Nafasi ya kutafsiri Video za mkutano wa TED kwenda Kiswahili

mzeemzima

Senior Member
Apr 14, 2010
122
78
Habari zenu wadau,

Kwa wale ambao hawalifahamu hili ni kwamba kuna mkutano ambao umekuwa maarufu sana duniani unaitwa TED(TED: Ideas worth spreading), mkutano huu unakusanya wataalamu wa kada mbalimbali kujadiliana kuhusu jinsi ya kutatua na kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. mijadala hii inarekodiwa katika video ambazo mtu yeyote anaweza kuziangalia, lakini mara nyingi lugha inayotumika katika mijadala hii ni kiingereza ,ili kuweza pia kuwafikia watu wengine duniani ambao kiingereza sio lugha yao, TED imeanzisha mpango wa kujitolea wa mtu yeyote kutafsiri video hizi kwenda katika lugha yake. Kwa upande wa kiswahili mwamko umekuwa mdogo sana, ukizingatia kutafsiri ni rahisi sana kwa mtu yeyote ambaye ana nia hiyo. kuna fursa mbalimbali ambazo TED wanazitoa kwa watu wanaojitolea kama kupewa nafasi za kuangalia mikutano ya TED live wakati inafanyika popote pale duniani. Kwa yule atapenda kufanya hivyo, tafadhali tembelea hapa , Translate | Participate | TED . jisajili na fuata maelekezo mafupi ili uweze kuanza kutafsiri.

​
 
ANGALIZO:Mawazo yanayoibuliwa kwenye video za TED ni mawazo yanayohusu
fani/nyanja mbalimbali za kitaalamu. Mfasiri atatakiwa awe mtu anayezifahamu istilahi za nyanja nyingi.Kiswahili
kinachotakiwa siyo kile cha 'vipi mwanangu, mshikaji ametia timu hapa?'.
 
ANGALIZO:Mawazo yanayoibuliwa kwenye video za TED ni mawazo yanayohusu
fani/nyanja mbalimbali za kitaalamu. Mfasiri atatakiwa awe mtu anayezifahamu istilahi za nyanja nyingi.Kiswahili
kinachotakiwa siyo kile cha 'vipi mwanangu, mshikaji ametia timu hapa?'.

Kutafsiri si kazi ambayo unaweza kuifanya kwa kuwa tu unafahamu lugha zote mbili, ni kazi ya kitaalamu ambayo inahitaji ujuzi wa pekee. Mfasiri yeyote anaelewa angalizo hilo na kamwe hawezi kuharibu kazi katika kiwango hicho...
 
Back
Top Bottom