Nafasi za Masomo China

Nafasi za Masomo China

Ngida1

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2009
Posts
586
Reaction score
206
Kuna fursa ya kujiendeleza kimasomo Nchini China, ambapo muombaji anaomba moja kwa moja kupitia mtandao. Zipo fursa katika vyuo mbalimbali, fursa ambazo maelezo yake yajitosheleza ni kwa Chuo cha Beijing Insitute of Technology(BiT) naUniversity of International Business and Economics(UIBE).

Lugha ya kufundishia:
Kiingereza(English) ndio lugha ambayo wanatumia kufundishia, isipokuwa ukihitaji kusoma kwa kichina pia hiyo fursa ipo.

Beijing Insitute of Technology(BiT)
Master's Degree Programs in English:
▪Electronics and communication Engineering
▪MBA
▪Mechanical Engineering
▪Automatic Control
▪Software

Doctoral Degree Programs in English
▪Wasiliana na chuo - University of International Business and Economics(UIBE)

Master's Degree Programs in English:

▪Accounting
▪Applied Economics
▪Finance
▪International Business
▪Logistic Management
▪Law
▪Finance(Actuarial Science and Risk Management)
▪International Relations
▪IMBA"

Doctoral Degree Programs in English;

▪International Economics
▪Finance
▪Industrial Economics
▪Business Management
▪Law

Udhamini(Scholarship) unajumuisha:

▪Application, tuition, basic learning materials, experiment and internship
▪Accommodation (on campus or off-campus student dorms)
▪One-time settlement subsidy: CNY 1,500(USD 245 or Euro 185)
▪Comprehensive Medical Insurance
▪Monthly Living allowance:
▪Master's: CNY 1,700(USD 275, or Euro 210)
▪Doctorate: CNY 2,000(USD 325, or Euro 245)
Muda wa Masomo
▪Muda wa masomo Master Degree ni kipindi cha miaka 2-3
▪Doctoral Degree ni kipindi cha miaka 3-5.

⚠Vigezo vya kuomba:

▪Uwe raia wa nchi yeyote lakini sio china
▪Shahada ya kwanza uweumeipata nje ya china
▪Kigezo cha Umri usiwe Umezidi Miaka 35 kwa Masters na Doctorate Miaka 40

⚠Kusoma Lugha:

▪Endapo katika kujaza fomu utachagua unahitaji mafunzo ya lugha kabla ya "Major courses", basi utapata mafunzo ya lugha mwaka mmoja kabla ya kuanza major courses zako. Usipochagua utaanza moja moja "major courses" zako huku ukisoma lugha ya kichina kwa ‘semester' moja/mbili tu. Unafundishwa lugha yao ili uweze kuwasiliana, lugha kuu ya mawasiliano ni kichina.

⚠Jinsi ya kuomba:

▪Jisajili katika mtandao wa scholarship za china ambao nihttp://laihua.csc.edu.cn . Chagua Chinese Government Scholarship kwa aina ya scholarship unayoomba. Wakati wa kujaza ikihitajika Agency Number ya chuo tumia zifuatazo.
▪Beijing Institute of Technology ni 10007
▪University of International Business and Economic(UIBE) ni 10036

Ukimaliza hatua zote mpaka mwisho, pakua(download) na ‘print' hiyo fomu ya maombi. Bandika picha yako katika fomu na jaza taarifa za ziada ambazo hukuzijaza mfano sahihi(signature).

▪Baada ya hapo ‘scan' nyaraka zifuatazo Fomu ya Maombi, Advanced Diploma au Degree Certificate, Official copy of Transcript, Study/Research plan(if you have), Photocopy of Passport (including the valid visa page if you are already in China), Recommendation letters from two professors or Lecturers vilevile usisahau kuandaa CV ambayo pia utaituma.

▪Baada ya hapo tuma hizo document ulizo'scan' kwa email ukijulisha ni maombi ya kusoma masters:
▪Beijing Institute of Technology: lq8120@bit.edu.cn copy to master_phd@bit.edu.cn
▪University of International Business and Economics(UIBE):sie@uibe.edu.cn

▪Kwa chuo cha UIBE muombaji itabidi aingie katika tovuti yao University of International Business and Economics kisha kiungo cha Internatioal Student kisha apply online. Hapo ajisajili kwa kutengeneza akaunti kisha kujaza taarifa zake kupitia akaunti hiyo.

⚠⚠Msimu wa Maombi:

▪Kuanzia Septemba 1 hadi April 30 kwa kila miaka miwili inayofuatana. Hivi sasa ni 1 Septemba 2014 hadi 30 April 2015

⚠⚠ Angalizo;

i.) Udhamini huu hautoi nauli ya ndege endapo utafanikiwa kuupata. Hivyo gharama zote za huko nyumbani (Tanzania) yaani visa, passport, medical checkup, nauli ya ndege na nyinginezo mpaka unafika China itakuwa ni juu yako. Vilevile ukifika hapa china hakuna kurudishiwa(compensation) gharama ulizotumia katika harakati zote hizo.

ii.) Barua pepe(email) address ambayo utaijaza katika form za maombi unatakiwa uwe na mazoea ya kuifungua mara kwa mara, usitumie ya mtu mwingine.

Mawasiliano yote na chuo baada ya kuwa umepitishwa kupata udhamini yatafanyika kupitia barua pepe yako.

Ushauri:

i.) Ni fursa nzuri kwa anayehitaji kujiendeleza kielimu na hawezi kumudu gharama. Muhitaji yeyote ambaye yupo tayari ajaribu fursa hii kwani utaratibu wa maombi upo wazi. Maombi ni kupitia internet,yanawafikia wahusika moja kwa moja hakuna urasimu.

ii.) Muombaji ambaye amemaliza chuo hivi karibuni tu na bado hajafanikiwa kupata Certificate yake asiwe na hofu anaweza kuanza mchakato wa maombi sasa, katika hatua za awali atatumia Transcript. Pia ambaye hana passport asiwe na hofu kwani si miongoni mwa vigezo vya kupata scholarship, isipokuwa itahitajika baadae wakati ukifika.

iii.) Gharama zote ambazo muombaji atakabiliana nazo(visa($80), passport($75), medical checkup, nauli ya ndege na pesa kujimudu safarini($700) ni takribani USD $900. Ambaye hawezi kumudu na uwezekano wa kuazima upo, basi anaweza kuazima(kukopa) pesa huko nyumbani na akazirudisha taratibu kwani gharama za maisha hapa china zipo chini hivyo kimakisio unaweza ukatumia kiwango cha chini USD $75 au $100 kwa mwezi hivyo ndani ya miezi 5 a 6 utaweza kukusanya USD $ 1000 kutokana na pesa za matumizi unazopewa na kurudisha ulichokopa. Pia gharama hizi ni makadirio ya juu endapo unamiliki passport, ukatumia BIMA yako afya, upande wa ndege ukafanya booking miezi miwili kabla ya safari basi gharama zitapungua.

Ukihitaji maelezo kutoka kwa chuo wasiliana nao:

Beijing Insitute of Technology:
Director International Student: Wany Ying
email :wangying318@gmail.com or yingwang@bit.edu.cn
Graduate Programs Coordinator: Chen Hui
email: master_phd@bit.edu.cn
Tovuti Maalum ya wanafunzi wa kigeni: http://isc.bit.edu.cn
Tovuti ya Chuo: http://english.bit.edu.cn

University of International Business and Economic:
Admissions Office, School of International Education
Email: sie@uibe.edu.cn
Tovuti ya Chuo: http://english.uibe.edu.cn"

Excerpt From: Appleseed, John. "Study in China." iBooks.
This material may be protected by copyright.

Chanzo: Zanzibar Ni Kwetu, tafuta chini ya mada - "NAFASI ZA MASOMO CHINA"
 

Attachments

  • china.jpg
    china.jpg
    5.9 KB · Views: 446
Wish to complete my BA degree as fast as possible
 
Wish to complete my BA degree as fast as possible

Then go ahead brother. The road is clear and paved!
Wachina wanajua ufisadi unaofanyika na rushwa inayotendeka katika kuchagua vijana kuenda kusoma nje na ndio maana wanataka vijana waombe moja kwa moja bila ya kupitia kwa fisadi au mlaji rushwa yoyote!!
 
Then go ahead brother. The road is clear and paved!
Wachina wanajua ufisadi unaofanyika na rushwa inayotendeka katika kuchagua vijana kuenda kusoma nje na ndio maana wanataka vijana waombe moja kwa moja bila ya kupitia kwa fisadi au mlaji rushwa yoyote!!


Aseee hiyo ni nzuri inaondoa favouritism and bureaucratic issue ni nzuri hiyo
 
Ngida1 a salute you.
Umetufungua wengi!
 
Last edited by a moderator:
aisee ni nzuri sana hio umefungua macho wengi thanks
 
Then go ahead brother. The road is clear and paved!
Wachina wanajua ufisadi unaofanyika na rushwa inayotendeka katika kuchagua vijana kuenda kusoma nje na ndio maana wanataka vijana waombe moja kwa moja bila ya kupitia kwa fisadi au mlaji rushwa yoyote!!

Mkuu nikitaka mwaka 2016 au 2017 nafasi zitakuepo??
 
Mkuu nikitaka mwaka 2016 au 2017 nafasi zitakuepo??

Usitake kubabaishwa na fisadi au mla rushwa yoyote, kiandikie chuo moja kwa moja kama unalo suala lolote lile. Nikikujibu mimi nitakuongopea na mwisho nitakuibia, ksababu ndivyo tulivyozowea kuibiana nchini hapa. Nakuhakikishia kuwa Wachina wanajibu kila msg wanayoipokea!
 
Unaweza kuapply moja kwa moja kwenye chuo husika china ukaweka Agency number ya chuo au ukaapply kupitia wizara ya elimu au ubalozi wa china hapa Tanzania. Ukituma applications ubalozini weka Tanzanian Agency number ambayo ni 8341
 

Attachments

  • Screenshot_2015-02-08-04-08-01.png
    Screenshot_2015-02-08-04-08-01.png
    80.5 KB · Views: 341
Fursa vijana changamkieni hiyo.Hicho kigezo cha umri,kitawabania wengi.Vipi ukiamua kujilipia mwenyewe kuna age restrictions?
 
Back
Top Bottom