Nafasi mbili za ‘UN Security Council’ ziko wazi. Je, Tanzania tumo?

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,477
2,000
UN Security Council ni sehemu muhimu sana , na kwa sasa kuna viti viwili vya Africa vitakuwa wazi ifikapo September 2019, Security council ndiyo Idara yenye nguvu sana ndani ya Umoja wa Mataifa, na uwepo wa nchi yoyote katika viti hivyo, kutawaletea manufaa nchini kwao kwenye mambo climate change, sustainable development and the region’s security.

Tanzania au nchi yoyote kuchukua hatua ya kuwa na nia ya kuchukua kiti kimojawapo, itakuwa jambo muhimu kwa nchi zinazoendele ndani ya huu mhimili muhimu duniani.

swali jee Tanazania na Iko macho kwa jambo hili, na wanafanya mikakati gani kufanikiwa, tunao watu wengi wenye uwezo wa kushikilia nafasi hii. wenzetu kenya weshaanza campaigne. Tanzania inaheshimika sana barani Africa na nina Hakika na kama tuna habari ya nyadhifa hizo kuwa wazi na tuna nia ya kuzipigania, basi tutaungwa mkono na nchi nyingi wanachama.

Kenya begins early campaign in bid to win seat on UN Security Council
https://www.nation.co.ke/news/Kenya...y-Council-seat/1056-5081808-a3xw30/index.html
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,590
2,000
Kwenye international community tumepotea, kiongozi wetu anaogopa kukaa meza moja na 'mabeberu'
 

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
13,694
2,000
Tanzania inaheshimika sana barani Africa ...
ungeandika "ilikuwa inaheshimika sana barani Afrika" Kati ya nchi zilizotuzunguka hivi sasa kuanzia Malawi, Msumbiji, Kenya, Zambia, Burundi, DRC, Rwanda, hata visiwa vya Comoro, ni ipi kati ya hizo inayotuheshimu kama zamani?
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,477
2,000
Nani Kakudanganya
Nimeishi miaka mingi njee na bado niko njee ya nchi. Tunaheshimika sana tena sana.

Ninazungumzia kama nchi na wananchi wake, tofautisha kati ya nchi na unavyofananisha mawazoni mwako.

Tanzania ni mchi nzuri na yenye watu wazuri.
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,477
2,000
ungeandika "ilikuwa inaheshimika sana barani Afrika" Kati ya nchi zilizotuzunguka hivi sasa kuanzia Malawi, Msumbiji, Kenya, Zambia, Burundi, DRC, Rwanda, hata visiwa vya Comoro, ni ipi kati ya hizo inayotuheshimu kama zamani?
Zote isipokuwa kenya na Malawi, waliobakia wote hawataweza isahau Tanzania kwa msaada wake.

Inapokuwa mambo ya nchi tywache ushabiki wa kisiasa
 

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
13,694
2,000
Zote isipokuwa kenya na Malawi, waliobakia wote hawataweza isahau Tanzania kwa msaada wake.
Umefuatilia mahusiano ya kidplomasia siku za hivi karibuni kati ya Tanzania na majirani zake?

Kenya wanasema ni kwa nini wanataka kuwemo, jee hoja ya sisi kutaka kuwepo ni ipi?
 

sijalih

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
601
500
Kama kuna kuulizana maswali hasa ya haki za binadamu,utawala bora na uhuru wa vyombo vya habari, tusijaribu tutaaibika vibaya
 

Bobwe2

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
2,450
2,000
"Tumeibiwa sana na mabeberu" alisikika mzee mmoja mwenye upara mitaa ya lumumba.
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,217
2,000
Nimeishi miaka mingi njee na bado niko njee ya nchi. Tunaheshimika sana tena sana.

Ninazungumzia kama nchi na wananchi wake, tofautisha kati ya nchi na unavyofananisha mawazoni mwako.

Tanzania ni mchi nzuri na yenye watu wazuri.
Mpuuzi wewe,unadhan nje ya nchi unaishi peke yako ?
Umefanya research au na wewe Una air your groundless thoughts
 

Zigi Rizla

JF-Expert Member
May 25, 2019
1,014
2,000
'Tanzania tunaheshimika sana nje ya nchi'
Screenshot_20200618-205046.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom