Nafasi ya CHADEMA Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi ya CHADEMA Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanu Youthleague, Jun 23, 2012.

 1. T

  Tanu Youthleague Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanabodi kwa mara ya kwanza tangu CDM ianze kuwa na wabunge imekuwa ikishiriki vizuri katika vikao vya bunge na hasa uchambuzi wa bajeti. lakini mwaka huu imekuwa tofauti na imeonekana kuchuja sana na kati ya vigezo ni hivi

  1. Makosa ya wazi katika hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani ambayo imekuwa ikinadiwa kuwa ni bajeti mbadala. Makosa haya yalifichuliwa na mchumi daraja la kwanza Mwigulu Nchemba.

  2.Katika kuonyesha kuzidiwa Tundu Lissu wakati wa kujadili bajeti aliinuka na kutaka kutoa taarifa. Taarifa yake ikaonyesha kukana zile propaganda zilizokuwa zimefanikiwa kuwa huwa wanatoa bajeti mbadala. Lissu akasema ni makosa kuita maoni ya upinzani bajeti mbadala. Spika alikubali lakini swali je hii maana yake nini? Ukipekua hansard wabunge wengi wa chadema wakiwamo viongozi wametamka mara nyingi neno bajeti mbadala-umakini uko wapi? Kumbe wakizidiwa wanatafuta ukweli halisi.

  3. Hicho kinachoitwa mabadiliko ya baraza kivuli la mawaziri ni kituko (ni baraza dhaifu). Tafakari eti hii ndiyo timu ya serikali mbadala; Peter Msigwa (mropokaji) vs Hamis Kagasheki (Ambassador, Senior Diplomat); Said Arfi (mwanasiasa asiye na utalaamu wowote) vs Harrison Mwakyembe (Mwanasiasa na mwanataaluma mahiri na mzalendo); Wenje (mtengeneza fitina wa Mbowe-Nyamagana dhidi ya Chagulani) vs BM (Bernard Membe- gwiji wa diplomasia, mzalendo na mwanadekorasia aliyewalisha ugali Chadema (Lema, Millya) walipokwenda jimboni kwake Mtama. Mnyika (zero knowledge katika rasilimali za nishati (gesi) Vs Sospeter Muhongo (Profesa, mwanajiolojia-Lissu anamjua vizuri). Ni kwa ufupi tu. Pointi hapa ni kwamba kwa sababu Chadema ina watu dhaifu katika BARAZA KIVULI basi wangechukua wabunge wengine wa upinzani-ubinafsi umewaponza. Waziri kivuli ninaye mkubali ni Lissu (Katiba na Sheria).

  4. Katika Bunge hili imedhihirika Chadema hakuna wanachokisimamia kwa dhati bali ni usanii. Hii inathibitishwa na mwenyekiti wao Mbowe kupinga matumizi ya magari yakifahari (V8) yanayogharimiwa na fedha za umma lakini sasa amelichukua gari alilokataa. Hawa hawa ndiyo wanaojidai kupinga matumizi makubwa yasiyo ya lazima lakini nyongeza ya mishahara ya wabunge maana yake ni nyongeza ya matumizi (ya kibajeti), je, hoja yao ya fedha nyingi zitengwe kwenye miradi ya maendeleo ina ukweli?

  5. Wamepinga bajeti ya serikali ambayo ndani yake Waziri wa Fedha ameahidi kusaidia wakulima wa pamba kwa kuvipa unafuu wa kodi viwanda vya nchini vinavyozalisha kwa kutumia pamba ya ndani. Hii maana yake soko la pamba ya ndani litakuwa na uhakika bila kuyumbishwa na soko la dunia. Siasa za kanda ya ziwa ni zao la pamba, serikali itapendekeza kusaidia wakulima wa pamba, wao wanapinga bajeti. Hapa wamechemsha, na mchesho itakuwa umeiva vizuri na kunukia pale pamba itapokuwa na soko la uhakika la ndani kama waziri alivyoahidi. Watasikia kanda ya ziwa muda si mrefu.

  6.Wameshindwa kutekeleza kwa vitendo, kwa mwaka wa pili mfululizo kuonyesha uchambuzi wa kibajeti kuwa wanaweza kutoa elimu bure (shule ya msingi hadi form 6) kama alivyoahidi Slaa kwenye ilani yao, lakini pia wameshindwa kuainisha namna uchambuzi wao wa kibajeti unavyoweza kushusha bei ya saruji ili iuzwe kwa elfu tano kama alivyoahidi Slaa au angalau pungufu ya elfu 10.

  itaendelea
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Miaka 50 MAdini ccm inagawa bureee na kupokea vyandarua kwa mgongo wa bushi. Mwaka huu wa fedha unaoishia tumeshuhudia serikali ya jamaa dhaifu ikikopa mpaka ndani. Riba ya kukopeshana mashirika ya fedha na bank imepanda ghafla toka 4% mpaka 15%-18%. Nchi imeyumba nawe hapa watoa hoja za kiktoto. gari la Mbowe alilinunua yeye au amepewa atumie. Zile pesa za Stimulus Packages ziko wapi na wabunge wa chadema wamehoji sanaa na hakuna mahesabu yoyote. Sarakasi na uongo utawaua kabisa.
   
 3. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kwa mpumbavu kama wewe hakuna dawa. Mshauri DHAIFU aache kuzurura na bakuli nje ya nchi, abaki hapahapa na asimamie mapato ya humuhumu na hasa migodi na madini anayoyagawa kama uroda kwa wawekezaji wezi.
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Nothing new
   
 5. No admission

  No admission JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaweza kuwa na watu safi na wasomi wakubwa kabisa katika safu ya uongozi. Jambo kubwa linalotakiwa ni uadilifu. Swali: Hata kama hao mawaziri ni waadilifu watafanyaje kazi kwenye corrupt system? You may have a point but yet to be proven correct for more than 50 years. Kaa kimya wewe tanu
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  urgument za kitoto kafanye na watoto wenzio kule fb..yaani umejiunga JF specific kuchangia hilo au?
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtoa mada ni haohao GENGE LA WALAJI LA AKINA NGELEJA.DHAIIIIFUU
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Magamba tunawatambua hata kwa maneno yenu na si kwa vitendo tu!
   
 9. M

  Mzalendo K Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ameandika pointi ambazo haziwezi kufutwa kwa matusi au mabomu ya FFU, pointi zinafutwa kwa kuibua pointi nyingine "mbadala" ili sisi wengine tusio na upande tupime pumba na mchele. Wanacdm jitokezeni kujibu na si kuonyesha makosa ya upande mwingine huwezi kujidanganya eti unajibu hoja kwa kuonyesha makosa ya mshindani wako. Huo ni udhaifu. watu huru kifikra tunasubiri majibu!
   
 10. s

  sambamba Senior Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba hawana jipya
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata hivyo kiasi alichokwenda kuomba nje tr 1.4 na kilichopotea hapa kwetu ni tr 1.6 si bora angekaa hapa akachunga hizo tunazokusanya siziibiwe

   
 12. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Inawezekana unalitumia neno "pointi" bila kujua maana yake! sio kila neno linaloandikwa huwa linaitwa pointi.
   
 13. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Uchambuzi mzuri sana. Katika bajeti ya mwaka huu Magwanda wamechemka ile mbaya. Imekuwa ni aibu tupu.

  Somo la Wassira liliwaingia kiukweli, lakini kwa sababu msimamo wa kichama ni kuikataa bajeti, walisema 'hapana' kinyume na dhamira zao za kweli. Kumbuka jinsi walivyokuwa wanatikisa vichwa kuashiria vidonge vya Wassira kuwaingia.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tanu Youthleague umefunga kazi tazama majibu "0" yatakavyo miminika, hadi raha.
   
 15. y

  yaya JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nilitaka kuujadili na kuchangi kwa upeo wa akili yangu uzi huu uliouandika.
  Lakini niliposoma na kufikia hapo nilipopawekea wekundu nikagundua huna hoja ila unaleta ushabiki usio na maana. Nimemua niache niperuzi kwingine.
   
 16. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wanaccm hata mtoto mdogo anawazidi kwa hoja.
   
 17. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,668
  Likes Received: 16,608
  Trophy Points: 280
  Nimewaangalia wabunge wachadema tuongee kwa haki kabisa walikuwa wanatoa michango mizuri sana wanastahili pongezi.Kwanza ukiangalia umri wao mdogo na maeneo wanayogusa hakika walikuwa wazuri wala hawajchuja.Pili Tanuyouthleague sina uhakika kama kweli unaijua vizuri chama hicho cha vijana cha enzi hizo,kuna ibara moja kwenye katiba ya chama hicho inasema "Nitasema kweli daima fitina kwamngu mwiko"
  Angalia waliochangia mada wa CCM wameongea mapungufu makubwa ya bajeti na kuonyesho kutoweza kutekelezeka lakini mwisho wa siku kwa woga na unafiki uliokubuhu wanakubali hoja,kweli kabisa haiingii akilini mwa binadamu mwenye akili timamu.
  Tatu huwezi kuwa na experience kama hauna uthubutu.Sidhani kama kuwa waziri kivuli ni kupigana au kutukanana ila kusimami upande wa pili unafanyaje na waziri mwenye akili timamu na busara atakaribisha maoni na kukubali ideas za upande wa pili na pia kuwafundisha ni namna gani wizara inafanyakazi.
  Kuwa kijana au mzee hakumaanishi kuwa na uwezo mkubwa,ila mara zote kijana anachotakiwa ni kupokea ushauri mzuri anaopewa.Vijana jitokezeni kugombea nafasi hizi ni wakati wa kujifunza kuongoza nchi baadaye,siyo vijana wa Chadema tu hata vijana wa CCM.Tuwe protaifa na siyo provyama.
   
 18. B

  Bidders Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katumwa na mzee wa gombe wana hasira hawa cdm hatukuhitaji
   
 19. m

  mamajack JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  heee,kumbe nawewe ni mwehu.!!!!!!!

   
 20. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Join Date : 18th June 2012

  Posts : 1
  Rep Power : 0

  Likes Received 2

  Likes Given 0


  Nakufananisha na Simbachawene vile.... au nimekosea?? Umetumwa au unajituma?? Karibu JF napole kwa BAN
   
Loading...