Nafasi ya Waziri Mkuu katika utawala wa Serikali inaweza kupunguzwa

Yule ni mwanasheria na ukiangalia comedy zake utajua uRais haukuja bahati mbaya
Sasa usingesema tu muuza duka anaweza kuwa rais kwa kuona ni kituko wakati anaweza akawa na elimu yake yenye kustahili kuwa rais.
 
1.Ubunge wa viti maalum na wa kuteuliwa ufutwe

2.Nafasi za Mkuu wa wilaya zifutwe, wabaki DAS.

3. Ziara za mawaziri zidhibitwe, hakuna haja ya waziri Nape kuzunguka na chopa.

4.Nafasi za Manaibu waziri zipunguzwe, wabaki makatibu wakuu wa wizara.

5.Punguza ununuzi wa magari ya kifahari.
Waziri mkuu ni ''dude'' linalokula fedha za bure kabisa. Hiki cheo hakina faida yoyote na mbaya zaidi mawaziri wakuu wamekuwa kama mzigo wa mawe hasa kuanzia awamu ya 4. Infact serikalini na mashirika ya umma kuna sehemu nyingi sana za kupunguza matumizi kwa kuondoa vyeo na wafanyakazi wasio muhimu na pia kuondoa matumizi ya anasa kama kusafiri kwa first au business class, kusafiri na ziara, vyombo vya usafiri avoidable, yaani kuna sehemu nyingi sana..
 
Na Waziri siyo lazima awe Mbunge,mtu yeyote mwenye uwezo kutoka nje ya Bunge ateuliwe.
 
Unaunga hoja ya msingi mkono ?
Au umekuja kuonyesha uchungu wako tu dhidi ya waliokuwa wanaipopoa legacy ya mpendwa wako na watu wake?
Uzuri wa Mbongo akili Kama panzi, Hakuna anacho simamia.

Wanachojua ni kufuata mkumbo tu.

Baada ya serikali ya Samia kupata madaraka stori zikaanza , ooh Majaliwa atoke Majaliwa atolewe.

Wenye akili wakashauri, gharama za kuhudumia wastaafu Ni kubwa kuchagua WM mpya halafu na anayeondoka kuhudumiwa Ni gharama avumiliwe amalizie.

Misukule ya Wanasiasa yenyewe OOOh oooh Mbowe kasema ajiuzulu.

Haya Leo uko Happ tena unabweka kuwa kuhudumia mawaziri wastaafu 8 Ni gharama.

Na, Je angekuwa ametumbuliwa MAJALIWA na Sirro Kama wanasiasa mnavyotaka ?? ingekuwaje?
 
Unaunga hoja ya msingi mkono ?
Au umekuja kuonyesha uchungu wako tu dhidi ya waliokuwa wanaipopoa legacy ya mpendwa wako na watu wake?
Leta hapa ushahidi kuwa Mimi nimewahi kumuunga mkono Kibwengo magufuli.

Ukishindwa kuleta ushahidi, basi UNAKALIA 👇👇👇

20220216_225742.jpg
 
Wakati huu ambapo tupo kwenye kupanda kwa bei za mafuta na nishati nyinginezo anayetazamwa ni waziri wa nishati na Rais.

Mbolea na pembejeo za kilimo zikipanda bei anayetazamwa ni Waziri wa Kilimo na Rais.

Usumbufu wa panya road wanaotazamawa na kusemwa ni IGP, waziri wa ulinzi na Rais.

Matatizo ya maji yanaelekezwa kwa waziri wa maji na Rais.

Kupanda kwa vifurushi na kufungiwa magazeti anawajibika na lawama zinaenda kwa waziri wa habari na Rais.

Mikopo ya wanafunzi wanaonekana moja kwa moja ni waziri wa elimu, bodi na Rais.

Ukiangalia mtiririko huo utaona katika muundo wa serikali kuu ni waziri wa wizara husika na Rais ndio wanaoonekana wanawajibika na maisha ya wananchi moja kwa moja. Ni mara nyingi pia tunamsikia Rais akitoa maelekezo moja kwa moja kwa waziri husika bila kupitia kwa waziri mkuu.

Kwa mantiki hii ni sahihi kuendelea kuwa na nafasi ya waziri mkuu kwa kigezo tu cha mtendaji mkuu wa serikali?

Mawaziri hawawezi kuwajibika kwa Rais moja kwa moja kama zilivyo nchi nyingine nyingi zenye mfumo wa Urais wenye nguvu kama huu wa kwetu ?
Well said, ila hata nafas za DC ,RC, manaibu waziri, naibu spika zingine nyingi tu kwa nchi yetu zina umhimu ila sio za lazima zinaweza kuondolewa na nchi nikawa poa tu.
 
It will make a lot of sense kama serikali itabana matumizi kwa kupunguza nafasi za kiutawala hawa wote wanalipwa, wanapewa ulinzi, madereva. Mi naona hata idadi ya wabunge ipunguzwe sijawahi kujua kazi yao haswa ni nini
 
Back
Top Bottom