Nafasi ya mahakama ndani ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi ya mahakama ndani ya katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Bilionea Asigwa, Jun 11, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  Mahakama kama moja ya mihimili mitatu ya serikali ina nafasi sawa kikatiba kama ilivyo BUNGE na UTAWALA(EXECUTIVE). lakini hili halidhihiriki kama linavyotakiwa katika nchi yetu.Kitendo cha mahakama kuwa chini ya wizara ya sheria na katiba ni kuifanya iwe chini ya mhimili mwingine wa serikali ambao unasimamiwa na waziri mkuu na mawaziri wake.. Hoja yangu hapa si kupunguza uingiliaji wa rais katika uteuzi wa majaji ila ni kuiondoa mahakama chini ya wizara na kiufanya iwe huyu kama lilivyo bunge
  Bunge la jamhuri hii haliko chini ya wizara yoyote na wala hakuna waziri(na hata waziri mkuu) aliye na dhamana ya kuangalia uendeshaji wake wa siku kwa siku sasa iweje kwa mahakama iwe chini ya kiongozi wa kisiasa ambaye anatoka katika mhimili mwingine wa utawala
  Juzi juzi nilimsikia waziri wa sheria akiipa mahakama maagizo ya kuharakisha kesi za mahabusu ili kuwapa watu haki zao hasa wale ambao wanasota na vijikesi vyao havieleweki eleweki ,japo jambo hili si baya lakini kama waziri mbaye yuko chini ya waziri mkuu anaweza kutoa maagizo haya kwa mhimili mwingine inaonekana hata waziri mkuu wa nchi hii yuko juu ya mahakama japo katiba hailitamki hili wazi wazi

  MY OPINOIN

  moja ya mambo ya msingi ambayo wanasheria wa nchi hii wanabidi wayatolee maoni katika katiba mpya ni hli la kuiondoa mahakama chini ya wizara na kiwe chombo huru chenye government struture yake na jaji mkuu inabidi ndio awe TOP kama alivyo SPIKA katika bunge japo rais anweza kuendelea kuwa na mamlaka kama aliyo nayo
  Mimi si mwanasheria ila nadhani wanasheria wanaweza kulitolea hili ufafanuzi mzuri wa kina
  naomba kuwasilisha
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pia litazamwe kwa kina ktk mchakato huu wa katiba mpya.
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  Tanzania, mihimili ya dola imevurugwa. Mihimili inaingiliana, mmoja ukionekana supa kuliko mwingine. Kitendo cha mtu kuwa mubunge halafu waziri, hakikubaliki kwa dhana ya mihimili. Inatakiwa kila mutu awe independent ili waheshimiane.

  kwa hiyo naunga mkono kabisa kuwa, mihimili hii itenganishwe, mahakama ikae kivyao, bunge likae kivyao na serikali yaani mawaziri wakae kivyao, ili kila mtu awe na nguvu ya kumshughulikia mwenzke hasa pale anapofanya madudu.

  ilivyo sasa, mtu anachaguliwa kuwa mbunge(mhimili wa kwanza), huyo huyo anateuliwa kuwa waziri(mhimimili wa pili) na mbya zaidi anapewa kuwa kiongozi wa mhimili mwingine mfano mahakama. haya ni makosa makubwa.

  tena haikubaliki mkuu wa kaya kuwateua watu katika mihimili hii, wapatikane kwa mfumo members ndani ya mhimili watakao ona unafaa.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwa utaratibu wa sasa mahakama Kama taasisi haiwajiki kwa chombo chochote, kitu kinachofanya uhuru wake chini ya dhana ya uhuru wa mahakama usiwe na mipaka.

  Ni muhimu kuhakikisha kuwa taasisi ya mahakama inawajibika kwa wananchi.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nimependa wording za Katiba zifiatazo :

  Uganda: article 126: judicial power is derived from the people and shall be exercised bythe courts established under the constitution in the name ofthe people andin agreement with law, values and aspirations of the people.

  Kenya: article 159: judicial authority is derived from the people and vests in, and shall be exercised by, the courts and tribunals established by or under this constitution

  Mamlaka ya mahakama ikitoka kwa wananchi maana yake mahakama zitakuwa zinawajibika kwa wananchi.
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  ukiwasikiliza kwa kina wanasheria kitu ambacho wanakijadili ni madaraka ya raisi katika kuwateua majaji lakini hili wala hawalioni kama kikwazo kwao katika DHANA HALISI YA UHURU WA MAHAKAMA

  hata kama raisi hatateua majaji lakini kama bado mko chini ya wizara mtakua mnaathiriwa na uingiliaji wa EXECUTIVE party katika utendaji wa huu mhimili
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  hili ualolisema ni sahihi kabisa kwani mtu kama ni mwaziri wa sheria na kwa kawaida lazima apitie kwenye ujaji nafikiri automatically anakua anaingia kwenye mihimili yote mitatu..kama ishu ni interconnection nafikiri utaratibu kama ule wa kamti za bunge ni mzuri sana..kwamba mahakama iwe huru ila ziwepo kamati za mahakama ambazo zinaweza kuingiliana na mihimili mingine kama ni bunge au UTAWALA
   
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  suala la kuwajibika kwa wananchi sidhani kama ni la maana sana kwani hiki ni chombo kinacho simamia haki na sheria ambzo zipo.. kama mahakama itaweza kuwa inawajibika kwa wanachi basi mfumo wa kidemokrasia ambao dhana yake ni wengi wape hata kama wako wrong itaanza kujipenyeza katika hukumu
  kitu ambacho ni hatari sana kwa haki
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sijakuelewa, unaweza kufafanua!
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mfumo wa kidemokrasi unalazimisha wengi wapewe hata kama ni mataahira..kama ikitokea tukaamua kuanzia leo kula nyama ya mtu ruksa tunaweza kutunga sheria na tukaipitisha ikaruhusu ulaji huo

  unapowapa wanachi mamlaka ya kuiwajibisha mahakama si kitu kizuri sana hasa kisheria kwani mahakama inatakiwa isimamie haki hata kama ni ya mtu mmoja against the whole nation..na ikumbukwe pia sheria ni proffesional ambayo mtu anyeweza kuiwajibisha ni proffesional vilevile ambaye anao uwezo kuthibitisha kuwamisingi ya kitaaluma imekiukwa
  chukulia mfano LEMA alivyovuliwa ubunge pale arusha , kama mahakama ingekua inawajibika kwa wananchi moja kwa moja mahakama nzima ingepigwa chini na uteuzi mpya ungefanyika kitu ambacho ni hatari sana kwa utoaji wa haki
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Dhana ya mahakama kuwajibika kwa wananchi, haina maana ya raia mmoja kuiwajibisha mahakama, ni dhana pana mno ambayo inaifanya mahakama kutekeleza wajibu wake kwa misingi ya Katiba.

  Kwa mfano kuchelewa kuandika hukumu, huwezi kulalamika mahali hata Kama kesi yako iko pending kwa miaka kumi, kutopata nakala ya hukumu ni suala nyeti sana ambalo aghalabu watu wengi wanakosa haki kwa sababu hiyo. Lakini mahakama ikisema tunashindwa kukupa hukumu mwananchi utalalamika wapi? Kuna utaratibu wa kikatiba wa kufanya mahakama ziwajibike kwa wananchi.

  Mfanyakazi yoyote, ili apande Cheo au kuteremshwa cheo lazima afanyiwe assesment kila mwaka, kwa mfano kipimo cha utendaji kazi kwa mahakama zetu ni Nini? Kumaliza kesi nyingi, hakuna anayejua, kuachia watu wengi? Hakuna anayejua, kufunga watu wengi hakuna anayejua, kuandika hukumu nzuri? Haki na anayejua. Kuitetea serikali, kutetea wanaharakati?

  Hii ni dhana pana sana, ambayo mwisho wa yote inaleteeza uwajibikaji wa mahakama kwa wananchi.
   
Loading...