Nafasi za kazi, mhasibu CORECU LTD

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,432
1,387
Position: MHASIBU
Coast Region Cooperative Union (CORECU LTD)

Job Summary
Ili kuhakikisha kinaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake, CORECU (1984) Ltd kina tangaza nafasi ya kazi iliyooneshwa hapo chini kwa Watanzania wenye sifa.

Minimum Qualification: Bachelor
Experience Level: Mid level
Experience Length: 3 years

Job Description
Chama cha Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani (CORECU (1984) Ltd chenye namba ya usajili Na. 5008 kilisajiliwa mwaka 1985. Chama hiki kilianzishwa kwa dhumuni la kutoa Huduma Bora kwa wakulima wa mazao ya Korosho, Ufuta na Pamba kwa Mkoa wa Pwani.

SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe na elimu isiyopungua Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu katika Uhasibu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
  • Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta na mifumo mbalimbali ya kifedha pamoja na sifa nyingine za ziada kadiri itakavyoonekana inafaa;
  • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 3 katika nafasi aliyoomba;
  • Awe nasifa ya uadilifu;
  • Awe hajawahi kufukuzwa kazi kwa tuhuma za upotevu wa fedha;
  • Awe na umri kati ya miaka 25 hadi 45.
MAJUKUMU YA KAZI
  • Kusimamia utendaji wa kazi katika Idara ya Uhasibu;
  • Kusimamia utunzaji wa mapato ya Chama na Kuhakikisha matumizi ya naendana na yale yaliyoidhinishwa;
  • Kusimamia utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka na kuwasilisha bajeti kwa Meneja wa Chama;
  • Kutoa taarifa ya fedha za Chama kila mwezi, kila baada ya miezi mitatu na mwisho wa mwaka kwa Meneja wa Chama;
  • Kutoa ushauri mara kwa mara kwa Meneja kuhusu hali ya mapato na matumizi ya Chama; (vi) Kutayarisha na kutoa malipo yaliyoidhinishwa na mamlaka ya fedha kulingana na taratibu za fedha za Chama;
  • Kufanya malinganisho ya miamala ya leja kuu na hesabu za benki kila mwezi;
  • Kubuni mbinu za kupata mapato ya ziada kwa Chama;
  • Kushirikiana na wakaguzi wa hesabu wa ndani na nje katika kukamilisha ukaguzi wa hesabu za Chama;
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wakazi;
MSHAHARA
Kiwango cha mshahara kitakuwa kwa mujibu wa viwango vya Chama

MASHARTI YA KAZI
  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wakuaminika,
  • Barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainiwa;
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika,
  • Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificate from respective Board) “Testmonials” “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE)
  • Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
  • Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushiwa husika watachukuliwa hatua za kisheria
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATA FIKIRIWA
  • Maombi yote yatumwe kupitia anuani tajwa hapo chini
MWENYEKITI WA BOADI
CORECU LTD
S.L.P. 30182,

KIHABA - PWANI

E mail: corecupwan@gmail.com

Mwisho wa kupokelewa kwa maombi yote ni tarehe 23 Juni, 2020 saa 10:00 Jioni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom