Nafasi ya mitandao ya kijamii katika kulinda maslahi/nafasi ya Kiraia na kuwajibisha viongozi

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20210402_114057_707.jpg

Nini maana ya nafasi ya kiraia?

Nafasi ya kiraia imeundwa na seti ya sheria zinazokubalika ulimwenguni, ambazo huruhusu watu kujipanga, kushiriki na kuwasiliana kwa uhuru na bila kizuizi mawazo yao, na kwa kufanya hivyo, wanaathiri miundo ya kisiasa na kijamii inayowazunguka.

Nafasi ya mitandao ya kijamii katika kulinda haki ya raia

Mitandao ya kijamii kama Twitter, Telegram, Instagram, Facebook, WhatsApp n.k imesaidia kwa kiasi fulani kukuza haki ya raia ya kujieleza

Mtandao wa Twitter unaongoza kwa majadiliano ya kisiasa, kijamii na maendeleo. Wanasiasa pia wamekuwa wakitumia zaidi jukwaa hili kuwasilisha maoni na maendeleo ya majukumu yao kwa wananchi, na wananchi wanatumia nafasi hii kuwawajibisha viongozi wao pale wanapokosea

Majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa kiasi fulani yamekuza uhuru wa kujielezea. Yamekuwa ndio madaraja ya raia kuelezea hisia zao kwa viongozi wao, na hata wafanyakazi wa umma.

Mitandao hii pia hutumiwa na asasi za kiraia zinazotetea haki za raia, kufikisha ujumbe kwa wahusika.

Hashtag mbalimbali zinaanzishwa kwa leo la kutetea haki za raia. Kwa umoja raia hutetea kwa pamoja haki zao pale zinapokuwa zinakandamizwa.

Mitandao ya kijamii imetengeneza mazingira ya wananchi kuwasilisha kero zao kwa wakati, mfano, kero maji, umeme, barabara n.k. Hii imefanya viongozi na mashirika mbalimbali kupokea kero za raia kupitia majukwaa hayo.

Nchini Tanzania kuna matokeo ya mambo mbalimbali yanayotokana na hatua ya kuwasilishwa mtandaoni. Baadhi ya viongozi huchukua maoni mtandaoni kwa kujadiliana nao na kubadilishana mawazo, baadhi kuchukua kero hizo kimya kimya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom