Nadharia tatu kutekwa kwa Mohammed Dewji

Nadharia tatu kutekwa kwa Mohammed Dewji

mawazomgala

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
342
Reaction score
212
Na Mwandishi Wetu
UTEKAJI wa watu maarufu barani Afrika imekuwa ni suala la kawaida hasa kutokana na kuanza kuja kwa kasi kubwa tofauti na awali, ambapo suala hili lilionekana kuwa ni kitu cha hatari kutokana na teknolojia ilivyokuwa awali, imefichuka.

Hali hiyo inatokana na watu hao, wanaolengwa ni wafanyabiashara maarufu kutekwa mara kwa mara huku suluhu yao ikiwa ni kutoa kitu kidogo kutoka kwa watu hao, ambao wamekuwa na sababu zao mbalimbali wanazokuwa nazo.

Jamvi la Habari, limekuja na uchunguzi unaonyesha kuwa makundi matatu yanayohisiwa huenda yakawa ni miongoni mwa watu waliohusika na kufanya kitendo hicho cha kutekwa kwa mfanyabiashara huyo, ambaye amekuwa na mafanikio makubwa ya kibiashara.

Sababu hizo tatu ambapo wahisiwa wakuu watatu, moja wanaweza wakawa maharamia waliobadilika na kuingia kwenye mtindo wa watekaji watu ili waweze kujipatia fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo, sababu nyingine ni wafitini na wachonganishaji wanaotumia matukio ya kupotea kwa watu na wao kufanya hivyo.

Sababu nyingine ya tatu ni inatajwa huenda wakawa wabaya wake wa kibiashara wale wanaofanya naye biashara au aliofanya nao biashara zamani, kupitia kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (METL), ambapo hapa imegawanyika makundi mawili inaweza ikawa yeye binafsi au baba yake Gullam Dewji, ambao wamekwaruzana.

Taarifa zimeelezwa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, maarufu Mo, ambaye pia ni mmoja wa wanahisa wanaomiliki klabu ya Soka Tanzania, Simba kwa asilimia 49 pamoja na kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises, alitekwa juzi saa 11 alfajiri alipokuwa anajiandaa kufanya mazoezi katika klabu ya mazoezi ya Colloseum iliopo Oysterbay, mjini Dar es Salaam.

Sababu ya maharamia inapewa asilimia 60.
Hii ni sababu moja kubwa, ambao wataalamu wa intelejesia ya nchi wanapaswa kuwa nayo makini hasa kutokana na mfumo ulioingia sasa wa utekaji wa wafanyabiashara wakubwa ili waweze kujipati fedha mbalimbali.

Jamvi la Habari, limepata taarifa kuwa watu wanaofanya shughuli za utekaji huu ni watu wenye ueledi mkubwa wa matukio ya kijinai na wanafanya shughuli hizo kwa ustadi mkubwa ikiwemo kumfuatilia mtu kwa muda mrefu, huku muda mwingine wakishirikiana na watu wa karibu wa mfanyabiashara tajiri wanayetaka kumteka ili wapewe kiasi kikubwa cha fedha.

Hii inatokana na tukio la MO, linafanana matukio mengine matano ya utekaji ya watu maarufu, ikiwemo tukio la kwanza la kutekwa mfanyabiashara maarufu mjin Maputo, Msumbiji April 22, 2018 nje ya hoteli maarufu ya Gloria Hotel.

Mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiasia (Jina lake lilifichwa) alitekwa akiwa nje ya hoteli hiyo na kuambiwa awapigie simu ndugu zake atoe kiasi kikubwa cha fedha na kufichwa katika nyumba zilizo jirani na hotel aliyotekwa.

Katika tukio hili, watekaji wa mfanyabiashara huyu saa 11 alfajiri walihitaji kulipwa jumla ya Dola za kimarekani 162,000 sawa na wastani wa Sh 368,000,000 za kitanzania, ambapo kabla ya kufanikiwa kupewa fedha hizo, watekaji walikamatwa na walipobanwa walieleza mchezo mzima ikiwemo kuwepo na mtu wa karibu wa mfanyabiashara huyo, waliyeshirikiana naye.

Taarifa zaidi za tukio hilo ziliwekwa wazi kwenye mtandao wa gazeti maalumu la Msumbiji, ambapo linapatikana kupitia Police rescue Indian kidnap victim in Maputo - AIM report huku pia tukio lingine likiwa limetokea Lilongwe nchini Malawi, ambapo pia mfanyabiashara Atul Manek alitekwa.

Atul naye alitekwa alfajiri akiwa anatoka nyumbani kwake, nje ya nyumba yake iliyopo eneo wanaloishi watu mashuhuri liitwalo Area 9 mjini Lilongwe, ambapo watekaji waliomteka Atul mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na anayesimamia kampuni kubwa kubwa Malawi na Afrika kwa ujumla walitaka fedha ili wamuachie.

Walimshikilia kwa muda mrefu hadi familia yake ilipolipa kiasi cha Dola 1,000,000 sawa na zaidi ya Sh bilioni 2.2 (2,280,000,000/=), ambapo watekaji hao waliielekeza familia na wasaidizi wake mahala pa kwenda kuiweka fedha hizo na walipohakikisha wameziona walimuachia huru.

Taarifa zaidi iliwekwa kwenye mtandao wa gazeti la Malawi linaloitwa Nyassa Time na inapatikana pia katika mtandao wa https://gossipier.com/malawi-police...ok-atul-manek-in-lilongwe-malawi-nyasa-times/.

Pia, tukio lingine ni kutekwa kwa mfanyabiashara kwenye jiji la Cape Town, Afrika Kusini, ambapo walimteka mfanyabiashara Liyaqat Parker mwenye umri wa miaka 65, ameachiwa kutoka kwa watekaji Septemba 18, mwaka huu baada ya kushikiliwa na watekaji kwa zaidi ya miezi miwili mfululizo.

Maharamia waliomteka mfanyabiashara huyo walitaka walipwe jumla ya Randi Milioni 3.4 za Afrika Kusini sawa na zaidi ya sh. Milioni 532,766,221 za kitanzania, soma zaidi kwenye link hii Kidnapped Cape Town businessman released

Pia, tukio lingine la tano lilitokea katika jiji la Durban, Afrika Kusini ambapo mfanyabiashara mwengine maarufu nchini humo Sikhumbuzo Mjwara, aliripotiwa kutekwa Agosti 30 mwaka huu nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Verulam jijini Durban.

Mfanyabiashara huyo anayemiliki mgahawa maarufu wa Barrio Restaurant uliopo Umhlanga‚ anasimamia pia biashara kadhaa nchini humo, ambapo hadi sasa haijulikani alipo huku jitihada za kuokoa maisha yake zinaendelea. Soma zaidi kwenye link hii Hunt continues for 'kidnapped' Durban businessman.

Sababu hii inapewa nafasi kubwa na ina asilimia 60 kutokana na mfumo uliopo sasa kwa maharamia hao, kuja na mfumo mpya wa utekaji wa watu ili waweze kujipatia fedha, kutokana na kazi za uharamia wa utekaji meli kushindikana kama zamani.
Kuwepo kwa matukio ya utekaji watu na uchonganishaji inapewa asilimia 20

Wafitini na wachonganishaji wanaotumia matukio ya kupotea kwa watu na wao kutengeneza la kwao ili waweze kuichonganisha serikali na watu na kuonekana kuwa nchi haina usalama na ndio maana tukio hili limekuwa likishikiriwa sana na vyombo vingi vya habari.

Jamvi la Habari linaamini hii inapewa asilimia 20, hasa kutokana na watu wasioitakia mema nchi, kuamua kuingia katika mfumo mwingine wa kuichafua nchi hasa kutokana na utendaji kazi unaofanywa kwa umakini mkubwa na serikali ya awamu ya tano kuwatumikia watanzania kwa kukuza uchumi wa nchi.

Uwepo wa matukio ya utekaji nyara watu unaochipuka kidogo kidogo nchini, na unafanywa na watu wasioitendea mema nchi kufanikiwa kujipenyeza katika mgongo wa matendo ya ovyo ili waweze kujinufaisha na watu hao wanaouwezo wa kutenda tukio hilo ili kuonyesha nchi sio salama.

MO ni mtu mkubwa na aliyefanikiwa kibiashara, hivyo malengo ya watu wanaotaka kumdhuru lazima wawe makini na ndio maana suala lake limekuwa na msukumo mkubwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ambavyo vimekuwa vikiripoti tukio hili.

Hili ni eneo ambalo watu wa upelelezi wanaofuatilia suala hili, wanapaswa kulitazama kwa umakini mkubwa ili waweze kuja na majawabu makubwa ya kuondoa tatizo hili na kulikomesha kabisa suala la kutekana watu nchini.

Pia, ukitazama kwa umakini na utangazaji wa tukio hilo ni kama baadhi ya vyombo vilijiandaa kwenye tukio hili, na jamii haipaswi kudharau kwa kuwa nchi imekuwa mstari wa mbele katika vita ya uchumi.

Lazima tung’amue mambo. Sikatai kuwa watekaji wanaweza kuwa wahuni wanaotaka hela lakini hebu tusijifungie kwenye bakuri. Let’s look beyond. Si mmesikia ushahidi wa awali kuwa waliohusika ni raia wa kigeni(wazungu).Lazima tutafakari.

Hebu tizama, kwa tukio hili tu tayari baadhi ya balozi haraka zimewatahadharisha wageni wa kada za utalii na uwekezaji, waliopo nchini na wale wanaotaka kuja kuhusu usalama Tanzania.

Vita ya uchumi kote duniani ilikofanyika imeacha mtikisiko.Wapo walioitwa magaidi, walioitwa madikteta, walioitwa wavunjaji wa haki za binadamu, na waliovurugiwa nchi zao kabisa kwa matukio ya kupangwa na intelijinsia za kiwango cha juu kabisa.

Tukio hili linavyotangazwa na media za kimataifa ni dhahiri taswira ya nchi inalengwa. Na hiyo inatokana na nchi kuwa mstari wa mbele katika kukuza uchumi wake, ili jamii iweze kufika mbali zaidi na kuwa na mafanikio makubwa.

Ninachotaka kusema vyombo vya dola na taifa tulitazame hili tukio kwa sura kubwa. Misimamo yetu mipya na mikali katika rasilimali inaweza kupelekea matukio ya aina hii ili tuyumbe hasa pia uwepo wa matukio madogo madogo ya utekaji.

Hakuna ugeni duniani katika matukio ya kuteka, kujeruhi kwa silaha, kufadhili makundi ya kigaidi, kuibua hisia za ukabila na udini na hatimaye vita ya wenyewe kwa wenyewe, kuua hasa viongozi na watu maarufu pale adui anapotaka kumtikisa aliyegusa maslahi yake. Mifano ipo mingi.

Watu wenye uhasama na Mo wanapewa asilimia 20.
Katika mafanikio yeyote lazima kuwepo na vita, hakuna ubishi Mo ameikuza na kuitengeza Mohammed Enterprises hasa baada ya baba yake, Gullam Dewji kumkabidhi madaraka ya uendeshaji wa kampuni hiyo ya kifamilia.

Mafanikio hayo hadi kumfanya Mo kuwa bilionea kijana zaidi Afrika, ni mafanikio makubwa, ambayo mapito yake, amepitia kwenye mambo mengi ikiwemo vita ya kibiashara, hivyo ni wakati wa Polisi kuanza na watu wote waliofanya biashara na mfanyabiashara huyo.

Kukamatwa kwa watu huo, kutakuwa ni mwanzo mzuri wa kufahamu mambo mengi zaidi kuhusiana na kutekwa kwa mfanyabiashara huyo, aliyekuwa na mafanikio makubwa katika muda mfupi toka alipotekwa juzi na wazungu wawili na tukio hilo linapewa asilimia 20 huenda likawa ni sehemu ya sababu ya kutekwa kwa M0.
 
Zakari naye kidogo atekwe,sema akawa na silaha ndipo mambo yalivyoharibika!Mbona kundi hili hujalitaja?Kundi hili linasemwa sana huku mtaani kuwa ndio limeshiriki!
 
Takwimu zenu za kupikwa hizo hatuzihitaji " Maana ukweli una fahamika
 
Back
Top Bottom