Nafanya Tafakari..!

mndumsolo

Member
Feb 11, 2011
51
8
Nafanya tafakari....
Naiona nchi yenye maziwa na asali...
Naona viongozi wake wasiojali...
Bila huruma wakijitafunia za wote rasilimali.!

Naona wananchi wake maskini..
Wengi wao wakiwa bado usingizini..
Nawaona wachache wakiwa katika maamkizi..
Wakizinduana toka wa muda mrefu usingizi.!

Naona baba na mama wakitazamana..
Nawaona wakishauriana nini cha kufanya..
Juu ya shida lukuki zinazowaandama..
Juu ya njaa na umaskini unaowaandama.!

Naona wananchi wenye nyingi hasira..
Kwa makundi makundi wakiwa..
Kwa jazba wakijiambia..
Ukingoni mambo yamefikia.!

Nawaona wakiwa tayari tayari..
Barabarani au msituni kuingia..
Haki zao kudaia..
Njaa yao na watoto wao kuondolea.!
 
Back
Top Bottom