Nafasi za kazi AHB project

KANOSAWA

Member
Sep 16, 2016
55
39
Njoo kazini utapata nafasi
Tunachakata taka (Recycling)
Tunahitaji Waokotaji Taka (Waste Pickers), toka majiji na mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.
Mwisho wa Maombi 30/6/2024
Tupigie Tafadhali +255 789 753 808. Usitume Sms. Au tuandikie africahomebinahb@gmail.com
MAGNETIC MIND.jpg
 
Mmefikia hatua kwamba kuna member humu tunaweza okota makopo
Nashukuru kwa maoni yako.
Hii platform ni ya jamii na ako na freedom ya kuweka anything positive to the society.

Kama ulikuwa hujui hapa nchini kuna viwanda vinahitaji Malighafi Taka zaidi ya tani 200 kwa siku. Na ni viwanda vya wawekezaji. Na mwekezaji hawezi kuweka kiwanda pasipo ruhusa ya Mwenye nchi yake.

Uwekezaji huu ni faida kwako, kwa kuwa mwokotaji taka hadi mwekezaji wanachangia pato la taifa. Kwani pesa hizo zinatumika kwa namna mbalimbali kwenye maendeleo ya jamii.

Pili, watu wengi wanaamuka asubuhi kwenda viwandani jambo ambalo ni jema. Muokotaji taka ni sawa na anayeenda kiwandani kwa sababu waliomo ndani ya viwanda hususani vya Uchakataji Taka (Recycling); hawawezi fanya lolote bila malighafi taka toka huku nje ya kiwanda.
Mfano: Mtengenezaji wa Tishu unayoitumia hotelini hawezi itengeneza bila box lililookotwa na mwokotaji taka.
Mtengenezaji wa mfuko hii mbadala ya mifuko ya rambo hawezi tengeneza bila taka boksi nk nk.

Tatu, hii ni fursa ya ajira na inaajiri watu wenye akili zao timamu; sema tu imezoeleka kuona walaibu wa unga humo mitaani kana kwamba ndiyo wenye kazi. La hasha !!! Walaibu wamo humo kwa kuwa fursa ina nafasi za ajira kwa wenye darasa sifuri hadi graduates. Inategemea tu ni utaratibu gani mmejiwekea.

Kwa hiyo, kama umenielewa; AHB Project tuna fursa za kazi kwa wenye sifa zifuatazo
  • Awe na darasa zero na kuendelea hadi chuo kikuu
  • Awe na akili timamu
  • Asiwe anatumia kilevi chochote hususani madawa ya kulevya
  • Awe na afya njema

Na isitoshe wote waombaji wanaingizwa darasani kwa mafunzo hususa kwanza (Induction Waste Training)

Nne, tuna nafasi za Mafunzo Maalum kwa wenye mitaji na Unatamani na wewe kuendesha Mradi au Biashara aina hii. Nawakaribisha pia.
Asante mdau wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom