Nafasi ya Makamu wa Rais Ifutwe

Nafasi ya Makamu wa Rais Ifutwe

Hata huu muungano ufutwe maana si muungano ni uvamizi na ndio yakazuka haya mambo ya makamo wa Raisi.

Wazanzibari hawautaki muungano ni nguvu ya jeshi tu ndiyo inayotumika pamoja na umafia wa CCM na kanisa katoliki
Kwa nini na nyie zanzibar msitumie nguvu ya jeshi kuvunja muungano
 
Yan ht wife ambae co mfuatiliaji wa mambo ya politiki amenambia kitu hicho, aliniuiliza hivi kazi ya makamu wa raisi ni ipi mbn namuona huyu mama yy kila siku ni kufungua makongamano, maonesho, majengo nk..... mm naweza sema ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma!
Kweli aisee
 
Makamu wa Rais huchukua u-Rais pale Rais anapokutwa na mauti.
U mauti ni lazima na ni amri ya Mwenyezimungu ....itokeapo hilo Makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais kumalizia kipindi kilichobakia au ataapishwa kuwa Rais kwa miaka mitano...??
Makamu amechaguliwa kwa nafasi hiyo sasa inakuwaje awe Rais...???
 
Huapishwa na kuwa Rais ili kumalizia kipindi kilichosalia. (Kwa mujibu wa Katiba yetu)
 
Kwa muungano wetu huu wa kimagumashi sanaa......VP lazima awepo!! Kuimarisha muungano wetu wa kimagumashi
 
Makamu wa Rais huchukua u-Rais pale Rais anapokutwa na mauti.
exactly hawa jui kazi yake vizuri pale ndo ndo utamuona kazi yake anavyo chapa.yaya anakua kivuli tuh kwasasa nasio kwamba afanyi kazi mbona makamu wote ndo hivyo hivyo. ila hafe raisi ndo utamsikia saaana
 
Salaam,
Natambua kwamba nafasi ya Makamu wa Rais imetajwa katika Sehemu ya Pill ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 47(1) nanukuu Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye ndiye atakuwa msaidizi mkuu wa rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla na hususani.

a) atamsaidia rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hats siku za mambo ya Muungano
b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na rais
c) atafanya kazi zote za rais kama rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.Mwisho wa kunukuu

Tangu tuanze kuwa na makamu wa rais asiye rais wa Zanzibar pia, nafasi hiyo imekuwa mama ya kuwafurahisha watu wa Zanzibar, haina nguvu wala mvuto. Waziri Mkuu anaonekana kama anamsaidia rais vizuri na kwa ufanisi zaidi kuliko makamu wake, Ana sauti, nguvu na mamlaka.

Akitoa maagizo yanafuatwa. Kuna haja gani tena ya kuwa na makamu wa rais? Ni matumizi mabaya ya rasilimali, tunapoteza fedha. Naona ofisi ya makamu wa rais ina waziri anayeshughulika na Muungano na Mazingira.

Mazingira ni active zaidi kuliko muungano. Makamu wa Rais ni kama anapuuzwa. Fikiria kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo,anagoma kutekeleza maagizo ya bosi wake kuhusu itifaki inakuwaje?

Nafasi hii napendekeza ifutwe. PM anatosha.
Usiseme Nafasi yeyote ifutwe Tanzania hii wapo akina Pole Pole walizunguka Nchi Nzima kwenye Vyombo Vya habari kusema wakuu wa wilaya wafutwe hawana kazi Lakini Alipopewa nafasi hiyo alisema yuko busy kutokana na mrundikano wa kazi.. bongo hiyo kaka.

Alikuja prof kitila alisema Rais aache kabisa kuteua watu kutoka Udsm Maana wanaupungufu wa wakufunzi alipiga kelele tukamwona mzalendo mwenye kutaka Elimu ya Vijana isonge mbele Alipoteuliwa wewe alitoa shukrani kubwa sana kwa Rais nakumwona Rais mtu makini sana kwa kumteua yeye... Ndo Bongo yetu hii

Leo wewe ukipewa 2020 uwe mgombea mwenza ili mkishinda uwe makamu wa Rais utazunguka Tanzania yote kuelezea utakachofanya ukipita wakati leo unaona haina maana hana kazi hahahahaha Wabongo Tunajuana Wenyewe.
 
Yan ht wife ambae co mfuatiliaji wa mambo ya politiki amenambia kitu hicho, aliniuiliza hivi kazi ya makamu wa raisi ni ipi mbn namuona huyu mama yy kila siku ni kufungua makongamano, maonesho, majengo nk..... mm naweza sema ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma!
Unatudanganya mkuu, unasema mkeo anasema kila siku anamuona kwenye............. Huyo ni mfuatiliaji wa kila siku.
 
Unatudanganya mkuu, unasema mkeo anasema kila siku anamuona kwenye............. Huyo ni mfuatiliaji wa kila siku.
Sawa labda nitumie neno kila anapobahatika kumuona ni either anazindua, anafunga/fungua kongamano, na mambo yanayofanana na hayo
 
Hivi kuna jambo au ushauri uliotolewa na huyu Makamu wa Rais ukapokelewa na huyu bosi wake? Naamini atamaliza kipindi chake huyu Mama bila ushauri wake kufanyiwa kazi. Anadharauliwa hata na mkuu wa mkoa sembuse bosi wake. Ataishia kufungua/kufunga makongamano, mikutano na kukata utepe tu.
 
Chadema visa sana!

Yaani Ofisi ya Makamu wa Rais ifutwe kwa kuwa Lema hajapewa Fursa ya kupiga Soga Msibani!

Ule Msiba wa Kitaifa uliitishwa na Serikali ya CCM na wao si waitishe Matanga ya Kitaifa waongee mpaka wachoke na wamnyime nafasi ya kuongea Mkuu wa Mkoa?
..yani ule msiba wa wanafunzi arusha ni CCM waliuitisha..??!! makubwa
 
Yan ht wife ambae co mfuatiliaji wa mambo ya politiki amenambia kitu hicho, aliniuiliza hivi kazi ya makamu wa raisi ni ipi mbn namuona huyu mama yy kila siku ni kufungua makongamano, maonesho, majengo nk..... mm naweza sema ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma!
mnakosea kaz ya uraisi ndo ifutwe
 
awamu hii tusingekuwa na waziri mkuu na huyu mama tanzania ingepotea kwenye ramani ya dunia ,,,,,,,,,,,,,,
huyu jamaa anaweza kutuchamba tu kuna mto ngono, sijui blablabla
unadhani anaweza kuongea nini international?
 
Chadema visa sana!

Yaani Ofisi ya Makamu wa Rais ifutwe kwa kuwa Lema hajapewa Fursa ya kupiga Soga Msibani!

Ule Msiba wa Kitaifa uliitishwa na Serikali ya CCM na wao si waitishe Matanga ya Kitaifa waongee mpaka wachoke na wamnyime nafasi ya kuongea Mkuu wa Mkoa?
Sikujua kama we jamaa ni mweupe namna hii !
 
Back
Top Bottom