Nafasi za kujitolea JKT

Nafasi za kujitolea JKT

intelligence hiyo kazi yao ni kuchunguza... unadhani utaweza kuwachunguza?

Si uchunguzi wa nia mbaya, vijana wanatamani kua walinzi wa taifa lao ndio maana wakaitaji uelewa juu ya vyombo ivyo.
 
Habari ndugu Mujo na wengine wote mnaofatila nafasi za jkt na jwtz pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama! Utakapo itaji taarifa za uandikishwaji wa vijana wa kujitolea nakushauli utembelee mala kwa mala website ya chombo husika maana hapa jf na mitandao mingine ya kijamii utakutana na majibu ya kukuchanganya maana kila mmoja atakuja na lake. Nazungumza hivi kwa kuwa nina uzoefu na majibu ya miaka iliyopita yaliyojibiwa na wachangiaji mbalimbali kwa watu waliotaka kujua juu ya nafasi za vyombo husika hususani jkt. Kwa nijuavyo mimi ni kwamba kila mwaka huwa wanachukua mala moja na nafasi hutangazwa mwezi wa 12 na mafunzo huanza mwezi wa tatu, lakini kwa maelezo haya yasiwe ni jibu kamili kwako bali jibu kamili utalipata kwa wahusika (jkt) kwa kutumia website yao (www.jkt.go.tz) bila kificho maana nafasi hizi ni kwa vijana wote raia wa Tanzania. Asanteni!!

Tunashukuru mkuu kwa maelezo
 
Back
Top Bottom