Naenda ukweni kwa mara ya kwanza

Naenda ukweni kwa mara ya kwanza

Hahahah Mimi nilienda kama IGP anaeenda kusaka wauza unga sikuogopa mtu wala kitu ,ila nafurahi nimepokelewa kama mfalme.

Ila nakushauri kama hukupata choo kubwa nenda chooni ujaribu kama itatoka unaweza kuhara mbele ya mdahalo
 
Kumbe serikali hawakukosea kurudisha zoezi la kwenda JKT baada ya kuhitimu form six, mwanaume utakuwaje muoga kiasi hicho kwa issue ndogo kama hicho?
Jkt kwani anaenda kupambana nao huko??......cha msingi ni confidence tu
 
Mwambie mpambe akutafutie viroba!!
Harafu fanya kama unatoka kuongea na simu, tandika viroba vyako vi4 fasta fasta rudi ndanj!!
Break ya kwanza utaenda kugonga tano na babako mkwe! Umemaliza mchezo !
 
Kuvaa kanzu is totally kujiweka off,,unless ndo vazi lako la kila siku...be real,vaa unavovaaga ilimradi ni ki-heshima..
 
Jijaze tu ni binadamu wenzio , weka heshima mbele, Salimia utakao wakuta kutokana na rika lao usipokuwa makini unaweza mwambia mtoto shikamoo
 
Anaogopa yawezekana akapangiwa mahari kubwa kuliko uwezo alionao.Jipange mkuu.
 
Katika thread zilizowahi kunifurahisha hii ni mojawapo....big up mleta Uzi ..maana Mimi mwenyewe nategemea kwenda ukweni mwaka huu....isitoshe mke wangu huwa anatoa taarifa ukweni pale tunapokosanaga ...!!???
We naye umeamua kuanzisha ka sub thread kako kwene thread ya mwenzio
 
Ukweni ni pahala pa heshima......hivyo unapaswa ujiheshimu uwapo huko......

-Jizuie kuwa muongeaji sana....hasa katika masuala ambayo hayakuhusu.....

- Jitahidi kutofautisha kati ya masuala yao ya kifamilia na mambo yanayokuhusu wewe.....

- Jitahidi kufuata sheria na taratibu za hapo hata kama zingine zinakera na kuudhi kwani hapo upo kwa muda tu

- Ficha udhaifu wako na aibu zako uwapo ukweni.....hapa namaaanisha kuwa kama wewe ni mtu wa pombe jitahidi sana kujizuia.....kwani unaweza ukasemaa unaonja matokeo yake ukapitiliza ukaja ukampiga busu mama mkwe au shemeji yako ukidhani ni mkeo......

-Jitahidi kuuzuia moyo na tamaa za kijinga.....sio tena unamuona shemeji yako katoka kuoga unaanza kutoa macho.....

Ni hayo tu....mengine utayakuta huko huko
Paragraph before the last one[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom