Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,140
- 1,983
Salaam,
Natambua kwamba nafasi ya Makamu wa Rais imetajwa katika Sehemu ya Pill ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 47(1) nanukuu Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye ndiye atakuwa msaidizi mkuu wa rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla na hususani.
a) atamsaidia rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hats siku za mambo ya Muungano
b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na rais
c) atafanya kazi zote za rais kama rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.Mwisho wa kunukuu
Tangu tuanze kuwa na makamu wa rais asiye rais wa Zanzibar pia, nafasi hiyo imekuwa mama ya kuwafurahisha watu wa Zanzibar, haina nguvu wala mvuto. Waziri Mkuu anaonekana kama anamsaidia rais vizuri na kwa ufanisi zaidi kuliko makamu wake, Ana sauti, nguvu na mamlaka.
Akitoa maagizo yanafuatwa. Kuna haja gani tena ya kuwa na makamu wa rais? Ni matumizi mabaya ya rasilimali, tunapoteza fedha. Naona ofisi ya makamu wa rais ina waziri anayeshughulika na Muungano na Mazingira.
Mazingira ni active zaidi kuliko muungano. Makamu wa Rais ni kama anapuuzwa. Fikiria kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo,anagoma kutekeleza maagizo ya bosi wake kuhusu itifaki inakuwaje?
Nafasi hii napendekeza ifutwe. PM anatosha.