Mkuu pole sana, najua hali unayopitia. Tena yaweza kuwa mbaya kuliko unavyoelezea hapa.
Binafsi nakushauri, kwanza punguza 'matarajio' makubwa. Usijilazimishe kufanya kazi mpaka ulipwe Tsh 20,000 au zaidi kwa siku.
Mimi niliwahi kwenda kuomba kazi kwa vijana waosha magari, tena nilitaka niwasaidie tu bila malipo ila wawe wananipa Tsh 1,000 tu lakini walikataa. Tena wakati huo nimetoka chuo !!
Kama huna ulemavu wowote, mzima wa afya kwanini usijishkize kwenye makampuni ya ulinzi wakati unajipanga taratibu. Tena usiende makampuni makubwa, nenda kwa hizi local companies unaweza kupata kazi siku hiyo hiyo.
Ingawa wanalipa Tsh 150,000 au less lakini ukikaa nyumbani utaipata wapi hata hiyo.