Nafasi ya mume. . .

Hiyo ya kugeuza watoto vijakazi haijakaa sawa. Sema ndio hivyo kukaa kwa mtu kazi, inabidi ufanye tu.

Inaweza kuwa ni kazi ndogo......fine, lakini it is not a guarantee kuwa yeye asifanye kwa sababu kuna watoto! Ebu fikiria, umeamka saa 5 umekuta mama mkwe kapika chai unakunywa! Badala ujifulie basi na wewe vijiguo vyako, ila unaloweka then huyoo unakula misele unasubiria flani aje akufulie.......kumbuka hapo hujihusishi na kazi nyingine ile!! Ukikuta nguo hazijafuliwa unaanza kulalamika na kusingizia kuwa ni flani alimkataza kumbe walaa ukute hata dogo hakuwepo au alichelewa kurudi!! Basi we unachukulia hasira tu, ukimsingizia kakondoo wala hana shida kabisa nakuelewesha tu lawama zikizidi sana nakuacha tu au namwambia mumeo atajua mwenyewe lakufanya!!
 
kweli aisee, maisha yanataka ukishaoa uachane na utaratibu wako wa zamani hasa usiompendeza mkeo, kama marafiki, ndugu, jamaa wote hawatakiwi kukufata fata wala wewe kuwafata fata. Unatakiwa kuchukulia ulimwenguni kama mmebaki nyie wawili tu. Eti eeh?

Kuachana na utaratibu sio ishu, kubadili ndio ishu. Huwezi kua na mke nyumbani alafu kila siku uko night club unaomba kila msichana namba kama bachela. Huwezi kua na mke nyumbani ukaishia kufanya maamuzi na ndugu zako ama kufanya wanayotaka wao bila kumshirikisha mke au kuzingatia hali yenu ilivyo.

Hayo ya muwe kama mmebaki wawili ni exaggeration, na mtu mwenye mawazo ya aina hiyo hata kama ndugu yake anasaidia kiasi gani, siku moja tu akisema hapana kwasababu mke wangu kasema hivi basi atasahau mazuri yote na kuaza kushutumu wametupwa,kaka hawajali, mke katake over akili yake na mengine kama hayo. Ndio mwanzo wa chuki zisizo na maana.
 
Inaweza kuwa ni kazi ndogo......fine, lakini it is not a guarantee kuwa yeye asifanye kwa sababu kuna watoto! Ebu fikiria, umeamka saa 5 umekuta mama mkwe kapika chai unakunywa! Badala ujifulie basi na wewe vijiguo vyako, ila unaloweka then huyoo unakula misele unasubiria flani aje akufulie.......kumbuka hapo hujihusishi na kazi nyingine ile!! Ukikuta nguo hazijafuliwa unaanza kulalamika na kusingizia kuwa ni flani alimkataza kumbe walaa ukute hata dogo hakuwepo au alichelewa kurudi!! Basi we unachukulia hasira tu, ukimsingizia kakondoo wala hana shida kabisa nakuelewesha tu lawama zikizidi sana nakuacha tu au namwambia mumeo atajua mwenyewe lakufanya!!
Huyo sasa kazidi, au alidhani kukaa kwa wakwe ni sawa na kukaa hotelini?
 
Mara nyingi huwa ni hulka tu maana unakuta wengine pamoja na kuwa na kazi zao nzuri na kuwa na maisha yao binafsi bado tu ataanza kumuandama mke wa kaka yake mara hivi mara vile mimi nafikiri hakuna sababu ya msingi sana zaidi ya kuwa ni hulka waliyonayo baadhi ya wanawake kuona kuwa kaka zao hawawezi kutunzwa vizuri na mwanamke mwingine ili hali uamuzi wa kuoa aliyeuchukua ni mwanaume na mwanaume akiendekeza hiki kitu ndio hapo mfarakano kwenye ndoa unaanza na mwanamke naye akiwa legelege ndio kabisa atapelekeshwa puta mpaka basi.

Maana hawa mawifi wakigundua weakness ya kaka yao ni wapi ndio hapo hapo wanapo hit na kumfanya mwanamke aliyeolewa kuonekana anashindwa kumudu ndoa yake kitu ambacho kinawapa nafasi mawifi kuonekana wao ndio wao binafsi kwangu mimi ndoa ni baina ya mwanamke na mwanaume ukiishaanza kuwa-entertain mawifi it will cost you big time..

Nakubaliana nawe kabisaaaa, ni hulka na ROHO MBAYA za kike tu... kwa sababu ukichunguza ni mara chache sana kuna kuwaga na bifu kati ya mwanamke na shemeji zake. Cha msingi ni kuwapotezea tu kila mtu awe na maisha yake but hili linawezekana kama mume ni mwelewa.
 
Kuachana na utaratibu sio ishu, kubadili ndio ishu..

kubadili aje hapo? Kama ulikuwa unaenda club kila siku (refer mfano wako) kwahiyo kubadili utaratibu awe anaenda mara moja moja au? Kama mkewe hapendi hata hiyo mara moja afanyeje? Kama mwanaume alikuwa anawashirikisha ndugu kwenye maamuzi, kwenye kubadilika unamaanisha asiwashirikishe tena akishao au awashirikishe nusu nusu. Kama asipowashirikisha hapo utasema amebadili utaratibu au ameacha?
 
ukitaka kujua wanawake ni viumbe vya ajabu ni hapo kwenye ugomvi wa mke na mawifi....
kila ambacho watapinga unachomfanyia mkeo ndio wao wataenda kukidai kwa waume zao....
hivi viumbe hivi lol

Walahi tena... ni wivu tuuu... wanaona kuna wanavyovikosa toka kwa waume zao na kaka yao anatoa kwa wife wanakuja kufukuzia l.o.l. Mbaya zaidi methodology zinazotumika ili wapate hiyo huduma ndo za kijinga kwani ni mpaka mgombane? Binafsi Na wa HATE sana hawa viumbee.. Ngoja niishie hapo tu maana wamo humu humu l.o.l
 
kubadili aje hapo? Kama ulikuwa unaenda club kila siku (refer mfano wako) kwahiyo kubadili utaratibu awe anaenda mara moja moja au? Kama mkewe hapendi hata hiyo mara moja afanyeje? Kama mwanaume alikuwa anawashirikisha ndugu kwenye maamuzi, kwenye kubadilika unamaanisha asiwashirikishe tena akishao au awashirikishe nusu nusu. Kama asipowashirikisha hapo utasema amebadili utaratibu au ameacha?

Naona sasa tunataka kuhamia kwenye malumbano ya lugha badala ya malumbano ya hoja.

Nwy, kawaida ni ngumu mtu kuacha kabisa mambo aliyozoea hivyo anatakiwa kupunguza ila kama anaweza kuacha na inamfaa yeye na mwenzi wake that's just as well. Mume hawezi kuacha kila anachopenda kumfurahisha mke (na kinyume cha hapo) , that's asking for too much.Muhimu ni kukutana katikati, kila mmoja anajitoa kwa mwenzake. Badala ya kuparty wiki nzima, anatoka weekend, badala ya kurudi nyumbani saa sita usiku kama alivyozoea anarudi saa mbili.

Kuhusu kuwashirikisha ndugu hilo haliwezi kuachwa kabisa kwasababu kuna mambo ambayo yatakua yanawagusa moja kwa moja (misiba kwenye ukoo,mali za ukoo n.k) hivyo ni muhimu nao wakawa na sauti. Ila huwezi kutegemea dada na mama wa mume ndio wamchagulie godoro tena, rangi ya sofa, carpet la sebleni, kiasi gani aweke akiba and the likes. Yani kuna maamuzi ambayo yanabadilika na kua ya mume na mke tu badala ya kijana kuwashirikisha ndugu zake kwasababu pale kwa kaka yao tu bali ni kwa kaka na mkewe. Hivyo maamuzi ya kule ndani ni yao na sio ya dada zake au hata dada wa mke. Wanaweza kushauri wakiombwa na sio kulazimisha kuwa sehemu ya
maamuzi.
 
Huyo sasa kazidi, au alidhani kukaa kwa wakwe ni sawa na kukaa hotelini?

Sometimes na mumewe nae anamuendekeza, kuna kipindi nilipomaliza form 6 nilipoenda nyumbani nikakuta huwa hajumuiki na wenzie, sosi likiandaliwa mezani dada wakazi anamuwekea chakula chake anampelekea ndani kwake ndo anaenda kula mwenyewe hata kama mumewe hayupo!! Mwanzoni nilidhani labda ni mila nami nikaendeleza system, tunakula ye amekaa pembeni tu ila baadae ndo anaingia ndani kwake anaoga alafu anakula. Mi sikufurahia, nikamuuliza mama au ni mwiko? Nikajibiwa sio ila ndivo alivo, sikumuuliza yeye wala mumewe! Nikawasubiria wako pamoja nikawachana live, hahah nikasikia mume anamuuliza mkewe, 'eti mbona huwa hukai na wenzio'?? Khaa mie baada ya kuwasilisha ujumbe nikiondoka ila nashukuru baadae hako katabia kaliisha!!!
 
Uko sawa BAK. Lakini uki-entertain maneno yanaendelea kuja. Kuna wake pia nao wana tabia ya kuwafuatilia wifi zao, kama kakako kakupa sh ngapi etc. Mi nadhani ni malezi na life style, usipoendekeza hayakupati. 'usilete ufundi kwa mwenzio, ngoja upate nafasi uwe na kwako tuje tukuone', period! Usi-comment any observation ya kwa ndugu,kaka wala rafiki!

Ni kweli kabisa King'asti na ndio maana nilikubalina na Queen Lizzy kwamba anayepaswa kuongea na hao mawifi ni kaka yao na si mke wa kaka yao ili kuhakikisha kwamba hivyo vijimanenomaneno vya wifi hivi wifi vile vinaisha mara moja ili kuondoa kabisa uwezekano wa tatizo kuwa kubwa zaidi.
 
huu uzi uko poa sana, ngoja nikalale ntarudi tena kesho.. G9t peoples
 
"....damu nzito kuliko,....!"
uchungu wa mwana...

..acheni madada waendelee kuwatetea kaka zao bana,
wake wengine ni wanyanyasaji banaa...hahaha..

...Mkuu Mbu uyasemayo ni kweli lakini madada wengine hata wakilambwa miguu na wake za kaka zao hawaridhiki hata kidogo!!! lazima tu wahakikishe wanaanzisha sokomoko ili kuondoa furaha ndani ya nyumba. Kaka yao ni mtu mzima ana uwezo wa kuchanganua baya na zuri kama haoni shida kwa mkewe kuamka saa tano, nguo zao kufuliwa na HG, vyakula vyao vyote kuanzia asubuhi hadi jioni kupikwa na HG kuna tatizo gani la kumfanya dada wa kaka akose raha na kutaka kuingilia maisha ambayo hayamuhusu!!!!?
 
Yaani BAK,I wish ungekuwa tu karibu....lol... sina hata la kuongeza kwenye hii mada,umezungumza yote!! Midada mingine inawafanya kaka zao kama wenyewe hawana uwezo wa kupima wanayotendewa,kila kitu wao lazima waweke pua zao na hata umtunzeje ndugu yao wao wanafikiri wangeweza kufanya zaidi ya mke...inatesa sana!
 
Mhhhh! lol! :photo::):)
 
...Mkuu Mbu uyasemayo ni kweli lakini madada wengine hata wakilambwa miguu na wake za kaka zao hawaridhiki hata kidogo!!! lazima tu wahakikishe wanaanzisha sokomoko ili kuondoa furaha ndani ya nyumba. Kaka yao ni mtu mzima ana uwezo wa kuchanganua baya na zuri kama haoni shida kwa mkewe kuamka saa tano, nguo zao kufuliwa na HG, vyakula vyao vyote kuanzia asubuhi hadi jioni kupikwa na HG kuna tatizo gani la kumfanya dada wa kaka akose raha na kutaka kuingilia maisha ambayo hayamuhusu!!!!?

Wivu tu hua unawasumbua.
Wifi anapata hiki, anapata kile na wao wanataka. Wengine basi tu hawaoni raha kuona mwanamke mwingine ana furaha.
 
Eti anachekelea. . ..
Ngoja nimsaidie dearest kumalizia. . . angekufinya ili ahakikishe haoti kwamba kuna wanaume wenye mawazo kama yako.Lolz

he he he he dearest, naona aibu sasa...sikutaka kusema direct hivyo,now he knows...i wish...lol
 
he he he he dearest, naona aibu sasa...sikutaka kusema direct hivyo,now he knows...i wish...lol

Hehehehe. . . dearest nimeona nimwambie ajue maana alishadhani eti unamtokea kisirisiri.Lolzz. . . .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mimi kama kaka yako Husninyo nakujibu
mke wangu lazima 'ajimwage mwage nyumbani' kwake kama wewe unaona dharau tafuta nyumba yako...

na kama unaishi nyumbani kwangu ambako mke wangu ndie malkia wa nyumba
lazima habari zako zote azijue,usije kupewa mimba ukashindwa kusoma nikapoteza pesa nazotumia kukusomesha...

misiba na wagonjwa hawezi kwenda bila mimi kumruhusu....so sio kosa lake
na sio kila msiba unakwenda.....utaenda misiba mingapi mjini hapa....?.

ni lazima ajioneshe ili awaoneshe wale waliosema 'ningeshindwa kumtunza na kumpa furaha' how wrong walikosea
so muache aringe na kujionesha ni haki yake

na kuhusu nyinyi dada zangu kuja nyumbani..
hiyo ndo chanzo cha umbea na majungu....mimi mwenyewe sitaki...
mkiwa na shida mnifuate oficin....mke wangu ana haki ya kulala mmchana na kutazama tamthilia bila bughudha
na nyinyi mna haki hizo majumbani mwenu sawa????

so now umenisikia.......i hope utanielewa...

Nimeipenda saana The Boss.
Hivyo ndivyo inavyotakiwa wanaume kusimamia ndoa zao dhidi ya ndugu wabomoaji.
 
Back
Top Bottom