Nafasi za Kazi za Ndani Middle East

Nafasi za Kazi za Ndani Middle East

Voltaire

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2013
Posts
1,964
Reaction score
2,188
Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisheni watanzania wenzangu kwamba,kuna nafasi nyingi za kazi za ndani (kupika,kudeki,kuosha vyombo,kulea watoto wadogo na wazee pamoja na za usafi wa mazingira).

VIGEZO:

Umri miaka 22-44.
Akubali kupima magonjwa yote atakayotakiwa kabla ya kuondoka ikiwa ni pamoja na ukimwi.
Gharama ya passport kama hauna utailipia mwenyewe.
Akubali mkataba wa kufanya kazi miaka miwili.
Elimu ni form four au darasa la saba lakini awe na uelewa wa kiingereza kidogo cha maneno,kama,baby,food,clean na zaidi.

MENGINEYO:

Mshahara ni $250-400.
Ticket ya ndege ya kwenda na kurudi.
Usalama wako utahakikishwa sababu wizara ya mambo ya nje ya Tanzania na ya Kuwait zitakuwa na taarifa zako.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 0768883183.
 
tumeishawajua ninyi, waongo wakubwa, kazi zenu za kudhalilisha watu tumeishawastukia, sasa ole wenu dawa yenu iko jikoni inachemka!
 
Funny...kama hautaki kazi tafadhali usiwakatishe wenzako tamaa...sijajua hata unaongea kwa data zipi ulizonazo koz watanzania wengi tu tumewapatia kazi na wanawasiliana vyema na ndugu zao, please,tusilitumie hili jukwaa vibaya,liwe ni ngazi ya kukwamuana na kujengana kwa fikra na fursa sio mambo ya ajabu ajabu!
 
hawa waarabu wanatutesa huku Bongo ba vielimu vyetu sasa tukienda kwao si ndio tutakoma.
NASIKIA WANAKUHASI ILI USIJE ZAA NA WATOTO WAO. AKUU
 
Hiyo namba ya simu mbona siyo ya uarabuni?? Au ndo wizi unaanzia hapo? Danganya jingajinga.
 
Namba ni ya Tz koz ni wakala hapa Tz,ok,wa Tz tuna tendency ya ku politisize kila kitu,so far Kenya na Uganda zimekuwa zikipeleka watu wengi tu na fursa nyingine zinafungukia huko huko,mwenye macho haambiwi tazama!
 
Ya kweli haya jamani!!!?

Ukweli ni ya kweli. Nilishakutana na mama moja Mtanzania uwanja wa Bole, Ethiopia. Katika mazungumzo akaniambia kamaliza mkataba wa miaka miwili uarabuni akifanya kazi za ndani. Nilimwuliza kuhusu fununu za unyanyaswaji akasema yeye binafsi hakunyanyaswa na alikuwa hata anafikiria kurenew mkataba kwani waajiri wake waikuwa wamemwomba arudi.
 
tumeishawajua ninyi, waongo wakubwa, kazi zenu za kudhalilisha watu tumeishawastukia, sasa ole wenu dawa yenu iko jikoni inachemka!

Acha wadada waende wakapige kazi.
Si unajua waarabu wanaoa wanawake bikra, lakini inabidi wajifunze majambo kabla hawajaoa, acha wadada waende wakawe specimen za kujifunzia.
 
Funny...kama hautaki kazi tafadhali usiwakatishe wenzako tamaa...sijajua hata unaongea kwa data zipi ulizonazo koz watanzania wengi tu tumewapatia kazi na wanawasiliana vyema na ndugu zao, please,tusilitumie hili jukwaa vibaya,liwe ni ngazi ya kukwamuana na kujengana kwa fikra na fursa sio mambo ya ajabu ajabu!

mdau watu wana doubt maana wengi waliowai fanya kazi middle east kwakweli ushuhuda wanaouleta huwa -vely,sasa unapaswa kuwahakikishia watu hapa,nimefatilia hizi mambo si tanzania hata kenya nao wameshawai kuelezea hizi changamoto,pamoja na Uganda hii niliiskia BBC
 
Namba ni ya Tz koz ni wakala hapa Tz,ok,wa Tz tuna tendency ya ku politisize kila kitu,so far Kenya na Uganda zimekuwa zikipeleka watu wengi tu na fursa nyingine zinafungukia huko huko,mwenye macho haambiwi tazama!

mdau hapa jf lazima watu wahoji,wewe au huyo mwenye namba ni agent ambae ana kamishen yake so lazima a-romanticise,lakini kiukweli manyanyaso yapo babu,watu weus tunasumbuliwa sana ughaibun,haya mambo kila uchao yanaripotiwa
 
Aya sasa wanaokwenda waende but wawe makini katika kazao maana wengine wakienda kule wanakwenda kuwa...
 
Ukweli ni ya kweli. Nilishakutana na mama moja Mtanzania uwanja wa Bole, Ethiopia. Katika mazungumzo akaniambia kamaliza mkataba wa miaka miwili uarabuni akifanya kazi za ndani. Nilimwuliza kuhusu fununu za unyanyaswaji akasema yeye binafsi hakunyanyaswa na alikuwa hata anafikiria kurenew mkataba kwani waajiri wake waikuwa wamemwomba arudi.
Inaweza huyo mama akawa kweli hakunyanyashwa lkn kuna taarifa mbalimbali kupigia kwa wasichana ambao wameshawahi kwenda kufanya kazi katika maeneo hayo na wamelalamika kufanyiwa vitendo hivyo na mie Mwenyewe shemeji yangu alishawahi kwenda karudi
 
Kuhusu issue ya udhalilishaji, jee hapa nyumbani wafanyakazi wa ndani hawadhalilishwi! Jee mishahara ya shilingi 30,000 - 60,000 kwa mwezi walipwazo wengi wa house girls na barmaids sio pia udhalilishaji?

Cha msingi ni kwamba ajira isiwe ya kinyemela, serikali iitambue na balozi zetu huko uarabuni zijue watu wetu waliko. Acheni wawezao wachangamkie nafasi hii ya ajira wajikwamue angalau kwa muda! wanaobeza mshahara wa dola 450 kwa mwezi, hebu walinganishe na shilingi 50,000 za housegirl au barmaid nyumbani.
 
Mi hua namshangaa sana mtu ambae anaeongea pumba kama vile ati sijui nyie waongo maneno mengi ya kijinga bila kuchunguza, hivi shekhe au padri akiwa mlevi utasema dini ndo inafundisha hivo? wakati ni mapungufu ya mtu.

Kesi ile ilikua ni hivi, Huko arabuni walikua wanataka machangudoa ili wawaweke kwenye madanguro yao wapige hela, na wakatafuta ma agent wenye kujua nchi yao watafute wanawake warembo, sasa ma agent badala ya kwenda kubeba machangu wakaona washachuja sasa njia nzuri ya kupata watu ni kwa kusema wanahitaji wasichana wa ndani, maana ukimwambia mtu unaenda kua changu wasingepata watu, na ni kosa la hao ma agent na sio hao waarabu.

Watu kibao wapo nje na wanapiga kazi fresh na hawataki kurudi, hela hiyo ni sawa na mshahara wa offisini dola 250-450 ni laki 4 mpaka 7.

Kuhusu unyanyaswaji hakuna kitu kama hicho ili kutengwa tegemea hilo na mapema, utakua unatumia kila kitu chako tofauti, kwanzia vyombo vya chakula mpaka choo na bafu, ila nayo sio wote.

Cha msingi kabla hawajaenda wawe na uhakika na hao ma agent na pia wawe na uhakika na taarifa zao ziwe ubalozini.

Tuache maneno ya kijinga, ndo maana hatuendelei. Manyanyaso yapo hata kwa rangi nyeusi ma house girl mara ngapi wananyanyaswa na wabongo wenzao.

Ni hayo tu.
 
Acha wadada waende wakapige kazi.
Si unajua waarabu wanaoa wanawake bikra, lakini inabidi wajifunze majambo kabla hawajaoa, acha wadada waende wakawe specimen za kujifunzia.

umeona ee? jamani, yaan mimi nina ushahid wa ndugu yangu, nafasi zilitangazwa tena mpaka kwenye magazeti na wakaweka namba za sm za tz, na hukohuko kuwait! lakini walichofanyiwa! hata sijui kama shirika la haki za binadam kama wanajua huo ukatili unaofanywa na hao watu wa kuwait, wanadanganya eti wana kazi afu wanawatumia watz wenzetu kutangaza hizo kazi! ila mi nasema mwisho wao upo tu, hizo nafsi wanazozitesa zitawalilia!
 
Mwaka juzi nilikutana na mama mmoja ametokea dubai jomo kenyeta airport alikuwa anafanya kazi za ndani. alinionesha makovu ya kupigwa na anasema alinyang'anywa pass yake so akawa awezi kutoroka anasema mpaka wamemrudisha amewasumbua sana na kwenda ubalozini ndio pona yake na hapo airport alikuwa anasubiri flight yake ya kuja dar saa kumi na moja jioni me nilimkuta asubuhi

Arabuni upate profession job nahisi utakuwa uhuru
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom