Nadhani bado sijaelewa kuhusu hii kodi ya majengo

Duuuu mkuu pole sana soma paka mwisho kina sehemu wamesema tadhari usipo lipa kwa muda watakusanya kwa nguvu

Wadau hebu tujiongeze na tusijitoe ufahamu mbona bia na sigara waziri akipandisha hatusemi bei zianze mara moja? Tuache kujitoa ufahamu.Waziri katoa mapendekezo na mpaka bunge wajadili wakipitisha kuanzia Julai,2017 ndiyo itakuwa utaratibu.Je angesema laki 5 ungesema barua uliyopewa ineandikwa 90,000 hivo unataka ongezea kikichopungua?Wewe kalipe tu.Nachojua wazee wa miaka 60+ wenye nyumba mmoja ambayo siyo ya biashara wamesamehewa na walemavu wasiokuwa na shughuli ya kuwaingizia kipato nao wamesamehewa.
 
Sasa kama kila mkoa una rates zake kulikuwa na sababu gani kwa waziri kusoma bungeni, maana nilidhani ameipeleka bungeni kama kiwango cha kitaifa
Nadhani alisoma kuashiria kwamba sheria iawataka TRA kufanya makusanyo kwa niaba ya serikali za mitaa....ila kiutaratibu kodi ya majengo inatakiwa ilipwe kwa kuangalia thamani ya jengo, kwa kuwa kufanya tathimini inakuwa issue kila halmashauri inakuwa na rate zake ambazo ni flat rate ila halmashauri nyingi ni 20,000 though kuna ambazo zina 10,000, 15,000 na nyingine zaidi ya 20,000.

Ila kwa TRA tutalia sana na kitakachotokea itakuja kurudishwa halmashauri au kuangalia utaratibu mwingine kama walivyofanya Road licence maana wao wanachojua ni kutoza riba tu ukichelewa kulipa na kwenye nyumba watagusa wengi ambapo unakuta mtu kalimbikiza deni anadaiwa milion alafu hela hana. Pamoja na kwamba wanasema watauuza jengo lakini bado haiingii akilini
 
a64ec4ce61795972e1e53a8b5b3bafd3.jpg
wakuu nimerudi kazini nakutana na barua kutoka TRA kulipa kodi ya majengo tatizo nyumba yangu ni yakuishi tu naambiwa nilipe 90000 juzi serikali si ilisema nyumba za chini ni elfu kumi hii 90000 inakuwa aje tena na mikoa mingine nayo ni hivi hivi au ni huku mwanza tu
Mpaka Arusha ni ivyo
 
Wadau hebu tujiongeze na tusijitoe ufahamu mbona bia na sigara waziri akipandisha hatusemi bei zianze mara moja? Tuache kujitoa ufahamu.Waziri katoa mapendekezo na mpaka bunge wajadili wakipitisha kuanzia Julai,2017 ndiyo itakuwa utaratibu.Je angesema laki 5 ungesema barua uliyopewa ineandikwa 90,000 hivo unataka ongezea kikichopungua?Wewe kalipe tu.Nachojua wazee wa miaka 60+ wenye nyumba mmoja ambayo siyo ya biashara wamesamehewa na walemavu wasiokuwa na shughuli ya kuwaingizia kipato nao wamesamehewa.
Unajua ulichoandika hapa kweli au
 
Nawaombeni ndugu zangu ufafanuzi wa kulipia ardhi, nilinunua robo eka nje ya mji na nimejenga kibanda cha vyumba viwili na nimelipia jengo, sasa swali langu je hicho kipande cha ardhi nalipia wapi na ni kiasi gani naomba ufafanuzi.
 
Kila Nyumba Ina Kodi Yake Hapo Ndo Wamebugi Walitakiwa Waseme Za Ghorofa Kiasi Hiki Na Zisizo Za Ghorofa Kiasi Hiki
 
Hii kodi ndio itakayowaangusha CCM kodi haieleweki imechukuliwa kwa vigezo gani. Lazima hii kodi iangaliwe upya la sivyo haitawaacha watu salama
 
Mkuu mm wamenipa mbili ya pili ni barua tu alafu wameandika limbikizo la kodi ya nyuma ni sifuri na pia nyumba siyo ya biashara ni yakuishi tu
Kabla ya kuandikiwa hiyo bill kuna fomu ya kujaza kuelesea status ya nyumba ie Aina ya matofali,paa, Dari, sakafu, milango, kuta (rangi ) miundo mbinu (maji umeme simu) bustani, fence nk.
Hivyo gharama itatokana na ubora na thamani ya jengo lako. Idadi ya vyumba nk.
Hata hivyo 90,000/12 just peanut (maguuz voice)
 
Si bora wewe Mimi Niko Tabora nililetewa kalatasi nikalipie 200,000
In nyumba kuishi tena sins hats mpangaji siendi kulipa nasubiri watakacho kuja kufanya
Usikate tamaa. Andika barua kwa tra regional manager wako ukomplain.
 
Nawaombeni ndugu zangu ufafanuzi wa kulipia ardhi, nilinunua robo eka nje ya mji na nimejenga kibanda cha vyumba viwili na nimelipia jengo, sasa swali langu je hicho kipande cha ardhi nalipia wapi na ni kiasi gani naomba ufafanuzi.
Unayo hati ya ardhi?
Kodi ya jengo utalipa.
 
Nadhani alisoma kuashiria kwamba sheria iawataka TRA kufanya makusanyo kwa niaba ya serikali za mitaa....ila kiutaratibu kodi ya majengo inatakiwa ilipwe kwa kuangalia thamani ya jengo, kwa kuwa kufanya tathimini inakuwa issue kila halmashauri inakuwa na rate zake ambazo ni flat rate ila halmashauri nyingi ni 20,000 though kuna ambazo zina 10,000, 15,000 na nyingine zaidi ya 20,000.

Ila kwa TRA tutalia sana na kitakachotokea itakuja kurudishwa halmashauri au kuangalia utaratibu mwingine kama walivyofanya Road licence maana wao wanachojua ni kutoza riba tu ukichelewa kulipa na kwenye nyumba watagusa wengi ambapo unakuta mtu kalimbikiza deni anadaiwa milion alafu hela hana. Pamoja na kwamba wanasema watauuza jengo lakini bado haiingii akilini

Mimi nilidhani wameweka flat rate kwa nyumba zisizo na ghorofa 10,000 na zile zenye ghorofa 50,000 kila ghoroga, kuna ndugu mmoja anasema amekuwa anatozwa 360,000 kwa mwaka kwa nyumba isiyo na ghorofa na watu wa mapato walimwambia wanataka kiwango hicho kwakuwa inatumika kwa biashara, sasa hizi double/triple standards zinatofautiana na kusababisha mkanganyiko kwa walipa kodi, ingefahamika tu kwamba nyumba ni ya biashara rates ni kiasi fulani, nyumba ya kuishi kiasi fulani kwa nchi nzima
 
Mimi nimeletewa inayodai shs 157,000/- badala ya 50,000/- kwa nyumba ya kuishi ya ghorofa moja . Nimeuliza kulikoni nimejibiwa hiyo 50,000/- inaanza July mosi . Hivyo nikalipe hiyo 157,000/- niliyoletewa . Je , ni sawa wakuu ?
 
Kila Nyumba Ina Kodi Yake Hapo Ndo Wamebugi Walitakiwa Waseme Za Ghorofa Kiasi Hiki Na Zisizo Za Ghorofa Kiasi Hiki

Waziri amesema hilo, lakini wadau wengine wanasema viwango vinapangwa na Halimashauri, sasa swali linakuja viwango alivyotaja waziri ni vya wapi na vile vya halimashauri vinatoka kwenye mwongozo gani
 
Mimi nimeletewa inayodai shs 157,000/- badala ya 50,000/- kwa nyumba ya kuishi ya ghorofa moja . Nimeuliza kulikoni nimejibiwa hiyo 50,000/- inaanza July mosi . Hivyo nikalipe hiyo 157,000/- niliyoletewa . Je , ni sawa wakuu ?

Wangefanya kama road license tu kila kitu kianze upya maana inachanganya sana na hii itawafanya watu kuibiwa mno ukizingatia mambo ya receipt za kuandika kwa mkono kama za barabarani
 
Dhumuni la kodi hii ni kugharamia huduma za jamii zinazotolewa na serikali kama barabara, kuzoa taka, zimamoto nk. Ilitakiwa serikali ianze kwanza kutoa huduma hizi ndio kisha itoze Raia wake kodi. Sasa imekuwa kinyume kwake. Ila hela ya kununulia ndege ipo!
 
Mimi nimeletewa inayodai shs 157,000/- badala ya 50,000/- kwa nyumba ya kuishi ya ghorofa moja . Nimeuliza kulikoni nimejibiwa hiyo 50,000/- inaanza July mosi . Hivyo nikalipe hiyo 157,000/- niliyoletewa . Je , ni sawa wakuu ?
Mkuu mm sitolipa nitazungushana nao
 
Mimi nilidhani wameweka flat rate kwa nyumba zisizo na ghorofa 10,000 na zile zenye ghorofa 50,000 kila ghoroga, kuna ndugu mmoja anasema amekuwa anatozwa 360,000 kwa mwaka kwa nyumba isiyo na ghorofa na watu wa mapato walimwambia wanataka kiwango hicho kwakuwa inatumika kwa biashara, sasa hizi double/triple standards zinatofautiana na kusababisha mkanganyiko kwa walipa kodi, ingefahamika tu kwamba nyumba ni ya biashara rates ni kiasi fulani, nyumba ya kuishi kiasi fulani kwa nchi nzima
Bora flat rate, mie huwa nalipa 20,000 kwa mwaka tangu 2010, nina mashaka kwa ujio wa TRA naweza nikabambikiwa maana halmashauri ilikuwa unakwenda kumwona mtu lakini TRA unapambana na mfumo ili uweze kuweka sawa kunakuwa na mlolongo mrefu...ngoja na mie nifuatilie ila TRA wametoa template inayoonyesha ada kwa kila mkoa / halmashauri. Hiyo 360,000 nadhani anatakiwa afuatilie ama kama kuna wajuzi wa mambo watufafanulie maana kama jengo linatumika kwa biashara linakodi yake nadhani ni 10% ya kodi ya pango ya kila frame ama chumba na kama ni jengo lote linatumika kwa biashara yaani kama mtu amepanga ni 10% ya kodi ya pango (sina uhakika ila nifahamu kuna kitu kama hicho sas unapokuja kucharge 360,000 kwa kigezo cha inatumika kibiashara hapo kuna ukakasi)
 
Kabisa Mkuu
 
Back
Top Bottom