markbusega
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 826
- 850
Unawasiwasi gani wakati mshenga yupo atakayeongea kila kitu
Ukweni ni pahala pa heshima......hivyo unapaswa ujiheshimu uwapo huko......
-Jizuie kuwa muongeaji sana....hasa katika masuala ambayo hayakuhusu.....
- Jitahidi kutofautisha kati ya masuala yao ya kifamilia na mambo yanayokuhusu wewe.....
- Jitahidi kufuata sheria na taratibu za hapo hata kama zingine zinakera na kuudhi kwani hapo upo kwa muda tu
- Ficha udhaifu wako na aibu zako uwapo ukweni.....hapa namaaanisha kuwa kama wewe ni mtu wa pombe jitahidi sana kujizuia.....kwani unaweza ukasemaa unaonja matokeo yake ukapitiliza ukaja ukampiga busu mama mkwe au shemeji yako ukidhani ni mkeo......
-Jitahidi kuuzuia moyo na tamaa za kijinga.....sio tena unamuona shemeji yako katoka kuoga unaanza kutoa macho.....
Ni hayo tu....mengine utayakuta huko huko
Gonga viloba 3 vya konyagoWakuu,
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Baada ya masiku tele kupita, Leo nd'o naenda kutambulishwa ukweni kwa mara ya kwanza kabisa. Nasikia ukoo mzima umekusanyika huko, kuanzia akina babu, bibi, baba, mama, mjomba, shangazi, mashemeji wa kike na wa kiume na ndugu wengine.
Sasa hapa najiona kama moyo nimeuazima, yaani unadundadunda balaa, akili zinazunguka, kichwa kinanesanesa, miguu inapepesuka, sijanywa hata chai ila najihisi nimeshiba kinoumah, jasho linatiririka balaa, mikono yote imelegea,
hadi midomo inatetema na nimevaa ile kanzu yangu matata ninayoitegemea kwenye matukio muhimu ila bado mwili mzima najiona kama vile nipo uchi.
WAKUU,
NIPENI EXPERIENCE NA NAMNA YA KUONDOA HII HALI YA HOFU NA UOGA KWA M'LIOWAHI KWENDA UKWENI KWA MARA YA KWANZA WAKUU.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Piga viroba kadhaa na msokoto mmoja, ukifika wote utawaona kama katuni tu utakuwa unacheka tu