Nafasi ya muamuzi katika mashindano!

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
"Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu"
Mithali 18:18

Mara nyingi kumekuwa na kawaida kwa vyama vikuu vya pinzani na Chama kinachotawala kuvutana na kutokukubaliana kabla au baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, iwe Tanzania bara au Tanzania visiwani.

Mara zote hizi lawama zimeelekezwa kwa refa/msimamiaji wa uchaguzi kuwa anaegemea upande wa watawala, sababu ya wanaamini hivyo ni ule muonekano wa time inayosimamia uchaguzi.
Yaani M'kiti, makamishna wa time wanateuliwa na Rais na hapo Rais huyo huyo au mwenzake wa Chama chake akaingia kwenye mashindano.

Ni Kama Simba inacheza na Yanga halafu refa achaguliwe na M'kiti wa Yanga. Kwa akili ya kawaida Simba haiwezi kutoboa hata iweje. Moja wa wasaidizi wa refa awe Manara.

Time ya Uchaguzi sio tu inaaswa kuwa huru Bali ionekane kuwa iko huru na hapo ndipo shida ilipo. Yaani vyama vinavyogombea visishawishiwe kuwa time iko huru Bali kwa macho yao wwnyewe waone na kuthibitisha kuwa time hiyo iko huru.

Kivipi?

Sisi Kama wananchi wapenda Amani, tunashauri mabadiliko ya muundo wa Tume kabla ya Uchaguzi 2025.

Endapo mchakato wa katiba mpya hautaweza kukamilika kabla ya 2025 basi Kuna haja ya kuunda tume ya KUPITIA MAPUNGUFU YA TUME ILIYOPO NA KUUNDA TUME HURU MPYA itakayoshirikisha wadau wote muhimu, viongozi wa dini,vyama vya siasa, asasi zisizo za kiserikali, wabobezi wa Sheria na katiba bila kuwasahau... Jenetali Ulimwengu, mama Helen Kijo Bisimba, Pro Mwandosya, Askofu Benson Bagonza, Jaji Warioba, Mzee Butiku, Ismail Jusa na Tundu Lissu (Lissu na Jussa kama WANASHERIA ngawa na WANASIASA pia)

Tulimalize hili na maisha yasonge mbele.
Nchi hii tuopendayo yetu sote, tuipende na tupendane bila kujali uCCM , U CHADEMA, u ACT,. u NCCR hata u CUF. SOTE NI WATANZANIA.
HAKUNA MWENYE HATI MILIKI ZAIDI YA MWINGINE. TUIJENGE!
 
Back
Top Bottom