwenye D mbili na cheti cha NVA 3 au certificates za baadhi ya course kama Plumbing and Pipe Fitting na nyinginezo.

Naomba nitajie matokeo yake ya Kidato cha nne kwa masomo ya Physics, chemistry, Biology, Mathematics na geography inbox kwa maelezo zaidi.
 
Ivi Sinasikia Diploma mwaka huu wanakopeshwa na serikali?

Kwa Chuo cha Maji, mikopo inatolewa na Water Trustee Fund. Wanafunzi wanaopewa hela ya kula ni walioletwa na Serikali.

Hawa ni wale ambao wakati wapo kidato cha nne, walichagua kwenda Vyuo vya Ufundi badala ya Form 5. Wanafunzi hawa wanapewa hela ya kula (Kwa siku Tsh 6,000) kila mwezi, wanapewa maradhi bure na Chuo, na Hela ya field.
 
Duh!Hongera kwao,sisi wengine hata kama tuna nia ya kusoma tutaishia getini tu,pesa ngumu!Dah,huu ni mwaka wa 4 sasa nazunguka na Division II yangu.Tanzania balaa tupu :( :(
 
Alisomea course gani? Mbali na C D D za kidato cha Nne, pia tunampokea mwanafunzi mwenye D mbili na cheti cha NVA 3 au certificates za baadhi ya course kama Plumbing and Pipe Fitting na nyinginezo.

Naomba nitajie matokeo yake ya Kidato cha nne kwa masomo ya Physics, chemistry, Biology, Mathematics na geography inbox kwa maelezo zaidi.
Alisomea IT (information technology)Na o -level alichukua mchepuo wa arts
 
Kujiunga na Chuo, tunatumia matokeo ya kidato cha 4, sio ya Advance.
Mwanafunzi awe amesoma masomo ya Science, Physics, Biology, Chemistry, Mathematics na Geography. Pia, uwe na ufahuru wa C moja na D mbili katika hayo masomo, bila kua na F ya Mathematics.

Kwa kanuni za NACTE, mwanafunzi ili uwe na D nne katika matokeo yako ya kidato cha nne ili uingie Chuo chochote kwa ngazi ya Certificate na Diploma.
Je ukiwa na F ya phyz unaweza kujiunga Mimi nimepata ivi kwa masomo ulyosema apo
Math C
Bios C
Geo C
Chem D
Phyz F
Je,naweza kujiunga direct
 
Back
Top Bottom