Nafasi ya mume. . .

....huyu mzee hajawahi kuusikia ule msemo, "...be careful what you wish for!"...
Mke msomi anaweza kuwa chachu au chungu kwenye ndoa yako kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako,
mfano akiwa ni mtumishi wa umma, mbunge, nk, nk....yeye siku zote yu kwenye semina, vikao, safarini tuu...

Ridhika na maajaaliwa yako bana.

Ndugu yangu Mbu,

Wishes do cost nothing.

Hata hivyo ni human nature kutamani kile ambacho hakuweza kukipata.

Ila hii wish yangu inatokana curiosity na kushindwa kupata majibu ya hii phenomenon ya kuwaogopa wanawake wasomi. Halafu mbaya ni kwamba, wengine tumehangaika sana kuhakikisha wake zetu wanapata elimu ya kutosha ili wajitegemee kwa vitu vyao muhimu...

Kaka, inakera sana kama ukiwa na mwanamke ambaye anakuomba kila kitu hata hygiene towels!!

Babu DC!!
 
.....Mkuu DC unamwaga vitu vilivyojaa hekima na busara ya hali ya juu na ni ukweli mtupu. Hongera zako bana!!! Wanaume wanaogopa wanawake wasomi, lakini hawajui mke msoni ni asset kubwa sana kwa familia ukilinganisha na yule ambaye aliishia madarasa ya chini ama kwa kuukimbia umande au kutohimili mikiki mikiki ya shule.

Nadhani watu hawaelewi,

Hawa ndugu zetu ukiweza kuwahandle vizuri na kuwapa uhakika wa maisha yao, wanafungua kila kitu chao na kukubwagia mezani...Nadhani wanawake wengi wako hivyo...

Wakati binafsi najikuta nakuwa mkali na pesa zangu, Bibi DC akipata boom la kutosha hakawiii kuleta kila kitu na kumwagia nifanyie lolote ninalotaka...of course anajua kuwa siwezi kuhongea iwe pesa zangu au zake!!

Babu DC!!
 
Ndugu yangu Mbu,

Wishes do cost nothing.

Hata hivyo ni human nature kutamani kile ambacho hakuweza kukipata.

Ila hii wish yangu inatokana curiosity na kushindwa kupata majibu ya hii phenomenon ya kuwaogopa wanawake wasomi. Halafu mbaya ni kwamba, wengine tumehangaika sana kuhakikisha wake zetu wanapata elimu ya kutosha ili wajitegemee kwa vitu vyao muhimu...

Kaka, inakera sana kama ukiwa na mwanamke ambaye anakuomba kila kitu hata hygiene towels!!

Babu DC!!

Kumbe wamejaa watoto .... .... ..
 
kinachofanya mke ndo atofautiane na ndugu wa mume ni ile assumption kuwa mke anaondoka kwao na kujoin hii familia. kumbuka being sent off, you belong to the new clan! mimi naamini kwa tabia yoyote ndugu wa kiume walio nao, mke unaweza kuishi bila kutofautiona nao. Tatizo wake pia hutumia nguvu nyingi sana zisizo na sababu kutetea nafasi yao. Mke jifunze kunyama katika hali kama hizi, your sisters in law will never sleep with their brother! unachoweza kufanya ni kumpa mume wako mapenzi ya kumtosha asipate confusion! Jifunze kutokumpa mume wako nafsi ya kukuchagua wewe na ndugu zake, uchaguzi wowote atakaofanya utamuuma!Akikuchagua wewe akaacha dada zake si sawa, kuna mambo mengi tu ya kifamilia ambayo yatamfanya awahitaji na wala wewe huwezi kucheza hiyo nafasi, na akiwachagua wao akakuneglect wewe atapata msongo, maana kila uchao lazima mkutane, possibly kwa physical zero distance! mom, jifunze kupenda mawifi zako kwa hali yoyote. they can make good friends!
kumbuka
mke mwenye hekima hujenga nyumba yake, mpumbavu hubomoa tena kwa mikono yake(bila kusaidiwa na mawifi zake)

Tatizo lako wewe hujaelewa bado au unakataa kuelewa bado.

Let put this way, kwenye ndoa yoyote lazima kuna up and down au vipi, ikiwa nyie mnawapa chance watu wajue matatizo yenu basi weka akilini mtailetewa tu matatizo na watu.

Kama mme anaonyesha dalili siku zote mbele za ndugu zake na wazazi wake anampenda mke wake, vipi watasababisha matatizo katika ndoa yake.???

Unless huyo mwanaume kila wakati yuko kulalamika kwao kuhusu mke wake, hata kama mke wake kachelewa kumfanyia chai basi anaenda kupiga report kwao mke wake kachelewa kumfanyia chai.

Mimi naamini wazi kabisa Mme na Mke wakiwa napendana nawako kitu kimoja nawanamaliza matatizo yao wao kwa wao, hakuna atakaye subutu kuwaleta matatizo.

Siku njema.
 
kinachofanya mke ndo atofautiane na ndugu wa mume ni ile assumption kuwa mke anaondoka kwao na kujoin hii familia. kumbuka being sent off, you belong to the new clan! mimi naamini kwa tabia yoyote ndugu wa kiume walio nao, mke unaweza kuishi bila kutofautiona nao. Tatizo wake pia hutumia nguvu nyingi sana zisizo na sababu kutetea nafasi yao. Mke jifunze kunyama katika hali kama hizi, your sisters in law will never sleep with their brother! unachoweza kufanya ni kumpa mume wako mapenzi ya kumtosha asipate confusion! Jifunze kutokumpa mume wako nafsi ya kukuchagua wewe na ndugu zake, uchaguzi wowote atakaofanya utamuuma!Akikuchagua wewe akaacha dada zake si sawa, kuna mambo mengi tu ya kifamilia ambayo yatamfanya awahitaji na wala wewe huwezi kucheza hiyo nafasi, na akiwachagua wao akakuneglect wewe atapata msongo, maana kila uchao lazima mkutane, possibly kwa physical zero distance! mom, jifunze kupenda mawifi zako kwa hali yoyote. they can make good friends!
kumbuka
mke mwenye hekima hujenga nyumba yake, mpumbavu hubomoa tena kwa mikono yake(bila kusaidiwa na mawifi zake)

Sidhani kama ni suala la kuchagua upande, bali ni jambo la kuweka mipaka. Kitu gani ndugu wanaweza wakaingilia na kipi hakiwahusu.

Huwezi kukaa kimya wakati ndugu wanafuatilia uwezo wa mkeo kupika eti hutaki kuchagua kuwa upande wa mke......

Ndugu wabaki na mambo yanayotuunganisha kama ndugu wa baba na mama mmoja, ila yale yanayohusu mie na mke wangu na familia yangu watuachie wenyewe. Labda kama nimeamua kuwashirikisha au kama kuna jambo la hatari mke wangu amelifanya na wana ushahidi ambao wako tayari kuutoa popote hata mbele ya mke wangu!!
 
. . . kwenye conflict kati ya mke na ndugu wa mume.

Kwanza nianze kwa kuuliza. .
Hivi kwa nini ndugu wa upande wa mume (mawifi, mashemeji, mama mkwe) ndio hua wanaonekana kusababisha matatizo zaidi kwa wanandoa kuliko ndugu wa mke? Hii inasababishwa na nini?

Hili linaweza kuwa kweli au si kweli, kutegemea na jamii unayoongelea. Kuna jamii ambazo mwanamme na mwanamke "wanaoana" (kila mmoja anamuoa mwenzake) na kuna jamii ambazo mwanamme anamuoa mwanamke (kama jamii nyingi za kiafrika) na kuna jamii chache sana ambazo mke anaoa.

Nafikiri katika context yako unaongelea zaidi jamii zetu za kiafrika nyingi ambazo mume "anamuoa" mwanamke.

Kwanza mpaka hapo ushapata sehemu ya jibu. Ndoa imejengwa kwa msingi wa "mume kumuoa mwanamke". Kwa hiyo traditionally inakuwa kama familia ya mwanamme "imemchukua" mwanamke kutoka kwao. Kuna tamaduni nyingine hata kwenye harusi kaka na dada wa mume humpongeza kwa "kutuolea". Na hata mume akifa mdogo wake anaweza kumrithi mke (moja ya sababu za maambukizo ya Ukimwi).

Mfumodume huu mara nyingi humuangalia mwanamke kama chombo/ kitu, ndiyo maana analipiwa hata mahari. Na familia nyingine hufikia hata kudai mahari kama ndoa itavunjika.

Nikirudi kwenye nilichokusudia kuandika, juzi nilikua naongea na mtu maswala ya ndoa including mahusiano kati ya mke na ndugu wa mume yanavyoweza kufanya ndoa iwe chungu ikiwa hakutakua na maelewano kati yao. Mwenyewe aliniambia kwamba "matatizo yanayosababishwa na ndugu wa mume yanatokana na mume kutokua MSIMAMO pia SAUTI mbele ya familia yake."

Hili lina ukweli kiasi fulani. Lakini mimi nataka niliangalie kwa upana zaidi. Tatizo la msingi ni mila na tamaduni zilizopitwa na wakati ambazo zinachangia wanawake kuwa tegemezi na kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa kama mali. Kwa mfano, habari nzima ya kutoa mahari inachangia kumfanya mwanamke awe kama mali "inayonunuliwa" na mwanamme. Kama ndoa ni upendo, na inatakiwa kuwa ya usawa, kwa nini mahari itoke kwa mwanamme kwenda kwa mwanamke? Kwa nini kuwe na mahari? Naweza kuelewa a mutual exchange of symbolic gifts, lakini hizi exhorbitant mahari zinakuja kufanya mwanamme aonekane kama anamnunua mke. Mwisho dada wa mume wanasema "tumekutolea ng'ombe arubaini, tufulie nguo zetu".

Kinachotakiwa sio tu kukemea wanaume wanaoendekeza udhalilishwaji wa wake zao, bali mfumo mzima unaomnyima mwanamke nguvu za kiuchumi na kumfanya awe chombo cha mwanamme na familia yake. Si haki kumkemea mwanamme tu wakati yeye ana dada zake ambao nao wanaendeleza ukandamizwaji wa mwanamke mwenzao. Vita dhidi ya ukandamizwaji wa wanawake isigeuke vita ya jinsia kati ya wanaume na wanawake. Kuna wanaume na wanawake wanaokandamiza wanawake kama vile kulivyo na wanaume na wanawake wanaotetea haki za wanawake.

Nilipofikiria nikaona kwamba kuna ukweli mwingi ndani yake. Embu fikiria ukiwa na mawifi wasiojua kutulia kwao, na kwako wakija ni maneno tu alafu kaka yao nae akawa anawaacha tu na kupuuza malalamiko ya mke wake nini kitatokea?
Mawifi wataendelea au hata kuzidisha mbwembwe zao pale, mke atakasirika kwa kuingiliwa na mawifi + kupuuzwa na mume hivyo kupunguza au hata kuondoa maelewano kati ya mume na mke.

Wanaume nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha familia zenu (mama, baba,dada na kaka) wanaelewa kwamba nafasi yao ni tofauti na ya mke wako.

Hili ni jukumu la wote. Naelewa kwamba ni rahisi kwa mwanamme kuwasiliana na familia yake zaidi ya mke wake, hasa kama kuna tension. Lakini mwanamke naye anatakiwa kuwa na msimamo. Wanaume wengi wangeweza kupewa motisha zaidi kuwakemea dada zao kama wanawake wengi wangekuwa na ujasiri zaidi wa kutoa msimamo. Lakini tunarudi bado kwenye swala la mfumo wa uchumi uliojengwa katika mfumodume. Hat kama kuna exception chache siku hizi ambazo baba na mama wanafanya kazi, traditionally baba ndiye breadwinner wa familia, na kwa hilo wanawake wengi huona kum confront baba squarely kunaweza kuharibu dynamics za kiuchumi ndani ya nyumba. Mke anaogopa kuambiwa "Unataka kunigombanisha na ndugu zangu" anaumia kimya au kwa kusema chinichini. This is not blaming the victim, it is a mere wake up call.

Kwamba ukishaoa unakua na familia nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa inatakiwa ijitegemee (uongozi na maamuzi ndani ya nyumba) hivyo hawaruhusiwi kuingilia iwapo hamjawaomba kufanya hivyo.

Ukweli ni kwamba hii (nuclear family) ni concept ya kimagharibi zaidi na kwetu kama nilivyosema hapo juu, mwanamke "anaolewa" na mume na pengine na familia ya mume. Kutegemea na mazingira na mambo kama kisomo, uwezo wa kiuchumi, tamaduni na exposure. Lakini wabongo wengi hawana utamaduni wa nuclear family. Mimi nishaona mshkaji wangu (mbongo) kaharibu katika ndoa yake, mkewe (mmarekani) akawa anajaribu kumsemea kwa kaka yake, kaka mtu kamwambia dada yake "matatizo yenu ya ndani ya nyumba muyamalize wenyewe ndani ya nyumba". Nikaona hawa watu wako tofauti, angekuwa mbongo lingekuwa zogo hapo. As it turns out uamuzi ule ulikuwa wa busara kiasi kwani wanandoa walipatana na shemeji akaendelea kuwa na mahusiano nao mazuri wote. Imagine angeingilia kwa kumtetea dada yake, halafu wanandoa wapatane, jamaa angemuona mduanzi siku zote.

Na inapotokea wakajaribu uwaeleze kwamba hivyo sivyo mambo yanavyoenda. Badala ya kumwambia mkeo awavumilie tu, wakalishe ndugu zako chini uwaeleze kwamba mkeo hayuko pale kwaajili yao, kama wanaona anayofanya hayawapendezi wao ilhali wewe huna tatizo nayo basi nao watafute maboma yao ili wakafanye mambo wapendavyo huko. Usiruhusu maneno maneno ya ndugu zako yamkoseshe mkeo raha, hata kama ni madogo. Ndugu zako ndio wanaotakiwa kuBEHAVE na sio mke wako KUWAVUMILIA.

Kuna tabia nyingine ziko deep rooted na zimetiliwa mbolea ya miaka mingi ya malezi. Wewe familia ina watoto saba, mumeo kitindamimba na mwanamme pekee, matokeo yake kaishia kuwa mtoto wa mama na kazoea kuwa protected na dada zake (sisemi kwamba watu wa hivyo ndizo tabia zao, mfano tu). Anakuoa, hujafanya uchunguzi wa kutosha kumjua yeye na historia yake katika familia. Baada ya kuolewa unakuta vituko vya mawifi. Unajaribu kumbadilisha mtu. Good luck.

Hapa ndipo inapokuja sehemu ya kuchunguzana kabla ya kuoana. Zamani kabla ya kuona watu walikuwa wanafanya uchunguzi wa kutosha. Siku hizi watu wanakutana Facebook, washapanga mipango ya kuoana hata kabla hawajaonana, wakionana wiki mbili wametangaza ndoa, ndoa fasta kuliko quickies za Las Vegas. Matokeo yake umeoa ndoto kama wanavyosema "man of my dreams" lakini hawajamuoa mtu halisi.

Kwa hiyo kuepuka "majuto mjukuu" mchunguze mtu wako, ikibidi hamna kuoana bila ya uchumba wa kuwa karibu kwa kipindi cha angalau miezi sita.

Heri ya mwaka mpya. . . . natumaini utakua mzuri kwetu sote.

Na wewe pia.
 
Kiranga asante kwa uchambuzi mzuri. Umenisaidia kuelewa mambo mawili matatu ambayo siku nimefikiria.
 
JAMANI JAMANI JF MEMBERS!!!

Ukweli utabakia kuwa maswala ya ndoa yanahitaji hekima ya hali ya juu sana. Na hekima hii kwa ninavyojua na kuamini hupatikana katika vitabu vya Mwenyezi Mungu (both Qur-an and Bible).

Niaze tu kwa kusema kwamba kasoro zozote zinazojitokeza katika ndoa na kuanza kuchunguza kasoro za mume au mke KWA MADHUMUNI MABAYA (yasiyo ya kujenga bali kuvuruga) ni dalili tosha ya kwamba aidha UPENDO UMEPOA au UMEISHA KABISA. Kwa kuwa kimsingi hakuna mtu yeyote duniani aliye kamili/mtimilifu yaani ''NO BODY PERFECT" Lakini kama mtu akikosea (mke au mume) basi yapendeza kurejeshana kwa upendo (KWA NIA YA KUJENGA(NA) (KI)UPENDO) na si kwa chuki wala kubomoa sawa na neno la Mungu katika Biblia "Ndugu zangu, kama mtu akipatikana na dhambi fulani, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejezeni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa. 2Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Kristo. Wagalatia 6:1-2" na katika Quran "SURAT ASH-SHUURA 40. ...Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu." KWA HIYO KUSAMEHEANA NI JAMBO MUHIMU SANA KATIKA NDOA.

PIA "Kuchukiana huondokesha fitina, bali kupendana husitiri makosa yote. Mithali 10:12" Kwa hiyo mwanzo wa chuki na kutokusameheana ni kwamba upendo umeisha. Kwa wanandoa hawana budi kutafuta source ya tatizo.

MIGOGORO NDANI YA NDOA KUTOKA KWA WAKWE, MAWIFI NA MASHEMEJI.
Katika hili mume anatakiwa kujua kwamba mke wake ni mke wake na tena ni ubavu wake mwenyewe i.e mke wake ni yeye mwenyewe, na YAMPASA AMLINDE MKE WAKE (AJILINDE MWENYEWE) DHIDI YA WATU WOTE WASIO NA MAPENZI YA DHATI NA NDOA YAO. Na mke pia amlinde mume wake "Yeremia 31:22 22Utatangatanga hata lini, Ee binti usiye mwaminifu?
BWANA ameumba kitu kipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.’’ na kama kuna dosari zozote basi wasuluhishe kwa upendo (ref. para. 2 above) na msilundike chuki mioyoni mwenu kwa kuwa ikikomaa itasababisha ugumu wa msamaha. "SURAT AN-NISAAI 35. Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari."

Kwa ufupi mume awe na msimamo thabiti kuhakikisha kwamna hakuna migogoro inayoletwa kutoka nje ya ndoa yao mf. from mawifi, mashem na wazazi, kwa kuwa yeye ni mke wake mwenyewe na si mke wa mawifi, mashem and wakwe. Ni bora kuweka msimamo mapema na nadhani ni vema kusimama upande wa mkeo mbele za mawifi, wakweze na mashem hata kama amekosea ila ukiridhia mkeo amekosea ukamuonyee chumbani ili usiwape vichwa watu wa nje kwa kukosea kwa mkeo.

MWISHO: NAFASI YA MKE KTK NYUMBA.
Ndugu zangu wana JF, najua wengi wetu tunamwamini Mwenyezi Mungu, tusome vema vitabu vyake vitakatifu; maana hakika ndoa nyingi hukosa amani kwa sababu za Kibeijin confrence (naongelea usawa wa mume na mke as per Beijin declaration). Jamani tusipoenda sawa sawa na mafundisho ya dini amani kwa kweli haitakuwepo. MUME ANAHITAJI JAMBO MOJA KUBWA KUTOKA KWA MKEWE, "UTII" NA MUME ANATAKIWA AMPENDE MKEWE. (WAEFESO 5:22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa Lake." JE WANA JF KAMA KANUNI HII IKITUMIKA KULIKO YA BEIJIN CONFERENCE NI IPI ITALETA AMANI NA UPENDO NDANI YA NDO??????????????

MWANAMUME AMEUMBWA MTAWALA NA MKE KUWA MSAIDIZI (MWANZA 3:16 Kwa mwanamke akasema, “..............tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" PIA (MWANZO 2:20B Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 21Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.".

KWA LEO HUO NDIO MCHANGO WANGU NA YAPO MENGI NA MENGI AMBAYO NINGEWEZA KUYAELEZA JAMANI ILA MUDA WA KUFANYA REF. ILA USHAURI WANGU KWA WANA JF TUSOME SANA VITABU VYA MWENYEZI MUNGU MAANA MLE KUNAHEKIMA KUBWA NA AMANI NA UPENDO NA KANUNI ZOTE ZA MAISHA ZAPATIKANA HUMO.
 
Mkiwa kwenye ndoa tayari ni mwili mmoja, hivyo hata mke ana nafasi ya kuwaambia hao mawifi zake juu ya yale ambayo ni kero kwake, mambo ya kumtegemea mme tu ndo atoe sauti, huo tayari ni ubaguzi wa kindugu unakuwa ukifanyika.
 
BWANA ameumba kitu kipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.'' na kama kuna dosari zozote basi wasuluhishe kwa upendo (ref. para. 2 above) na msilundike chuki mioyoni mwenu kwa kuwa ikikomaa itasababisha ugumu wa msamaha. "SURAT AN-NISAAI 35. Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari."

Kwa ufupi mume awe na msimamo thabiti kuhakikisha kwamna hakuna migogoro inayoletwa kutoka nje ya ndoa yao mf. from mawifi, mashem na wazazi, kwa kuwa yeye ni mke wake mwenyewe na si mke wa mawifi, mashem and wakwe. Ni bora kuweka msimamo mapema na nadhani ni vema kusimama upande wa mkeo mbele za mawifi, wakweze na mashem hata kama amekosea ila ukiridhia mkeo amekosea ukamuonyee chumbani ili usiwape vichwa watu wa nje kwa kukosea kwa mkeo.

MWISHO: NAFASI YA MKE KTK NYUMBA.
Ndugu zangu wana JF, najua wengi wetu tunamwamini Mwenyezi Mungu, tusome vema vitabu vyake vitakatifu; maana hakika ndoa nyingi hukosa amani kwa sababu za Kibeijin confrence (naongelea usawa wa mume na mke as per Beijin declaration). Jamani tusipoenda sawa sawa na mafundisho ya dini amani kwa kweli haitakuwepo. MUME ANAHITAJI JAMBO MOJA KUBWA KUTOKA KWA MKEWE, "UTII" NA MUME ANATAKIWA AMPENDE MKEWE. (WAEFESO 5:22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa Lake." JE WANA JF KAMA KANUNI HII IKITUMIKA KULIKO YA BEIJIN CONFERENCE NI IPI ITALETA AMANI NA UPENDO NDANI YA NDO??????????????

MWANAMUME AMEUMBWA MTAWALA NA MKE KUWA MSAIDIZI (MWANZA 3:16 Kwa mwanamke akasema, "..............tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" PIA (MWANZO 2:20B Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 21Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.".

KWA LEO HUO NDIO MCHANGO WANGU NA YAPO MENGI NA MENGI AMBAYO NINGEWEZA KUYAELEZA JAMANI ILA MUDA WA KUFANYA REF. ILA USHAURI WANGU KWA WANA JF TUSOME SANA VITABU VYA MWENYEZI MUNGU MAANA MLE KUNAHEKIMA KUBWA NA AMANI NA UPENDO NA KANUNI ZOTE ZA MAISHA ZAPATIKANA HUMO.

Really?

Umeandika

Sasa kama mwanamke kaumbwa ili atawaliwe na mwanamme, na mwanamme hana tatizo na familia yake kumuingilia katika ndoa kuna ubaya gani hapo? Si mwanamme anamtawala mwanamke?

Mitazamo ya kidini kama hii inayojifanya kuuma na kupuliza ndiyo kichocheo cha matatizo, si solution.

We ushamwambia mwanamme yeye ndiye kichwa cha nyumba, na mwanamke kaumbwa ili kumsaidia yeye. Huu si ndio mfumodume wenyewe ninaoupinga huu?

Sasa mwanamme akishaambiwa na vitabu vya dini kwamba yeye ndiye kichwa cha familia na mwanamke ni msaidizi wake tu (sio equal) ataona shida gani kumfunga mdomo mwanamke ikiwa mwanamke atanyanyaswa na mawifi?
 
Mambo ya ndoa ni magumu saana. Na thou hayana formulae, kuna yale ambayo ni ya Msingi ambayo wanandoa yatakiwa kuzingatia ili kuweka nyumba iwe sawa.

Mwanaume mara nyiiiiingi hubebeshwa mzigo mkubwa na Mke na ndugu zake iwe wake kwa waume. Naamini sometimes ni ngumu kua Mume na kaka na mtoto wa mama at the same time. Mie hua hata nashangaa kua Mtu asema ampenda mumewe... Lakini kutwa kupeleka lawama kwa mumewe kuhusu ndugu zake kua wamnyanyasa.... Wewe kama mke what do you expect? As much as ni mume inabidi mke atumie busara saana kuweza mhandle mume pamoja na wifi zake. Wanawake (hasa) ndio husahau kua huyo mwanaume apenda dada/mama zake na Mke pia mapenzi yana nafasi yake; Kutwa kutaka shindana nani bora kwa huyo mwanaume (mke/dada/mama) Kinachotakiwa ni kua Mke atambue kua yeye ana nafasi kubwa hio ndoa na mumewe kuishi kwa Amani.

Nimependa Kongosho alivoongea.... Hii Vita ya kua haki sawa kwa mume na mke.... Hii ndo inavunja ndoa nyiingi siku hizi! Kweli haki ni muhimu BUT nashauri wanawake wenzangu watambue kua kuna vitu ambavo mwanamke hata agombee iwe haki sawa havitakua achieved no matter what! Sijui what the future holds ila kwa sasa ukweli ndio huo.... nimegusia hata katika mada ya Mbu juzi (Ndoa za sasa Vs za zamani). HAIWEZEKANI Mke na Mume waweke haki sawa ndani ya ndoa na eti ikadumu. Ni lazima mmoja awe chini kidogo.... Kumpa huyo mwanaume nafasi ya maamuzi ya Msingi (na kua na hio sauti ndani ya nyumba kwa maamuzi ya msing).

Mwanaume kumwambia kua amwambie mkewe awavumilie ndugu zake AMA awaambie dada zake wavumilie wifi yao ni kum’weka katika nafasi ngumu saana; For kila pande (Mke/Dada) itaona kama vile huyo Mume/kaka kadharau upande wake. Dawa ya kuepusha hayo.... Mke awasome wifi/Mama mkwe (kama kweli hataki mumewe kukeraika) na a deal nao Women to Women! In the long run kwa msimamo huo heshima itakuja tu! Mradi usi deal nao kwa dharau hata siku moja bali kwa heshima na kufuata haki na kuwaambia ukweli.

Kikubwa katika ndoa Mwanaume aelewe nafasi yake na Mke aelewe na kukubali nafasi ya mume (and Vice versa applies) hapo walau kuna kua na amani.

...LIKE, Mungu akubariki 2012 uwe mshaur mwema kwa other pple na Ndoa yako idumu MILELE. Amen
 
JAMANI JAMANI JF MEMBERS!!!

Ukweli utabakia kuwa maswala ya ndoa yanahitaji hekima ya hali ya juu sana. Na hekima hii kwa ninavyojua na kuamini hupatikana katika vitabu vya Mwenyezi Mungu (both Qur-an and Bible).

Niaze tu kwa kusema kwamba kasoro zozote zinazojitokeza katika ndoa na kuanza kuchunguza kasoro za mume au mke KWA MADHUMUNI MABAYA (yasiyo ya kujenga bali kuvuruga) ni dalili tosha ya kwamba aidha UPENDO UMEPOA au UMEISHA KABISA. Kwa kuwa kimsingi hakuna mtu yeyote duniani aliye kamili/mtimilifu yaani ''NO BODY PERFECT" Lakini kama mtu akikosea (mke au mume) basi yapendeza kurejeshana kwa upendo (KWA NIA YA KUJENGA(NA) (KI)UPENDO) na si kwa chuki wala kubomoa sawa na neno la Mungu katika Biblia "Ndugu zangu, kama mtu akipatikana na dhambi fulani, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejezeni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa. 2Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Kristo. Wagalatia 6:1-2" na katika Quran "SURAT ASH-SHUURA 40. ...Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu." KWA HIYO KUSAMEHEANA NI JAMBO MUHIMU SANA KATIKA NDOA.

PIA "Kuchukiana huondokesha fitina, bali kupendana husitiri makosa yote. Mithali 10:12" Kwa hiyo mwanzo wa chuki na kutokusameheana ni kwamba upendo umeisha. Kwa wanandoa hawana budi kutafuta source ya tatizo.

MIGOGORO NDANI YA NDOA KUTOKA KWA WAKWE, MAWIFI NA MASHEMEJI.
Katika hili mume anatakiwa kujua kwamba mke wake ni mke wake na tena ni ubavu wake mwenyewe i.e mke wake ni yeye mwenyewe, na YAMPASA AMLINDE MKE WAKE (AJILINDE MWENYEWE) DHIDI YA WATU WOTE WASIO NA MAPENZI YA DHATI NA NDOA YAO. Na mke pia amlinde mume wake "Yeremia 31:22 22Utatangatanga hata lini, Ee binti usiye mwaminifu?
BWANA ameumba kitu kipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.’’ na kama kuna dosari zozote basi wasuluhishe kwa upendo (ref. para. 2 above) na msilundike chuki mioyoni mwenu kwa kuwa ikikomaa itasababisha ugumu wa msamaha. "SURAT AN-NISAAI 35. Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari."

Kwa ufupi mume awe na msimamo thabiti kuhakikisha kwamna hakuna migogoro inayoletwa kutoka nje ya ndoa yao mf. from mawifi, mashem na wazazi, kwa kuwa yeye ni mke wake mwenyewe na si mke wa mawifi, mashem and wakwe. Ni bora kuweka msimamo mapema na nadhani ni vema kusimama upande wa mkeo mbele za mawifi, wakweze na mashem hata kama amekosea ila ukiridhia mkeo amekosea ukamuonyee chumbani ili usiwape vichwa watu wa nje kwa kukosea kwa mkeo.

MWISHO: NAFASI YA MKE KTK NYUMBA.
Ndugu zangu wana JF, najua wengi wetu tunamwamini Mwenyezi Mungu, tusome vema vitabu vyake vitakatifu; maana hakika ndoa nyingi hukosa amani kwa sababu za Kibeijin confrence (naongelea usawa wa mume na mke as per Beijin declaration). Jamani tusipoenda sawa sawa na mafundisho ya dini amani kwa kweli haitakuwepo. MUME ANAHITAJI JAMBO MOJA KUBWA KUTOKA KWA MKEWE, "UTII" NA MUME ANATAKIWA AMPENDE MKEWE. (WAEFESO 5:22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa Lake." JE WANA JF KAMA KANUNI HII IKITUMIKA KULIKO YA BEIJIN CONFERENCE NI IPI ITALETA AMANI NA UPENDO NDANI YA NDO??????????????

MWANAMUME AMEUMBWA MTAWALA NA MKE KUWA MSAIDIZI (MWANZA 3:16 Kwa mwanamke akasema, “..............tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" PIA (MWANZO 2:20B Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 21Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.".

KWA LEO HUO NDIO MCHANGO WANGU NA YAPO MENGI NA MENGI AMBAYO NINGEWEZA KUYAELEZA JAMANI ILA MUDA WA KUFANYA REF. ILA USHAURI WANGU KWA WANA JF TUSOME SANA VITABU VYA MWENYEZI MUNGU MAANA MLE KUNAHEKIMA KUBWA NA AMANI NA UPENDO NA KANUNI ZOTE ZA MAISHA ZAPATIKANA HUMO.

Nimeipenda kijana, ukweli mwing umetueleza. God blec u
 
Mkiwa kwenye ndoa tayari ni mwili mmoja, hivyo hata mke ana nafasi ya kuwaambia hao mawifi zake juu ya yale ambayo ni kero kwake, mambo ya kumtegemea mme tu ndo atoe sauti, huo tayari ni ubaguzi wa kindugu unakuwa ukifanyika.

Huwezi kuwaacha watu wasioelewana kabisa wamalizane wenyewe, labda kama unataka ugomvi wao ukue.
 
Back
Top Bottom