Nafasi ya mafunzo ya kazi.

bereng

bereng

Senior Member
114
170
Habari JF,
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Tuwafikie Tanzania Organisation inayojihusisha na maendeleo ya jamii katika elimu inatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu wa ujasiriamali kwa mkoa wa mwanza katika mradi wake wa WEZESHA MJASIRIAMALI unaoratibiwa na taasisi unaolenga kuwapatia elimu na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo kupata mtaji kiurahisi.
Lengo la mafunzo ni kuwaandaa wahitimu kuwa wahamasishaji wa mradi na waalimu wa ujasiriamali katika wilaya zote za mkoa wa mwanza.
Mafunzo yatakatolewa kwa siku 3 na baada ya hapo watapewa fomu za mkataba wa ajira na kupangwa wilaya husika kwa ajili ya kuanza kazi. Aidha watakuwa wakifanya kazi huku wakiendelea na mafunzo toka kwa wakufunzi ambao watakuwa wakiwatembelea katika wilaya husika kulingana na ratiba iliyopangwa.
Masomo yatakayotolewa kwa mara ya kwanza ni:-
-Kuutambulisha mradi wa W.M
-Ujasiriamali
-Uanzishaji na uendelezaji SACCOSS na VICOBA.
-Uanzishaji na uendelezaji wa NGO
-Uanzishaji wa kampuni za kibiashara.
-Utengenezaji wa bidhaa mbalimbali
Ada ya mafunzo ni tsh. 35,000/- tu fomu za kujiunga zinapatikana kwa tsh. 5,000/- tu. Zitatolewa na wawakilishi wetu wilayani.
Mafunzo yataanza rasmi tarehe 16 disemba 2013 na yatafanyikia mjini mwanza.
Kwa mawasino tuma email tuwafikiemwanza@gmail.com au piga simu kwa meneja wa mradi namba 0768955185.
 
S

Sharifa du Pont

Member
28
0
Vipi Dar es Salaam mafunzo hayo hakuna nayatamani sana jamani yakifika huku nifahamisheni kwa haraka
 

Forum statistics


Threads
1,424,934

Messages
35,076,363

Members
538,167
Top Bottom