Seneta Wa Mtwiz
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 3,622
- 4,138
Wakuu,
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Baada ya masiku tele kupita, Leo nd'o naenda kutambulishwa ukweni kwa mara ya kwanza kabisa. Nasikia ukoo mzima umekusanyika huko, kuanzia akina babu, bibi, baba, mama, mjomba, shangazi, mashemeji wa kike na wa kiume na ndugu wengine.
Sasa hapa najiona kama moyo nimeuazima, yaani unadundadunda balaa, akili zinazunguka, kichwa kinanesanesa, miguu inapepesuka, sijanywa hata chai ila najihisi nimeshiba kinoumah, jasho linatiririka balaa, mikono yote imelegea,
hadi midomo inatetema na nimevaa ile kanzu yangu matata ninayoitegemea kwenye matukio muhimu ila bado mwili mzima najiona kama vile nipo uchi.
WAKUU,
NIPENI EXPERIENCE NA NAMNA YA KUONDOA HII HALI YA HOFU NA UOGA KWA M'LIOWAHI KWENDA UKWENI KWA MARA YA KWANZA WAKUU.